Sayansi na uchawi !

Sayansi na uchawi !

kumbuka hata kibiblia uchawi unatajwa sana...kuna watu waliitwa 'wakaldayo' kwenye kitabu cha daniel..kuna wachawi wa misri kitabu cha kutoka...kuna wachawi enzi za mitume kitabu cha matendo..n.k


so uchawi upo hata leo ingawa hakuna hofu kwa wale walio ktk kristo Yesu.
 
Kupinga jambo ni rahisi sana maana unaweza hata kupinga jinsia yako mwenyewe,shida inakuja pale ambapo utaambiwa uelezee ni kwa vipi unapinga....

Hebu tueleze ni kwa namna gani hakuna uchawi na una uthibitisho gani hakuna ...!
sasa ushahidi wa kuwa hakuna uchawi niutoe wapi? nenda kwa huyo mtaalamu anifanyie uchawi unaodhani naweza kuja kushuhudia hapa, hakuna uchawi achaneni na hizo fikra,
 
CCM na UKAWA kamwe hawawezi kukubaliana au kutambuana,, ni sawa na uchawi na science
 
sasa ushahidi wa kuwa hakuna uchawi niutoe wapi? nenda kwa huyo mtaalamu anifanyie uchawi unaodhani naweza kuja kushuhudia hapa, hakuna uchawi achaneni na hizo fikra,

Watu kama nyie mara nyingi ndio wanakuwa wachawi wenyewe sasa ile guilt consious in apply hapa, wanakuwa wanahisi watu labda wanawajua kuwa ni wachawi na ile kuondoa hilo basi wanaanza kusema na kutetea kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Chunguzeni sana wale watu wanaodai hakuna uchawi wengi wao ndio wachawi wenyewe.
 
Watu kama nyie mara nyingi ndio wanakuwa wachawi wenyewe sasa ile guilt consious in apply hapa, wanakuwa wanahisi watu labda wanawajua kuwa ni wachawi na ile kuondoa hilo basi wanaanza kusema na kutetea kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Chunguzeni sana wale watu wanaodai hakuna uchawi wengi wao ndio wachawi wenyewe.
sasa wewe unayejua na kufahamu kuwa kuna uchawi ni kwanini na wewe usiwe mchawi kama umeweza kumjua mchawi?
 
unasoma kiswahili,.unatafakari kwakiswahili,.unaelewa kwa kiswahili,.
Unacomment kwa kiingilish,..jamanii
Is there anything wrong with that? Please stop within the sophistry.
 
​this comment section is a singularity of retardation to the main topic concerned..

I know it is hard for you to comprehend the existence of science prior to the revelation of it to mankind. Mathematics, logic and science are branches within philosophy. You cannot build upon anything that has no foundation in reason. The Christian scientists like Francis Bacon who invented Empiricism (the modern scientific method) did so on the basis that God was reliably rational and unchanging, so His order could be discerned by falsification.

There is no dichotomy between science and religion. They are separate areas of investigation. They scientific method is designed to investigate Natural physical phenomena. It is very good at this limited role, but it is limited. Science cannot tell you most truths. Science can prove that glass can cut skin, but science is impotent to prove hitting grandma over the head with a liquor bottle is morally wrong. Science is morally neutral.
 
Mtumishi umenena vyema sana,ni kweli kabisa sayansi ina limitation kwenye kuverify mambo na kama hili tutaluelewa tutaokoa maisha ya wapendwa wengi sana

Huyu jamaa yangu baada ya tukio hili nilimshauri kwamba aachane na waganga kwani kwa kuendelea kuwatumia anakuwa ni mtumwa na watakuwa wanamchezea tu na kimsingi nguvu iliyotumuka kumdhuru mkewe na iliyotumika kumponya ni ile ile hivyo hakuna uponyaji wa maana na anapaswa kumjua Mungu na kuachana na mambo ya waganga lakini alinicheka sana na kuniambia niache utani

Sikua na jinsi ya kumlazimisha lakini nimemuambia kuna siku atakumbuka kwani huko hakuna uponyaji wa kweli na wa maana

Jamaa haelewe na siku hizi waganga hawaishi nyumbani kwake

Nimeamua kumuangalia tu!
Kiongozi, basi wewe endelea kumuombea tu, ipo siku macho yake yatafunguka na kuifahamu kweli na kukumbua maneno yako.

