"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....


Swali jepesi kwanini Sauti ya watanzania hawajafanya maandamnano yasiyo na kikomo? Je kikwazo chao ilikuwa cdm?

Kuna mpango wa muda mrefu toka kipindi Cha dhalimu kuanzisha chama cha upinzani ili kifanye upinzani wa kuratibiwa na dola, na chama hicho kichukue nafasi ya cdm. Ndio mnatest mitambo ama? Hao sauti ya watanzania waendelee na mipango yao, sio lazima cdm wajiunge nao, na Wala cdm hawatawazuia kwenye mikakati Yao. Ccm walifanikiwa kuchezea watanzania muda mrefu, ila kwa sasa ni mambo ya wakati ukuta.
 

Tofautisha chawa humo. Wenye akili zao wamo.
 

Mkuu umeandika andiko refu lisilokuwa na mantiki lenye hoja zisizokuwa na mashiko labda kutengeneza mazingira ya mtu kuchoka kulisoma na hivyo kutokujibiwa madai yako yote.

Kwa hakika itabidi kwenda extra time kukujibu hoja kwa hoja.

Zawadini nikushukuru kwa habari za uwepo wa bandiko hili.

Mleta mada tegemea majibu hoja kwa hoja.
 
Ulitaka chama cha siasa kiendeshe programme ya kumsafisga Slaa ?
 
Nipende sasa kuukujibu kifungu uzi wako mrefu kifungu, tena kwa upendo tu ndugu Uzima Tele:


Mkuu aya hii ni mawazo yako binafsi. Kwamba ni kama zile hekaya tulizozizowea za wale nguli wetu kama kina "Deo Kisandu tu."


Aya zote hapa nazo ni mawazo yako mengine tena Yaani another Deo Kisandu style.


Hapa tena ni mawazo yako binafsi tu. Kwamba ni kama nabii Tito akifanya vitu vyake.

Wanatumia agenda zilezile zilizobebwa na CHADEMA yaani Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, mkataba wa bandari kama ndoano tu ya kunasia samaki [CHADEMA] huku wakiuficha unyoka wao...

Hapa umeandika kama Mrema na NCCR ya zama zile. Kwamba kumeibiwa agenda siyo?

Zingatia agenda hizo hazina hati miliki. Hizo ni agenda za wananchi.

Ni jambo la kushangaza mno kujimilikisha agenda kama hizo ndugu Uzima Tele.

CHADEMA waliliona hili. Hawakufanya makosa kuwashitukia. Hongereni CHADEMA, mmejiokoa..

Hapa tena ni mawazo yako. Wengine tunaona vinginevyo ndugu. Kwa vile wewe ni binadamu pia hitimisho lako kama hivi Kwa hakika litawafikirisha wenye akili zao tu, si chawa wa aina yako.


Kwamba Chadema hawajatokea rasmi kukukana hadharani ni jambo jingine la kushangaza mno.

Wewe nyuma ya keyboard na fake ID unaweza je kujinasibu kuwa Chadema kuliko kina Mdude? Kwa lipi hilo ndugu?

Wito kwa kina Mdude na wengine wote: hakuna kutoka Chadema kwa provocations za kijinga kama hIzi.

Kwamba kesi ile ilikuwa ni igizo na ukiwa nyuma ya keyboard siyo?

Hiyo utawaambia chawa wenzio tu ndugu Uzima Tele.


Mawazo yako tena hapa. Kwamba mwingine anaweza kukutuhumu wewe au awaye yote popote kutumiwa na hao jamaa siyo? Halafu nani atakuwa sahihi au nani atakuwa wrong?

Hisia? Kila mtu ana zake na si sahihi kudai zako tu ndiyo sahihi. Kwa kigezo kipi?
Hizi zinaitwa ramli chonganishi.


Mawazo yako tena hapa. Yaweza kuwa wewe na wenzio ndiyo mliotekwa kwa kujua au kutokujua na badala ya kupambana na adui yetu sasa mko busy mnapambana na washirika.

