Katika mambo haya yanayotokea sasahivi katika Nchi yetu. Madhira tunayopitia kutekwa, kuteswa, kuuwawa wa raia wezetu kwa sababu wote tunafahamu ni za kisiasa.
Katika ushirika huu wa uhalifu kati ya Serikali, Mahakama na Bunge. Katika sauti hafifu tunazosikia zikitoka kutetea wanyonge na kukemea wababe. Katika yote haya ni nani anafikiri yupo salama? Nauliza swahili hili utalijibu mwenyewe.
Katika tafakuli hii kuna watu wamenikumbusha madhira yaliowahi kutokea katika nchi El Salvador kule katika nchi Latin Amerika miaka ya 70 ilishuhudia mambo kama haya watala wababe, wanatumia majeshi na vikosi vyao vya watu wasiojulikana, kuteka, kuua na kugandamiza na kunyanyasa raia na kupoteza raia.