Biblia ipo wazi sana, inasema kuwa: Shetani hawezi kumpinga Shetani, meaning, huwezi toa pepo chafu kwa kutumia Waganga. Kinacho tokea hapo ni kuongezewa Majini kila siku. At the end of time, they will kill him. Very sad. But, hey, with prayers, all things are possible. Keep on praying for him.
 
sasa ushahidi wa kuwa hakuna uchawi niutoe wapi? nenda kwa huyo mtaalamu anifanyie uchawi unaodhani naweza kuja kushuhudia hapa, hakuna uchawi achaneni na hizo fikra,

Very funny, you want Eiyer to give you proof of your belief? That is your naive error not his. Most of the thinking world knows better.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,kwanza neno mtaalam lilianzia kwa baba yake na jamaa yangu na sio mimi

Inawezekana alipewa masharti maana kuna wakati alikuwa anapewa maagizo yeye peke yake

Kwani illusion maana yake nini?
Mkuu Illusion ni mazingaombwe au mauzauza, kuna jamaa huwa namwangalia anaitwa magician, sasa huwa ana break secret code lakini ni za hatari, The magician secret has finally revealed... Sasa yale ndio mazingaombwe sio uchawi...

nimesikia Tangazo hapa nilipo wanapita wanatangaza nikaone Waganga wanavyofanya, jinsi ya kupiga ramli, hirizi inavyopumua yenyewe elimu inatolewa bure... ngojea niahirishe safari yangu nikaone kwanza...
 
can you describe the evidence of absence?

Then provide an example of a valid refutation? You can't. Your logic IS flawed. Deeply and critically flawed. That's why reasonable people expect evidence. Unreasonable people expect proof. You expect physical evidence of a non-physical being or things? That's like expecting to find water with your metal detector.

Your denial is empty. You can refute nothing. Why does something exist rather than nothing?
 

Then provide an example of a valid refutation? You can't. Your logic IS flawed. Deeply and critically flawed.

That's why reasonable people expect evidence. Unreasonable people expect proof. You expect physical evidence of a non-physical being or things? That's like expecting to find water with your metal detector.

Your denial is empty. You can refute nothing. Why does something exist rather than nothing?
nimesema hakuna uchawi, wewe unataka nitoe ushahidi wa kisichokuwepo, who is imbecile between me and you?
 
nimesema hakuna uchawi, wewe unataka nitoe ushahidi wa kisichokuwepo, who is imbecile between me and you?

You got spanked by the evidence. You can't engage them either, much less refute them. You are just as frustrated and silly as Dirk. Your assumption that only Empirical science is evidence is silly and FALSE. That is your naive error not mine. Most of the thinking world knows better.

NOTE:
Dismissals are not refutations. You lack any refutation. You lack any evidence or arguments to justify your blind oafish non theist faith.
 
nimesema hakuna uchawi, wewe unataka nitoe ushahidi wa kisichokuwepo, who is imbecile between me and you?

hulazimishwi kuamini uchawi kama unataka kushuhudia uchawi jitahidi utauona huwezi kushinda ndani kwako ukaona uchawi

HUTAKI UNAACHA
 
hulazimishwi kuamini uchawi kama unataka kushuhudia uchawi jitahidi utauona huwezi kushinda ndani kwako ukaona uchawi

HUTAKI UNAACHA

Kumbe mpaka nitoke nje ndo ntauona?
 