Ukweli mchungu wananchi wanaona. Unadhani ni rahisi kuwauzia propaganda rahisi na kama hIzi?

Msimamo wa CHADEMA uliotolewa na Mwenyekiti wao Mh. Freeman Mbowe ni simple and very clear...

Mbowe si Mungu. Labda kama una maana kuwa ni mheshimiwa Mungu.

Unadhani walikosea waliosema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu?

Kwenye hili wengine tunaona Mwamba ameteleza na hii ni haki yetu kutoa maoni yetu.

Lakini jamaa hawa wanajifanya kutoelewa kabisa. Bila shaka ni wajinga hawa. Haraka haraka wameigeuza vita hii kuwa ya Freeman Mbowe personally. Wanatumia kanuni ya "mpige mchungaji, kondoo watawanyike". Wenye akili wameliona hili na wanawashangaa..

Wapi ulipoona hiyo vita na Mbowe? Tangu lini kukosolewa ikawa ni vita na mtu?

Heshimu mawazo ya watu ndugu Si Kila mtu anaweza kuwa chawa.

"Zidumu fikra za Mwenyekiti ni CCM huko siyo kwenye jamii iliyostaraabika. Tushawishiane kwa hoja."

Hebu take time na sikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kilichowakwaza hawa jamaa hapa👇👇
View attachment 2773537

Agenda za kina Mwabukusi ni agenda za wananchi. Hakutajwa Mbowe wala Chadema kwenye hoja zao.

"Hasira za mkizi hizo kwenye clip hiyo zilikuwa za nini? Tunajenga nyumba moja adui yetu ni mmoja. Wewe huoni bora angekaa kimya tu kama alikuwa kakwazika?"

Hebu mtu makini aniambie, hatuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA mpaka hapo ina shida gani hata hawa watu wakasirike kiasi hiki?

Kulikopo ni kukosolewa. Mbowe anakosolewa tena siyo na kina Mwabukusi bali na watu waliovunjika moyo na msimamo wake kama hivi.

Tofautisha kukosolewa ni kukasirikiwa na hata kuwa ni kutumiwa?


Clip yako ni ya lini ndugu? Kwenye siasa hakuna adui wala marafiki wa kudumu ila agenda.



Agenda aliyonayo Slaa leo ni agenda yetu wananchi. Kulikoni nyie na makasiriko haya?

Kwamba mnamchukia Slaa kama mtu? Chukieni hoja zake au tuonyesheni matatizo kwenye hoja zake.

Hadi hapa siyo siri kina Mwabukusi, Slaa na wenzao wako vizuri.

"Mnyonge mnyongeni .. ndiyo ulio ustaarabu?"


Wamekuwa wazi kuwa zikiisha, 7 Oct watatoa tamko kabla ya maandamano. Kwamba hukusikia hayo ni kwa sababu ya haya makasiriko?


Kwamba hujui walikwenda Mwanza kufanya nini? Wala mafanikio yaliyopatikana huko bayo huyajui? Kama ni kwa vile haikuhusu si waachie wenyewe ndugu?

Kwamba unadhani dunia au wananchi hawaoni? Kwani wewe ni CCm au ni kibaraka au usiyejijua tu?


Mkuu hakuna maswali yoyote Wala analysis yoyote ya maana uliyoweka hapa ndugu. Zaidi ni kuwa unaonyesha wazi kuwa hauwezi kuwa na mchango wowote kwenye ukombozi wa nchi hii.

Kwa hakika Chadema kwamba hawaja ku disown hadharani Hadi sasa kwa bandiko lako hili, litakuwa ni jambo la aibu sana.

"Ama kwa hakika aibu naona miye."


Ndugu kama hoja zao si unachana nao tu ndugu? Kama anqvyosema Mwamba:

"Kwani tatizo liko wapi?"

