Ubaguzi ni suala gumu sana, Leo hii nilikuwa na jamaa yangu mmoja tukakutana na rafiki yake, katika kutambulishana na mazungumzo mawili matatu yule rafiki yake akauliza sawali "we kabila gani"? Kwa kawaida huwa sipendi swali la aina hii kwahiyo sikumjibu.
Kwa uzoefu wangu swali la aina hii huambatana na maelezo kama vile; walewaleeee, au wazee wa kujifagilia, au vyovyote vile ambayo kimsingi si sawa.
Huwa najiuliza hivi ni kwanini kuna mtu mweusi ilhali mwingine ni mweupe? Kuna mrefu wakati mwingine ni mfupi? Lakini kuna mwembamba na mnene, kuna tajiri na masikini, kuna mlemavu na aliyekamilika na kadhalika