Sauti ya umauti masikioni mwangu

Sauti ya umauti masikioni mwangu

Habari ya usiku wana jf!

Leo ninayofuraha kuweka bando kwenye simu yangu baada ya siku nyingi bila kuweka bando!

Kwanini hiyo heading! Ipo hivi, mm kijana wa miaka 28.6, lakini nipo kama mtu mzima wa miaka 40. Sijaoa wala sina mtoto. Maisha nayoyaishi hiki kipindi sidhani kama Mungu ndiye aliyepanga niyaishi. Naishi maisha ya ovyo sanaa. Nimelelewa na mama tu na ndiye aliyenipambania hadi kupata haka kaelimu ka ovyo ambako hakana msaada na mm kabisa.
...
Nimekuona mpumbavu ulivyoanza kumtupia ujinga wako JPM! Kamtafute Yesu akusamehe dhambi zako na utarejeshewa miaka yako yote iliyoliwa na nzige, na madumadu, na tunutu!
 
Habari ya usiku wana jf!

Leo ninayofuraha kuweka bando kwenye simu yangu baada ya siku nyingi bila kuweka bando!

Kwanini hiyo heading! Ipo hivi, mm kijana wa miaka 28.6, lakini nipo kama mtu mzima wa miaka 40. Sijaoa wala sina mtoto. Maisha nayoyaishi hiki kipindi sidhani kama Mungu ndiye aliyepanga niyaishi. Naishi maisha ya ovyo sanaa. Nimelelewa na mama tu na ndiye aliyenipambania hadi kupata haka kaelimu ka ovyo ambako hakana msaada na mm kabisa.

Ipo hivi, mwaka huu tangu uanze sina hamu nao tena maana ulikaribishwa kwa majanga ya kuanza kumwuguza mama yangu. Toka mwezi wa 11 hadi huu mwez wa tatu ndo bi mkubwa amerudishwa nyumbani. Nimempambania ili nisije kubaki na uchungu hapa duniani kama mama angefariki. Ningejiona sina maana kabisa ukizingatia mama aliza vitu vyake vyote ili anisomeshe mm akiamini nikipata ajira nitamtunza. Marehemu hasemwi vibaya ila utawala wa mwamba umeniharibia future yangu kwa 100%.

Tuachane huyo marehemu na utawala wake,. Baada ya mama kulazwa ilibidi nitoe hela yangu yote hadi hela iliyokuwa kwenye biashara nikatoa yote. Haikutosha ikabidi nianze kukopa hela kwa wakopeshaji wa mitaani maana walikuwa wananiamin kuwa nitawalipa maana nilikuwa nafanya biashara na wao wanaona. Nimeingiza deni kubwa sana saiz linasoma milion 6. Mimi sina ata mia mbovu, yan ata cha kuuza. Uwanja nilishauza muda. Sasa jana nimeambiwa na mmoja wa watu niliowakopa akaniambia "nitakudai kwa namna nyingine" hii kauli imenitisha sanaa, niliwaza nitakamatwa na police ila nahisi hapana ni uchawi utatumika na jana usiku nimelala vibaya sijui n wenge sijui ndo simu ya kifo yenyewe hiyo nilipigiwa ndotoni!

Mwisho mm nina amani kuona nimemsaidia bi mkubwa. Lakini pia nina huzuni maana nahisi nakufa muda wowote na nawaza mama atasikiaje habari ya mimi kufa, nawaza mchumba niliyekaa nae miaka mitatu akinisubiri nimuoe atasikiaje habari ya mm kufariki. Kiufupi hicho ndo kinanitisha. Lakini acha iwe hivo tu maana sina uwezo wa kulipa hizo hela mm.

Makala ni ndefu poleni ila nawaomba tuwapende mama zetu, usimtendee baya mama yeyote huendi ndiye mama yangu ambaye nitamwacha pekee yake hapa duniani bila uwepo wangu. Upendo ni amri kuu ya Mungu!
Kama unaona mwamba ndo aliharibu maisha yako, nenda kwa Bi kidawa atakupa hela ya bure!
 
Anza kusali kanisani na hata ukiwa nyumbani omba, Soma biblia, imba nyimbo za tenzi, sio kwa ajili ya kujiandaa kufa Ila ni kwa ajili ya kuisikia sauti ya Mungu akikupa upenyo, epuka kumlaumu Mungu, mshukuru, amini binadamu anapofika mwisho ndipo Mungu anapoanzia.

Single parent kid, you have a lot to fight
 
Ukiwa na changamoto na kuanza kuwaza kufa kwanza unautumia vibaya ubongo wako na nguvu fikiria mnyama ambaye haijui kesho yake lakini anaruka ruka huku na kule kwa furaha wewe sio funza, sio nzi, sio konokono na wala sio chura tatua changamoto yako usiikimbie
Natamani kukabiriana nayo maana wakati nakopa nilijua nitapambana. Ila nimeishiwa pakuanzia sina. Deni la milion 6 riba yake 20% kila mwezi kwahiyo linakimbia spidi isiyo kifani. Sina sehemu ya kuingiza ata 5000. Nitapambanaje na deni linalotaka nilipe 1,000,000 kwa mwez ili libak constantly.
 
muombe aliekukopesha asimamishe riba... mwambie hali yako harisi... mkuu nayahisi maumivu yako... 😭😭😭​
 
anza kwa kufanya kazi za vibarua, kulipwa kwa day.
mpaka hii utasema huiwezi?
Hakuna kaz ya kutumia nguvu nitashindwa labda nguvu zangu ziwe ndogo sawa na ukubwa wa kazi. Shida ni kuwa nitatumia muda gan kulipa deni. Isingekuwa deni mbona easy ningechoma ata mahindi. Mkuu,
 
Back
Top Bottom