Sauti ya China yatarajiwa kusikika zaidi kwenye mkutano wa COP30 wa Brazil

Sauti ya China yatarajiwa kusikika zaidi kwenye mkutano wa COP30 wa Brazil

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG111584598627.jpg


Mkutano wa 30 kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP30) unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mjini Belém nchi Brazil, ambao unatajwa kuwa mkutano wa kilele wa kihistoria utakaoweka ajenda kuhusu mabadiliko ya tabia nchi duniani kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, muongo muhimu kabisa wakati dunia inaendelea kuathiriwa kwa viwango tofauti vya matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi.



Kuanzia joto kali lililotokea katika sehemu nyingi za kaskazini mwa dunia katika majira ya joto mwaka huu, mafuriko yaliyosababisha madhara makubwa katika baadhi ya miji, na baridi kali isiyo kawaida katika maeneo ambayo kwa kawaida yanatajwa kuwa ni maeneo yenye joto, yote haya yanatukumbusha kuwa dunia inatakiwa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa mtindo wa matumizi ya nishati duniani uwe na mwelekeo wa kupunguza utoaji wa hewa za ukaa.



China ambayo ni moja wa wachangiaji wakubwa wa utoaji wa hewa ya ukaa duniani, imekuwa inapiga hatua chanya kwenye suala la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na hasa kwenye uzalishaji na matumizi ya nishati safi, na kupata mafanikio mengi. Wakati Marekani ambayo pia ni mchangiaji mkubwa kwenye utoaji wa hewa ya ukaa, kupitia maamuzi ya serikali ya Rais Trump inarudi nyuma na kuunga mkono waziwazi matumizi makubwa ya nishati ya visikuku (fossil fuel), wakati wanasayansi wa mabadiliko ya tabia nchi wamefikia makubaliano ya kauli moja kuwa matumizi ya nishati hiyo, yana mchango mkubwa kwenye kutoa hewa ya ukaa inayosababisha ongezeko la joto duniani.



Jambo la kusikitisha ni kuwa Marekani imefuta ofisi ya Idara ya serikali inayoiwakilisha Marekani katika mazungumzo ya mabadiliko ya tabia nchi, kunakoifanya Marekani isiwepo kwenye mkutano huo wa Brazil. Wataalamu mbalimbali wa maswala ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi, wanaona kuwa kitendo cha Marekani sio cha kiwajibikaji na wanahofia kuwa kutokuwepo kwa Marekani kunaweza kuzikatisha tamaa nchi kuwa na tajiri, ikiwa ni pamoja na zile za Ulaya. Mkurugenzi wa Climate Action Network Europe, Chiara Martinelli, amesema nchi hizo zinaweza kutumia kutokuwepo kwa Marekani kwenye juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kama kibali cha kurudi nyuma kwenye hatua zilizofikiwa, au hata kutoyapa uzito yale yanayoweza kukubaliwa kwenye mkutano wa Brazil.



Mwanasayansi wa hali ya hewa katika Chuo cha Imperial London Bw. Joeri Rogelj, amesema kutokana na mchango unatolewa na China katika juhudi za dunia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na Marekani kujitoa kabisa kwenye mazungumzo hayo kunamaanisha kuwa sauti ya China kwenye mkutano wa COP30 itasikika zaidi, na kwamba China inaweza kutoa mwelekeo wa nini kinatakiwa kufanyika katika kipindi cha miaka kumi ijayo.



China kupitia taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje, imekuwa ikirudia msimamo wake kuhusu suala la mabadiliko ya tabia nchi, kuwa hii ni changamoto inayotukabili binadamu wote, hakuna nchi iliyo salama dhidi ya changamoto zake, na hakuna nchi inayoweza kukwepa changamoto hii, na nchi zote zinatakiwa kuchangia kwa namna moja au nyingine kwenye kukabiliana nayo.



Ni wazi kuwa hatua, msimamo na ahadi zilizotolewa na China kwenye suala la mabadiliko ya tabia nchi duniani zina uhalisia na zimefanya China iwe inaaminika zaidi kwenye suala hilo kuliko Marekani. Lakini ni wazi pia kuwa Marekani imeamua kuhujumu juhudi za dunia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kutokuwepo kwake, iwe ni kwenye mkutano wa COP 30 au kuendelea kuwa nje ya makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kunafanya mafanikio ya juhudi hizo kubwa mbali sana kuliko inavyotarajiwa.
 
Back
Top Bottom