SAUTI ya Watanzania na Maandamano ya Bila Kikomo - There is more Than one Way to Skin a Cat....

kwa hali tuliyofikia, kuandamana ni muhimu, maoni ya wananchi hayasikilizwi kabisa. Rejea katiba mpya ya wananchi inavyozungushwa, tume kadhaa zimechagiza mabadiliko ya sheria zetu, nani anafumba macho na kuziba masikio??
Kama hata mikutano yao inapigwa pini kwa technicalities (kumbuka hiki sio Chama cha Siasa) na wanaweza wakatumia loopholes kibao na technicalities kuwakataza..., hivyo basi badala ya kungaganiza kwenye ugumu na ambapo huenda ukafanyiwa faulo za kutosha kwanini usijaribu kujipenyeza pengine na ujumbe ukafika.....; Unaweza ukaandamana jamaa wakaleta mamluki au vijana wengine ili tu kuanzisha fujo na kinuke na wewe ndio ulaumiwe au polisi wapate cha kusema tuliwaambia inteligensia ilisema kuna fujo zitatokea....

Kumbuka...; 'You can't stop the waves, but you can learn to surf.'
 
Yote hayo yapo na yameshafanywa sana na mfumo, haki haiji kilaini hivyo mkuu.
 
Huwa unafurahi sana unaposikia kauli za kujutia baada ya kuvurunda kwa viongozi wetu wakishatoka madarakani eti eeh?
 
Yote hayo yapo na yameshafanywa sana na mfumo, haki haiji kilaini hivyo mkuu.
Kipi hakijafanyika na unataka kipi kifanyike ? Kwa Taarifa yako Mapinduzi / Mabadiliko Makubwa (For better or Worse) yataanzia chini na cha kusikitisha huenda yatakapoanza hayo itakuwa too late na itatuchukua karne kurudi kwenye reli....,

Upuuzi na Ujinga unaofanywa na walamba asali wa sasa..., Kukosekana kwa Fursa, na Umasikini na Matabaka unozaliwa kila leo kwa vijana kuingia kitaa bila ajira zenye ujira hence kutokuwa na cha kupoteza..., Kesho ya Tanzania ikiendelea hivi itakuwa ya kuogopesha na hayo yatatokea sio sababu ya fulani kasema au nani amewaamsha watu bali ni kwamba watu watakuwa cornered na wanaendelea kuwa cornered.

Hence ushauri wangu kwa walamba asali, wajue kula na vipofu ama sivyo janga wanalochuma watakuja kula na ambao hatukushiriki kwenye kupandikiza uozo....
 
Hakuna kisicho na dosari maishani, ukweli ni kwamba wengi wanaouongelea huo mkatana ni wageni kabisa kwenye masuala ya mikataba ya kimataifa, wengi wanasumbuliwa na uelewa mdogo wa kipi kinachotaka kufanyika.

Ni sawa na mtu awe na nyumba anayoishi yeye mwenyewe na pembeni yake anazo nyumba nyingine hivyo anaamua kuzipangisha hizo nyumba ili aweze kuongeza pato lake. Kwenye suala la bandari ni tofauti kidogo, kwamba magati namba tatu mpaka namba saba yanapangishwa kwa DP World na magati namba nane mpaka kumi na moja yanapangishwa kwa mwendeshaji mwingine ambaye tender ya kumpata imeshatangazwa tayari.

Kuna bandari za Bagamoyo na ile ya Tanga na zenyewe zitatafutiwa waendeshaji kwa tender kutangazwa.

Hayo maneno eti DPW kapewa bandari zote na hakuna mwendeshaji mwingine atakayetafutwa kwa maana kwamba ameshamiliki kila kitu ni siasa za kishenzi za baadhi ya mafisadi wenye kunufaika na bandari kwa kutegemea mfumo wa sasa wa uendeshaji. Wanatumia uelewa mdogo wa raia katika kuwadanganya juu ya kusudio la upangishaji unaotaka kufanyika hapo TPA.
 
Print hizo t-shirt wewe,

Wao waandamane maana ni HAKI kikatiba.
Hao watakao andamana ni Wapumbavu kweli, wafanye kazi wazisaidie familia zao, upuuzi wao utaongeza mzigo kwa familia kwa ajili ya mtu mmoja anayetaka kujitengenezea jina!,
-WAKIKAIDI WABONDWE TU.
 
Kama mtu amepanga kufanya maandamo akafanye maandamo yake bila kusumbua wengine...... siwezi kuacha shughuli zangu nipo bize kutimiza target za mtu mwngn
 
Unaandamana kwa maslahi ya mtu anayetafuta umaarufu wake yeye binafsi. Mtagongwa na askari mpoteane muache familia zenu zinataabika bila kujua la kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu alitangulia sasa ni zamu yako wewe kutangulia wala hutishwi wewe tangulia na ss tutakufata
 
Dokta Slaa na Siasa za "Ugagaa na Upwa..." ngoja tuone zitaishia lini.
 
Katiba mpya
Kusimamishwa kwa mkataba mbovu wa DP world
Nakubali ila watanzania ishathibitika ni waoga wa maandamano... ufirauni wa 2020 ndo ilikuwa sababu jaswa ya watu kuandamana ila kama tulipiga kimya sidhani kama tutaweza kuandamana kwa sababu kama hizo nyingine
 
ccm ni wakoloni weusi
 
Mbona watanzania wengi sana hawakubaliani na huo mkataba na walisema kuanzia mara tu mkataba huo ulipotolewa hadharani. Walishasema wazi wazi sababu za kutoukubali huo mkataba, sababu hizi hazina uhusiano wo wote wa kiitikadi za kisiasa, dini wala kabila.

Walioanza kusema ni pamoja na professa mashuhuri wa sheria, Prof. Shivji, Jaji Waryoba, Joseph Butiku na wengine wengi wa aina hiyo. Tundu Lissu alikuja kudandia baadaye huu mjadala na kuufanya wa kisiasa na kuanza kuwaporomoshea matusi viongozi wakuu wa serikali. Yaani Lissu alivuruga kabisa huo mjadala hadi wananchi na serikali ikabidi wajitoe kwenye huo mjadala.
 
Ni haki ya kina Lissu na hata vichaa na malimbukeni na wao kupinga wanachopinga kwa wakati wao bila kubughuzi wala kuingilia haki za wengine (ingawa viongozi wakidhihakiwa wawe na ngozi ngumu sababu wanaowadhihaki wanawalipa na hawakulazimishwa kuchukua hio kazi wanaweza kuacha muda wowote)...

Na mimi kwenye suala la Mkataba tangia mwanzo nipo upande mmoja tu wa Transparency (Total absolute Transparency kwenye Mikataba yote inayohusu mali za UMMA) sababu hata wakisema tunabadilisha tutajua vipi wakiamua kubadilisha tena ?
 
Kwamba Askari ndio wameandama kwa kwenda kuwazuia hence wameandama !!!; Well if that is the Case then well and good....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…