Kuna mambo yanatokea huku duniani na pia tunaambiwa kuna watu wanafanya utafiti kuhusu mambo mbali mbali, najiuliza hivi kuna maeneo maalum tu ya kufanyia utafiti au ni kila eneo?

Nauliza swali hilo kwa sababu kuna mambo ambayo yanatokea huku mtaani ambayo yanatia mashaka kabisa kuwa hiki kinachosemwa kukihusi kipo kwa uwazi mkubwa sana

Tumekuwa tukielezwa kuwa sayansi imeshindwa kabisa kuthibitisha uwepo wa uchawi na kwa sababu hiyo basi uchawi umebakia kuwa ni hadithi tena za nchi masikini kama zetu na zaidi sana ni story za kufikirika!

Natilia mashaka kuwa inawezekana hawa wanasayansi wanajua kabisa uwepo wa hii kitu na wanakana kuthibitisha kwa sababu tu unawafaidisha kwa namna moja au nyingine au sayansi ni dhaifu sana kiasi kwamba inashindwa kutoa majibu ya mambo kadhaa yanayotokea kwa uwazi mkubwa

Pia sitaki kuwa mpuuzi wa kudhani kuwa uchawi upo huku Afrika tu na haupo Ulaya kwani pote wanaoishi ni binadamu na kama kuna jambo moja mahali fulani uwezekano wa jambo lile lile kuwepo mahali pengine ni mkubwa kuliko zaidi.

Hebu soma hiki kisa hapa chini halafu uamue mwenyewe

**********************************************

Nilifahamiana na kijana huyu ambae kazi yake ni dereva taxi miaka mitano iliyopita wakati alipokuwa anafanya biashara ya mazao mkoani Shinyanga, aliondoka huko na kuhamia Mwanza kabla ya mimi kuhamia huku, mwaka jana alikuja na kuniambia kuwa baba yake amemtafutia mchumba huko kwao Bariadi na alitaka kwenda kuoa, nilimtakia kila la kheri na aliondoka na jamaa zake wanne kwenda huko kwa ajili ya kuoa...


Harusi ilifanyika vyema na baada ya wiki mbili kijana alikuja na mkewe akiongozana na baba yake pamoja na zawadi kadhaa ambazo alipewa huko harusini, walifika na walikwenda kwenye nyumba ambayo ilikuwa imeandaliwa na kaka yake huyu jamaa yangu kuwa ndio watafikia hapo, kijana alifika na maisha ya ndoa yalianza rasmi..

Baada ya mwezi mmoja baada ya harusi kufungwa mkewe na jamaa yangu alianza kujisikia vibaya, alipelekwa hospitali na kupatiwa vipimo lakini haikuonekana kama alikuwa na maradhi yoyote yale na alirudi nyumbani na kupewa dawa za kupunguza maumivu tu, mkewe aliendelea na hali hiyo kwa muda wa mwezi mmoja na ulipofika mwezi wa 11 mwaka jana hali ilibadilika na kuwa nzuri kiasi...

Jamaa yangu alipata dili la kuwapeleka jamaa fulani huko Kahama kwa gari yake na aliondoka kwa ahadi kuwa atarudi kesho yake, aliondoka na baada ya masaa kadhaa alitujulisha kuwa amefika salama na akasema ataanza safari kesho yake asubuhi ili awahi kurudi kwa kuwa mkewe hakuwa na hali nzuri...


Ilipofika usiku nilipigiwa simu kuwa mke wa jamaa yangu hali yake sio nzuri, niliondoka na kwenda nyumbani kwa jamaa yangu na kumkuta shemeji yangu haongei na alikuwa ametoa macho tu, tulimkimbiza hospital ya mkoa na alipokelewa na alifanyiwa vipimo lakini hakuonekana kama ana tatizo lolote, lakini kila muda unavyokwenda alionekana hali yake inazidi kuwa mbaya, tuliamua kumpeleka Bugando hospital kwa uchunguzi zaidi lakini matokeo yalikuwa yale yale...

