BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
SAUTI YA HAKI YA ASKOFU YAFIKA NJOMBE NA KUKEMEA VITISHO DHIDI YA WAALIMU NCHINI!
Tarehe 8 Oktoba 2020. Nimefika Njombe na kutoa ujumbe wa haki katika Mkutano wa Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Salum Mwalimu.
Pamoja na mambo mengine, nilikemea vitisho dhidi ya Waalimu nchini kote kuhusiana na utashi wao wa kisiasa hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu. Hivi karibuni, imeibuka tabia kwa baadhi ya watendaji wanaosimamia Waalimu kuwatisha Waalimu wanaoonyesha hisia zao za kisiasa kwa vyama vya upinzani.
Tuwaache Waalimu wawe huru kuonyesha hisia zao za kisiasa wawapo nje ya kazi au majukumu yao na tusiwalazimishe kukipenda na kukitumikia chama kimoja tu! Kuwafuatilia Waalimu kwa lengo la kudhibiti utashi wao wa kisiasa wawapo nje ya mazingira ya kazi au majukumu yao sio jambo zuri na ni kufinya haki yao ya kujumuika (freedom of association). Waalimu ni sehemu ya utashi wa kimaadili katika jamii, hivyo wasikubali kujazwa hofu na watendaji wachache wenye maslahi ya kisiasa ambao wanatumikia nafasi za uteuzi.
Kama Askofu nimesikia manung'uniko ya Waalimu walio wengi wanaoishi kwa hofu sehemu nyingi nchini baada ya kutishwa ili wasishabikie vyama vingine, bali washabikie chama kimoja tu! Tunawatahadharisha walio na mamlaka juu ya Waalimu kuacha kuwatisha Waalimu wanaoamua kushabikia vyama tofauti na kile kinachoshabikiwa na watendaji walio na mamlaka juu ya Waalimu hao kwani hakuna chama cho chote cha siasa kilichopewa haki ya kuwamiliki Waalimu! Tuepuke kujenga chuki za kiitikadi kwa Waalimu kwa misingi ya kiitikadi kwa kuwa Waalimu pindi wakifikia kikomo cha uvumilivu hakuna atakayeweza kuwanyamazisha! Tukumbuke kuwa, Mungu alimtumia mwalimu katika kuikomboa nchi hii.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki