SAUTI ya Watanzania na Maandamano ya Bila Kikomo - There is more Than one Way to Skin a Cat....

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Ushauri tu; Gandhi alivaa shuka sio sababu alikuwa hana pesa za Mavazi mengine na ingawa ilimfanya a-connect na masses (kuwa mmoja wao) bali huenda hii ilikuwa ishara ya Mgomo.... (Mgomo dhidi ya Viwanda vya Nguo vya Mkoloni); na impact yake ilikuwa ni kubwa na mpaka leo lile shuka limekuwa kama Identity ya Gandhi

Kuliko kufanya maandamano ambayo watu wataumia na huenda wala kusiwe na positive impact, sababu mtapigwa Propaganda kwamba mnafanya fujo mnaweza kufanya yafuatayo:-
  • Kuonyesha kutoridhika au kufurahishwa na kinachoendelea mnaweza mkasema watu barabarani na katika shughuli zao wavae Tshirt fulani za rangi fulani zenye ujumbe fulani...; na kwa kuhakikisha kwamba huu hauwi mradi wa wachache (printers) mnaweza kuzigawa bure au kila mtu mwenye rangi hizo kuprint zake (screen printing) kama kuna Artwork na kuendelea au hata kujishonea yake....

Binafsi ninavyowajua hawa wadau mtapigwa propaganda na huenda message yenu nzuri ya kugombania mnachogombania ikageuzwa kwamba nyie ni wafanya fujo, au hata kupelekea watu kuumizwa na lawama kuja kwenu na sio kwa aliyeumiza...
 
Nadhani ni haki ya kila Binadamu pia kutoa Ushauri kama ilivyo haki yako wewe Pia kupinga...., Ila ni haki ngapi za Kikatiba zinavunjwa na kupigwa Propaganda na mwisho wa siku kutokuleta Tija iliyokusudiwa ?
Ni sawa,

T shirt za Katiba mpya na Tume huru ziliprintiwa na kuvaliwa,

Njia ya maandamano haikuwahi kufanikiwa, so ni vyema nayo ikafanyika tuone impact.

Kusema watu wataumizwa wakiandamana, Si sawa, ni unafanya ionekane police kuwapiga wananchi wasio na silaha waliobeba mabango kupaza sauti zao kuwa ni halali!
 
Kama tu wamekatazwa na kushindwa kufanya Mikutano mpaka kwenda kufanyia kwenye nyumba zao na uani hayo maandamano yatafanyika sebuleni ?!!!!

Ndio maana nimesema kuna njia nyingi za kufanya mambo unaweza ukazibwa mdomo lakini ukatingisha kichwa na kuonekana kwamba unasema hapana...

Hizo Tshirt walizotengeneza waliziuza au waligawa bure ? Unajua watanzania na pesa zao za mafungu unadhani CCM wangekuwa wanauza Tshirt zao zaidi ya kuzivaa watu nane Tanzania nzima nani angezivaa...

Unaandama, maandamano ya kwanza mtu anavunjwa kiuno (unadhani badala ya watu kuongelea hicho kiuno au nani mwenye makosa tutaongelea tena Bandari)? na baada ya mtu kuvunjwa kiuno unadhani ni wangapi watatokea siku ya pili ya maandamano ?!!! Kumbuka hii ni Tanzania sio Kenya... (Utamaduni wa Maandamano Tanzania Hatuna)....
 
Lets be honesty... maandamano ya kudai nini haswa?
Mchakato wa Bandari / Kusikilizwa...., By the way wanaodai kitu kuna kitu wanakidai according to wao hata kama mimi na wewe tunaona hawapo sawa..., Hence Maandamano ni kufikisha ujumbe (jambo ambalo mimi ninashauri kuna njia nyingi za kufikisha ujumbe huo) Hata kama watu wakiogopa kuvaa tshirt vyenye maneno fulani wanaweza kuvaa rangi fulani ambayo indirectly mtu anaelewa lakini kuna sense of deniability (kwamba sisemi hivyo)
 
Imeshadhihirika kwamba maandamano Tanzania hayawezekani.. Kama tuliibiwa uchaguzi na tukakaa kimya, ina maana hatuwezi andamana kwa chochote.

Hayo mambo ya bandari na mambo mengine yanakuka kwa kuwa na weak democracy ambayo inatokana na uchaguzi.
 
Kama tu wamekatazwa na kushindwa kufanya Mikutano mpaka kwenda kufanyia kwenye nyumba zao na uani hayo maandamano yatafanyika sebuleni ?!!!!

