SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Hizo nakala za masomo hao watahiniwa walipewa vipi bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti, ina maana zilitolewa kinyemela?

Kuna mtu alikula pesa hapo, naamini atakuwa alishapoteza kazi muda mrefu, ila kama yupo ofisini itakuwa ni maajabu..

Na hao watahiniwa ni kama hawaamini walitoka salama, wanaonekana hawajiamini, ndio maana wameingia mitini wasije zirudisha waambiwe walifeli masomo mawili wanatakiwa kuyarudia.
 
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kimewafutia shahada Madaktari 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha St Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015-2019.

Notisi kwa Umma iliyochapishwa katika Gazeti la Daily mnamo Jumatatu (27 Machi, 2023), ilisema wahitimu 162 walikataa kimakusudi kurudisha nakala za masomo, 'Transcript' walizopewa bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu licha ya kukumbushwa kwa muda mrefu

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa seneti ya SAUT Balozi Prof Costa Mahalu inaeleza uamuzi wa kuondoa shahada hiyo umekuja baada ya kikao cha Seneti cha Chuo Kikuu kilichofanyika Februari mwaka huu.

"SAUT kupitia Seneti ya Chuo Kikuu katika Seneti yake ya 54 isiyo ya kawaida, mkutano uliofanyika tarehe 25 Februari 2023 katika chuo kikuu cha SAUT ina kwa mujibu wa Kifungu cha 47(1) & (2) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sheria Na. 7 ya 2005 ikisomwa pamoja na Vifungu. 6(3)(ii), 7,8 na Kanuni ya 29 (1) ya Mkataba wa SAUT GN. HAPANA. 580 ya 2020 ilifuta shahada walizopewa wahitimu 162 wa Madaktari wa Udaktari wa SFUCHAS kuanzia 2015 -2019,” inasomeka taarifa hiyo.

Source: Daily News
Wao ndio wazinguaji kwanini watoe transcript bila ufahamu, hii nchi bado vituko vinaendelea.
 
tukiacha kila mtu afanye anavyofikiria kichwani mwake mambo hayataenda.taratibu ziko wazi fuata kuepuka usumbufu na kama unadhani degree ni kile tu kilichopo kichwani kazi kwako kama utatumia kichwa kuomba kazi.
Mkuu elewa mambo yalivyo, huo Ni uzembe wa kimamlaka hadi kufikia unampa mtu cheti maana yake ushahakiki Mchakato!! Na cheti hakiwezi kutolewa Mara mbili mbili utakuwa uhuni tu..

Transcript nikirudisha then unaweka matokeo mapya umeyatoa wap!! Na Ni miaka 7 Sasa huo ni uhuni tu...
 
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kimewafutia shahada Madaktari 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha St Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015-2019.

Notisi kwa Umma iliyochapishwa katika Gazeti la Daily mnamo Jumatatu (27 Machi, 2023), ilisema wahitimu 162 walikataa kimakusudi kurudisha nakala za masomo, 'Transcript' walizopewa bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu licha ya kukumbushwa kwa muda mrefu

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa seneti ya SAUT Balozi Prof Costa Mahalu inaeleza uamuzi wa kuondoa shahada hiyo umekuja baada ya kikao cha Seneti cha Chuo Kikuu kilichofanyika Februari mwaka huu.

"SAUT kupitia Seneti ya Chuo Kikuu katika Seneti yake ya 54 isiyo ya kawaida, mkutano uliofanyika tarehe 25 Februari 2023 katika chuo kikuu cha SAUT ina kwa mujibu wa Kifungu cha 47(1) & (2) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sheria Na. 7 ya 2005 ikisomwa pamoja na Vifungu. 6(3)(ii), 7,8 na Kanuni ya 29 (1) ya Mkataba wa SAUT GN. HAPANA. 580 ya 2020 ilifuta shahada walizopewa wahitimu 162 wa Madaktari wa Udaktari wa SFUCHAS kuanzia 2015 -2019,” inasomeka taarifa hiyo.

Source: Daily News
Kutorudisha nakala za masomo......
Naomba mtu anieleweshe hapo kosa lipo wapi? Na ina maana chuo inazo orijino lakini inadai nakala (copy) walizonazo wahitimu zirudishwe.

Je kitaaluma imekaaje hii
 
Yaan nimemaliza 2015 na gamba mmenipa na nimeshapata ajira halafu unadai nirudishe transcript uidhinishe,,, !!!

uchawi ndio huu wa Nchi yenye mbuzi wasio na mwenyewe wanaozunguka jiji la Mwanza na Ilala.. Anyway
Soma charters za vyuo. Degree ni mali ya chuo husika. It can be revoked at anytime in case of justifiable abuse. Tafuta kisa cha waziri mmoja wa Ujerumani aliyevuliwa degree baada ya miaka kumi utaelewa.
 
Chuo kikuu cha St. Augustine kimebatilisha shahada ilizotoa kwa madaktari 162 waliohitimu chuo cha udaktari cha St. Franscis kuanzia mwaka 2015-2019.

St. Augustine imechapisha tangazo kwenye gazeti la Daily news ikitoa notisi kubatilisha shahada za wanafunzi hao 162 ambao inadai wamegoma kurejesha nyaraka ya matokeo(Transcripts) ambazo walipewa bila baraza la senete la chuo kuwa na taarifa na kuziidhinisha.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa seneti ya chuo hicho, balozi Prof Costa Mahalu imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mkutano wa senet ilioketi mwezi wa pili.

===

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kimewafutia shahada Madaktari 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha St Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015-2019.

Notisi kwa Umma iliyochapishwa katika Gazeti la Daily mnamo Jumatatu (27 Machi, 2023), ilisema wahitimu 162 walikataa kimakusudi kurudisha nakala za masomo, 'Transcript' walizopewa bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu licha ya kukumbushwa kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa seneti ya SAUT Balozi Prof. Costa Mahalu inaeleza uamuzi wa kuondoa shahada hiyo umekuja baada ya kikao cha Seneti cha Chuo Kikuu kilichofanyika Februari mwaka huu.

"SAUT kupitia Seneti ya Chuo Kikuu katika Seneti yake ya 54 isiyo ya kawaida, mkutano uliofanyika tarehe 25 Februari 2023 katika chuo kikuu cha SAUT na kwa mujibu wa Kifungu cha 47(1) & (2) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sheria Na. 7 ya 2005 ikisomwa pamoja na Vifungu. 6(3)(ii), 7,8 na Kanuni ya 29 (1) ya Mkataba wa SAUT GN. HAPANA. 580 ya 2020 ilifuta shahada walizopewa wahitimu 162 wa Madaktari wa Udaktari wa SFUCHAS kuanzia 2015 -2019,” inasomeka taarifa hiyo.

Source: Daily News
Kwanini watoe hizo transcript bila ufahamu, vyuo vingine miyeyusho tu
 
Pasipo hiyo seneti kujua kwa sababu hiyo nawaambia chuo wameshakiua tena kimekufa kifo cha mende. Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza akaomba kusoma chuo hicho tena.

Hiyo seneti ipelekwe mahakamani ikahojiwe hata kuhusu afya za watanzania waliotibiwa na watu ambao hawajajidhi vigezo.

Halafu vipi kuhusu hao waliowapa hizo transcript mbona mleta mada hajatujuza au wao hawagusiki?
 
Back
Top Bottom