Ukweli mchungu:

Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono

Habari ndiyo hiyo.

Cc: Zawadini
 
Hiyo mikutano umeshaawahi kusikia mbowe akilalamika kuhusu kupanda kwa mafuta zaidi ya kuimba democrasi ambayo haijawahi kuipractices mahala popote ndani ya chama
 
Huo ushawaishi wa kwa mwanachi utaupateje ikiwa mnakula na wakubwa huko juu halafu mnakuja kutunukishi shombo ili tuonekane tumekula wote
 
Kwenda mahakaman hata wewe unaweza enda kila mtu ana-uhuru wa kwenda ni haki ya kikatiba kwa kila mtanzania sio achievement
Kwenda mahakani sio achievement
Tunasafari ndefu sana kama fikra ndo hizi
Achievement kwa ni ile people's...
 
Machawa ya Mnowe bwana. Kiufupi Mbowe ndo anakwamisha harati za CHADEMA kwa sasa. Lussu us very clear and consistent. Mbowe is outdated for a needed opposition leader hapa. Tunataka mtu radical kuyaondoa maCCM. Lissu is the whole gem.
Mbowe mpaka leo akisimama jukwaani anaongea mambo ya democracy, wakati hot issue iliyopo wakati huo ni bandari ,ni kama swala la bandari hawalipi kipaumbele kabisa tofauti na Lisu
 
Ni akili ya kijinga sana kumuamini Dr Mihogo.

NI WAJINGA TU NDIYO WALIOSAHAU ALICHOTUFANYIA KIPINDI CHA MAGUFULI.
Nyumbu bana .. kwa hiyo kumuamini huyo mjasiriamali ndo unajiona unakili . Kwa nini usijipige kifua usema mimi ni mpumbavu
 

Mkuu tafadhali nataka kuwa na akili kma hizi za kupembua mambo nawezaje maana mimi nilikataa shule 4m2
 
WAFADHILI WA SAUTI YA WATANZANIA WENGI NI CHADEMA DIASPORA.

LENGO LETU NI MOJA TUSICHONGANISHWE NA MASHUSHUSHU WA CCM.

NO HATE NO FEAR
Amna ushushu hapa ,zaidi kuona ukweli kuhusu mbowe wenu ,mjesiriamali wa kisiasa inabidi tuamke
 
Tusipoungana, tusahau kuitoa CCM madarakani,

Watu wanatunza visasi Eti Slaa ni msaliti kana kwamba alikacha kufanya compaign kama Maembe!!

Kukaa Pembeni kumpisha mtu uliyemtuhumu Kwa ufisadi ni UZALENDO Si usaliti.

TEC, Mbarikiwa,Ndugai,Lissu, Dr Slaa, Mwabukusi, Madeleka, Mdude, Dr Nshalla , Bashiru, nk nk ndo wanabeba agenda za wananchi Kwa vitendo.

Wote tuungane nao Kwa vitendo.
 
1. Mimi si mwanachama wa CHADEMA na bila shaka wewe pia. Lakini wote tunahitaji mabadiliko ya kuondoa ukiritimba wa mfumo wa utawala wa CCM uliodumu kwa takribani miaka 60+ sasa.

2. Na wote (bila shaka) tunakubalina na kuamini kuwa CHADEMA ndicho chama cha siasa kilichosimama imara kinachoweza kuongoza wengine kupambania mabadiliko haya ya kimfumo...

3. Ukirejea hoja #2 hapo juu, ndiyo maana Sauti ya Watanzania waliwa - approach CHADEMA na sio CUF au NCCR MAGEUZI au ACT WAZALENDO ama wengine. Kilichokosekana ni mawasiliano na mipango mibovu ya wahusika na kikubwa zaidi kiwango kidogo cha kuaminiana na ndio msingi wa makala yangu hii..