Tuliamua kumjulisha baba yake na jamaa yangu nae alikuja pale hospital na kujaribu kutafakari cha kufanya, baba yake na jamaa yangu aliamua kutokumuambia jamaa yangu hali ya mkewe kwa sababu angeweza kuchanganyikiwa na kuamua kuanza safari usiku huo huo kitu ambacho hakikuwa salama kwake, daktari alimuita baba wa jamaa yangu na kumwambia kuwa anapaswa awaze kama mtu mzima kuhusu mgonjwa maana hali haikuwa njema...

Baba yake na jamaa yangu alimuelewa daktari na aliomba alale pale na kupatiwa huduma ya kwanza ili ajaribu kufikiri cha kufanya, shemeji yangu alipatiwa huduma pale japokuwa ilikuwa ni huduma ya kubahatisha tu kwa sababu vipimo vyote havikuonesha kuwa alikuwa anaugua nini, tulimuacha pale hospital na mama yake jamaa yangu na baadae baba yake na jamaa yangu ilibidi ampe taarifa jamaa yangu kuhusu hali ya mkewe, jamaa yangu aliahidi kuondoka alfajiri sana kuwahi ili wajue cha kufanya..


Tulilala na asubuhi na mapema nilifika pale hospital na tulikuwa tunamsubiri jamaa yangu afike ili tujaribu kufikiri cha kufanya, jamaa yangu alifika kwenye saa nne hivi asubuhi na baba yake na jamaa yangu alituambia tuongozane nae na alituambia kuwa hapa hakuna namna nyingine tofauti na kwenda kwa "wataalam", jamaa yangu hakugoma na tuliingia kwenye gari na safari ilianza, nilikuwa kimya tu huku nikiona matokeo ya hili jambo..

Tulifika kwa mtaalam baada ya nusu saa na tulikaribishwa ndani moja kwa moja maana ilionekana kuwa huyu mtaalam alikuwa na taarifa ya ujio wetu, tuliingia na tulikalishwa kwenye viti na mtaalam aliambiwa tatizo la shemeji yangu ambae wakati huo bado alikuwa Bugando, mtaalam alisikiliza na baadae alianza kuchanganya madawa yake pale na baada kama ya dakika tatu hivi alituambia kuwa tusiogope maana "watu" wake wanakuja, nilijisemea kimoyo moyo kuwa ngoja leo nione, aliposema hivyo tulisikia kishindo mule ndani na tukasikia sauti ambayo hatukuona ilipokuwa inatokea na ilikuwa ni ya lugha ambayo sikuielewa na iliongea kwa muda kama wa dakika nne hivi kisha kukawa kimya...


Mtaalam alileta kioo cha kujiangalia na baadae alikimwagia dawa fulani hivi na ghafla kikabadilika na kuwa TV na tulianza kushangaa sana tulipoona harusi yote ilivyofanyika kule kijijini na kila kitu kilichofuatia na tuliona mengi lakini machache ni kwamba nyama ambayo walikula kule harusini haikuwa nyama ya ng'ombe kama wao walivyodhania bali walikula nyama ya tumbili ambao tuliona walivyoandaliwa hadi kupelekwa kwenye harusi na wale ng'ombe waliochinjwa nyama yao ilichukuliwa na wale watu waliochinja wale tumbili...

Baada ya harusi walikaa kikao na kuamua wamuue yule dada ambae ni mke wa jamaa yangu kisa eti amepata mchumba kabla ya dada zake wanne na kiongozi wa kikao kile alikuwa ni mama mkubwa wa mke wa jamaa yangu, baadae tuliona vile jamaa yangu alivyoondoka hadi alipofika na kwenda kwenye nyumba aliyofikia, tuliona mengi sana ila kwa uchache ni hayo, baada ya kuona hayo mtaalam alituambia kuwa mke wa jamaa yangu alilishwa mawe ambayo yanamkaba bila kupata hewa vyema lakini pia alilishwa mjusi [wale mijusi ambao wanakaa sana kwenye majengo mabovu wanakuwa na rangi mbili, pink na rangi ya udongo]...