Ndio maana nimesema kuna njia nyingi za kufanya mambo unaweza ukazibwa mdomo lakini ukatingisha kichwa na kuonekana kwamba unasema hapana...

Hizo Tshirt walizotengeneza waliziuza au waligawa bure ? Unajua watanzania na pesa zao za mafungu unadhani CCM wangekuwa wanauza Tshirt zao zaidi ya kuzivaa watu nane Tanzania nzima nani angezivaa...

Unaandama, maandamano ya kwanza mtu anavunjwa kiuno (unadhani badala ya watu kuongelea hicho kiuno au nani mwenye makosa tutaongelea tena Bandari)? na baada ya mtu kuvunjwa kiuno unadhani ni wangapi watatokea siku ya pili ya maandamano ?!!! Kumbuka hii ni Tanzania sio Kenya... (Utamaduni wa Maandamano Tanzania Hatuna)....
Kumbe Maandamano ni utamaduni!!
 
Kumbe Maandamano ni utamaduni!!
Nini ambacho sio utamaduni ? Au maana ya utamaduni ni nini ? The simplest definition ya culture ni (The way we do things around here)
 
mipango hewa mingi mitandaoni,kiukweli kabisa majasiri wa kujitoa sadaka akuna.

shirt zitavaliwa ila zikipigwa mechi mbili za CAF kwa Mkapa na moja Simba na Yanga kwisha habari.
 
Ushauri tu; Gandhi alivaa shuka sio sababu alikuwa hana pesa za Mavazi mengine na ingawa ilimfanya a-connect na masses (kuwa mmoja wao) bali huenda hii ilikuwa ishara ya Mgomo.... (Mgomo dhidi ya Viwanda vya Nguo vya Mkoloni); na impact yake ilikuwa ni kubwa na mpaka leo lile shuka limekuwa kama Identity ya Gandhi

Kuliko kufanya maandamano ambayo watu wataumia na huenda wala kusiwe na positive impact, sababu mtapigwa Propaganda kwamba mnafanya fujo mnaweza kufanya yafuatayo:-
  • Kuonyesha kutoridhika au kufurahishwa na kinachoendelea mnaweza mkasema watu barabarani na katika shughuli zao wavae Tshirt fulani za rangi fulani zenye ujumbe fulani...; na kwa kuhakikisha kwamba huu hauwi mradi wa wachache (printers) mnaweza kuzigawa bure au kila mtu mwenye rangi hizo kuprint zake (screen printing) kama kuna Artwork na kuendelea au hata kujishonea yake....

Binafsi ninavyowajua hawa wadau mtapigwa propaganda na huenda message yenu nzuri ya kugombania mnachogombania ikageuzwa kwamba nyie ni wafanya fujo, au hata kupelekea watu kuumizwa na lawama kuja kwenu na sio kwa aliyeumiza...

Afya ya akili ni pamoja na kuwaza, kupanga na kutenda jambo au mambo yanayo kuathiri au kukuumiza wewe mwenyewe binafsi.

Tatizo hili ni kubwa mno nchini.

Miongoni mwa dalili za mwanzo kabisa za shida ya afya ya akili ni pamoja na kulazimisha kuvunjwa taya, kuteguliwa viuno, kuteguliwa na kuvunjwa miguu na mikono, kung'olewa meno, kipigwa ngeu za machoni, mdomoni na kupoteza muda, kupoteza fahamu, kupoteza maisha yako wewe binafsi huku ukiacha familia yako ikila msoto wa haja.

Sasa,
Kupanga ni kuchagua,
Na akili za kuambiwa changanya na zako...
 
Mwl Nyerere angeogopa kuvunjwa taya, Hadi Leo tungekuwa utumwani.

Usitishe wananchi kuvunja taya wakati gharama za maisha zilivyo juu, petroli juu, kukosa umeme na maji ,dhulma ni zaidi ya kuvunjwa taya.

By the way, polisi haruhusuwi kumpiga yeyote, Bali kumkanata na kumfikishia court.

Wajinga wameisha, hatudanganyiki!!
 
mipango hewa mingi mitandaoni,kiukweli kabisa majasiri wa kujitoa sadaka akuna.

shirt zitavaliwa ila zikipigwa mechi mbili za CAF kwa Mkapa na moja Simba na Yanga kwisha habari.
Kwanini ujitoe Sadaka wakati huenda unaweza kufanikisha kilekile bila kujitoa Sadaka..., Ofcourse kule Syria kwa mtu Kujichoma moto kulianzisha mapinduzi (sio sababu ya mtu kujichoma tu bali watu walikuwa wamechoka)..., French Revolution hali kadhalika (the time was ripe and people were tired)... Sasa kama unaweza ukafikisha ujumbe kwa urahisi huenda impact ikawa kubwa..., leo hii Mbeya kuamka watu wote wamevaa kofia nyeusi au Tshirts Nyeusi (ambazo kila mtu anazo kwake) itaonyesha watu kuuliza nini kinaendelea hata bila kuwaambia....