4. Ni kwa msingi huu kuwa, tunajadili yaliyojiri kati ya hawa wanaojiita Sauti ya Watanzania vs CHADEMA. Na katika kujadili huku kila mtu anaweza kuja na mtazamo wake. Wewe umeuona mtazamo wangu kuwa too judgemental. It's ok. Lakini ndiyo mtazamo wangu.

5. Hakuna mtu amesema CHADEMA hawana jambo wanaweza kukubaliana na hawa watu. Yapo na ni karibu yote. Tatizo ni kwa kiwango gani Sauti ya Watanzania wanaweza kuaminiwa na wenzao. Kumbuka yaliyowahi kuwatokea NCCR MAGEUZI mara mbili miaka ya 2000 na juzi kati hapa. Na kumbuka ya CUF ya Maalim Seif Shariff Hamad na ya Prof Lipumba..

6. CHADEMA watakuwa wajinga sana kama hawatatumia historia ya kufa na kudhoofika kwa vyama hivi kama bench mark ya kujifunza na ili wajue namna wanavyoweza kuenenda...

7. CCM is dying lioness. CCM is so desparate. Na CCM si wajinga. Wanaijua nguvu ya CHADEMA. Wanaumiza kichwa kila siku namna ya kukabiliana na CHADEMA hii ili kuvunja nguvu waliyonayo na wao waendelee kuishi kisiasa...!

8. Hatuna shaka na CHADEMA maana ni taasisi rasmi kisheria iko kwenye mapambano ya kisiasa kwa zaidi ya miaka 30 ikikua tukiiona. Hawa Sauti ya Watanzania walioibuka juzi na ghafla tu kujifanya washirikiane na CHADEMA, ni lazima wapite kwenye chekecheo la kipimo cha kuweza kuaminiwa..

Na kumbuka, shetani hamwendei mwanadamu anayetaka amharibu akiwa ktk sura yake ya ushetani. Ili ampate mwanadamu huyu lazima ajigeuze awe kama malaika wa nuru..

Unajuaje kuwa Sauti ya Watanzania si huyu shetani aliyejigeuza kuwa malaika wa nuru? Ni kwa kuwa tu wanazungumza lugha kama yenu?........ Oooh, utaliwa mchana kweupe!!!

Ni hilo tu, hakuna jingine ndugu Kalamu
 

Kulikuwa na uzi huu:

Lissu rudini ubaoni, Majukwaani hakutamng'oa CCM

Katika mapendekezo ilikuwa issue ya habari na propaganda.

Kwamba hadi sasa hawajaukana hadharani uzi huu wa ndugu Uzima Tele, ni jambo la kushangaza sana.

Haya sidhani kuwa ni mawazo ya Chadema bali ya chawa tena wasiojitambua.

Kwa hakika ukombozi si Kwa njia hii Chadema wanaonekana kuchukua.

Bila kutambua kuwa hakuna adui wala rafiki wa kudumu bali agenda, hakuna mafanikio hapo.

Ninakubaliana na list hii:

TEC, Mbarikiwa, Lissu, Dr Slaa, Mwabukusi, Madeleka, Mdude, Dr Nshalla , Mwamakula, nk nk ndo wanabeba agenda za wananchi Kwa vitendo.

Nikurekebishe hapa: Kina Bashiru na Ndugai na wa namma hiyo inabidi wajitokeze wazi wazi huku tujiridhishe zaidi.

Ni kweli kuwa hata wao si haba.
 

Chawa wakikuelewa tuletee mrejesho tunakusubiri. Tuko pale.
 
CDM ndio inasaliti watz ktk HOJA ya Bandari Kwa kuipeleka kwenye mikutano ya hadhara Badala ya kuongoza maandamano yasiyo na kikomo wakiungana na watz, sauti ya watz,Hadi Bandari zetu na maliasili zetu ziheshimiwe na Watawala.

Chadema kutowakana ndugu hawa hadharani haiwasaidii ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…