SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Hizo nakala za masomo hao watahiniwa walipewa vipi bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti, ina maana zilitolewa kinyemela?

Kuna mtu alikula pesa hapo, naamini atakuwa alishapoteza kazi muda mrefu, ila kama yupo ofisini itakuwa ni maajabu..

Na hao watahiniwa ni kama hawaamini walitoka salama, wanaonekana hawajiamini, ndio maana wameingia mitini wasije zirudisha waambiwe walifeli masomo mawili wanatakiwa kuyarudia.
 
Wao ndio wazinguaji kwanini watoe transcript bila ufahamu, hii nchi bado vituko vinaendelea.
 
tukiacha kila mtu afanye anavyofikiria kichwani mwake mambo hayataenda.taratibu ziko wazi fuata kuepuka usumbufu na kama unadhani degree ni kile tu kilichopo kichwani kazi kwako kama utatumia kichwa kuomba kazi.
Mkuu elewa mambo yalivyo, huo Ni uzembe wa kimamlaka hadi kufikia unampa mtu cheti maana yake ushahakiki Mchakato!! Na cheti hakiwezi kutolewa Mara mbili mbili utakuwa uhuni tu..

Transcript nikirudisha then unaweka matokeo mapya umeyatoa wap!! Na Ni miaka 7 Sasa huo ni uhuni tu...
 
Kutorudisha nakala za masomo......
Naomba mtu anieleweshe hapo kosa lipo wapi? Na ina maana chuo inazo orijino lakini inadai nakala (copy) walizonazo wahitimu zirudishwe.

Je kitaaluma imekaaje hii
 
Yaan nimemaliza 2015 na gamba mmenipa na nimeshapata ajira halafu unadai nirudishe transcript uidhinishe,,, !!!

uchawi ndio huu wa Nchi yenye mbuzi wasio na mwenyewe wanaozunguka jiji la Mwanza na Ilala.. Anyway
Soma charters za vyuo. Degree ni mali ya chuo husika. It can be revoked at anytime in case of justifiable abuse. Tafuta kisa cha waziri mmoja wa Ujerumani aliyevuliwa degree baada ya miaka kumi utaelewa.
 
Kwanini watoe hizo transcript bila ufahamu, vyuo vingine miyeyusho tu
 
Pasipo hiyo seneti kujua kwa sababu hiyo nawaambia chuo wameshakiua tena kimekufa kifo cha mende. Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza akaomba kusoma chuo hicho tena.

Hiyo seneti ipelekwe mahakamani ikahojiwe hata kuhusu afya za watanzania waliotibiwa na watu ambao hawajajidhi vigezo.

Halafu vipi kuhusu hao waliowapa hizo transcript mbona mleta mada hajatujuza au wao hawagusiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…