To win one hundred victories in one hundred battles is not the acme of skill. To subdue the enemy without fighting is the acme of skill. Sun Tzu
 
Mwl Nyerere angeogopa kuvunjwa taya, Hadi Leo tungekuwa utumwani.

Usitishe wananchi kuvunja taya wakati gharama za maisha zilivyo juu, petroli juu, kukosa umeme na maji ,dhulma ni zaidi ya kuvunjwa taya.

By the way, polisi haruhusuwi kumpiga yeyote, Bali kumkanata na kumfikishia court.

Wajinga wameisha, hatudanganyiki!!
nimeshatekeleza wajibu wangu, sidaiwi chochote dhidi ya damu yako na jamaa zako.

kupanga ni kuchagua,

Itoshe kusisitiza tu kwamba nimeshatekeleza wajibu wangu dhidi yako, sidaiwi chochote mbele ya Mungu dhidi yako.
 
Mwl Nyerere na waasisi wote walipewa vipi nchi, kutoka Ukoloni...., Unajua kwanini Bendera yetu haina rangi nyekundu ? By the way Utumwa Struggle hii tukiwapa kina Nyerere tutakuwa tumewakosea kina Mkwawa n.k. kwa kuwapa hii kazi nzuri kina Nyerere.... Na nani amesema watu wasifanye Struggle.., Hata mimi kufanya hiki nachofanya hapa ni Struggle..., Yule mkulima anayeendelea kulima ili wewe ule na kuweza kusema/ kudai unachodai na yeye anapambana (kila mtu kwa wakati wake)
Usitishe wananchi kuvunja taya wakati gharama za maisha zilivyo juu, petroli juu, kukosa umeme na maji ,dhulma ni zaidi ya kuvunjwa taya.
Siwezi kutisha wala sina uwezo wa kutisha wala kupangia mtu yoyote..., nachoweza kusema au kuona ni kwa mtizamo wangu ni vipi kitu kinaweza kuleta impact....
By the way, polisi haruhusuwi kumpiga yeyote, Bali kumkanata na kumfikishia court.

Wajinga wameisha, hatudanganyiki!!
Ni mangapi hayaruhusiwi na yanafanyika ? , Kwa logic hiyo hata Samia alichokifanya kuhusu Bandari haruhusiwi in the first place..., ila ndio hivyo alifanya....
 
nimeshatekeleza wajibu wangu, sidaiwi chochote dhidi ya damu yako na jamaa zako.

kupanga ni kuchagua,

Itoshe kusisitiza tu kwamba nimeshatekeleza wajibu wangu dhidi yako, sidaiwi chochote mbele ya Mungu dhidi yako.
Mjinga wewe,

Hakuna chombo chenye uwezo wa kuua raia ml 60!!

Wauzie wajinga wenzio huo uoga.

Kudai HAKI imeruhusiwa kikatiba, polisi Hana ruhusa kuua raia yeyote.
 
Kwanini ujitoe Sadaka wakati huenda unaweza kufanikisha kilekile bila kujitoa Sadaka..., Ofcourse kule Syria kwa mtu Kujichoma moto kulianzisha mapinduzi (sio sababu ya mtu kujichoma tu bali watu walikuwa wamechoka)..., French Revolution hali kadhalika (the time was ripe and people were tired)... Sasa kama unaweza ukafikisha ujumbe kwa urahisi huenda impact ikawa kubwa..., leo hii Mbeya kuamka watu wote wamevaa kofia nyeusi au Tshirts Nyeusi (ambazo kila mtu anazo kwake) itaonyesha watu kuuliza nini kinaendelea hata bila kuwaambia....

To win one hundred victories in one hundred battles is not the acme of skill. To subdue the enemy without fighting is the acme of skill. Sun Tzu
Hayo mambo ya weupe huko, Africa ni ima uingie uwanjani kiwake au utulie tu.
mambo ya kuvaa nguo za kufikisha ujumbe huku Afric ayafui dafu kwa watawala,kwanza wanaweza kuwatengenezea mvae kwa wingi kukata kiu yenu wao waendelee kutawala.
 
Unaweza kuniambia Tanzania kulishafanyika Maandamano Mangapi na Impact zake ? Ili tujue kama kweli Utamaduni wa Mtanzania ni kuingia Uwanjani ?
 
Back
Top Bottom