Nilimuona jamaa yangu akistuka sana na mtaalam alituambia kuwa hata sasa tukirudi hospital tutamkuta viganja vya mikono vya mke wa jamaa yangu vimeanza kubadilika na kufanana ngozi ya mijusi wale, nilihisi kijasho kikinitoka na nilisema ngoja nikifika Bugando nitaangalia mikono ya shemeji yangu, baadae mtaalamu alituambia kuwa mke wa jamaa yangu angeendelea na hali hiyo na baada ya wiki mbili angefariki...


Mtaalam alisema kuwa atakwenda na sisi mchana huo na tutakwenda kumtoa hospital na kwenda nae nyumbani kumtibu, baada ya maelezo hayo tuliondoka pale na mtaalam na vifaa vyake na baada ya nusu saa tulikuwa tumefika hospital, tulifanya taratibu zote na tuliondoka na mgonjwa, nilimtazama viganja vyake na kweli niliona vimebadilika kama mtaalam alivyosema, tulifika nyumbani kwa jamaa yangu baada ya dakika ishirini na kazi ilianza...

Mke wa jamaa yangu alinyweshwa maji fulani na alitapika mawe mawili na baadae alitapika mjusi ambae mtaalam alitueleza kabla na cha ajabu mjusi yule alikuwa hai, nilishangaa sana kwa kweli, na baada ya kutapika hayo nilimuona akianza kuhema kawaida tofauti na mwanzo na aliomba maji ya kunywa kitu ambacho hakikutokea mwanzo kabisa, mtaalam aliagiza apewe maji na alipewa na baada ya kunywa alinyanyuka na kukaa kitako pale kitandani, mimi nilikuwa natafakari sana haya mambo huku nikijisemea kuwa huku duniani kuna mambo....

Alipewa dawa nyingine akanywa kisha aliambiwa alale na aamke baada ya saa moja, alifanya hivyo na alipoamka aliomba kwenda kujisaidia haja kubwa na alikwenda na aliporudi alisema kuwa amejisaidia haja kubwa nyeusi kama mkaa na aliogopa sana, kumbuka mtu huyu asubuhi tu alikuwa haongei na wala alikuwa haonekani kama hata anahema na alikuwa ametoa macho tu lakini ghafla baada ya masaa mawili mtu amechangamka utadhani labda alikuwa anaumwa kichwa tu..

Mtaalam alisema vitu alivyojisaidia ni madawa ambayo aliyanywa kwenye maji kule kijijini, baada ya hayo alipewa dawa ya kutumia kwa wiki moja na aliambiwa kuwa atakuwa salama,nilikaa pale hadi jioni na niliaga na kuondoka huku nikistaajabu na kushangaa sana yote yale...

Niliendelea kwenda kumjulia hali shemeji yangu na alipona kabisa na sasa anaendelea na maisha yake na sijui walichofanya kuhusu wale waliowafanyia yote hayo na sikuuliza kabisa..

**************************************************************************************

Sasa hilo ni tukio moja tu, yapo mengi sana na yanastaajabisha na kuonesha kwamba kuna nguvu hii ambayo inadaiwa kuwepo nguvu ambayo ni hasi na inaitwa uchawi, sasa hawa wanasayansi hawayajui haya au wanajidai tu hakuna huku wakijua kabisa upo?

Huo utafiti wao unahusu maeneo gani kama wanasema haya ni hadithi tu? Hivi tukio kama hilo ni hadithi kweli?

Sidhani, hapa naona hii sayansi na wanasayansi wanajua kabisa kuna huu uchawi ila wanaamua tu kukanusha kwa faida yao au hii sayansi ni dhaifu kwa kiasi kikubwa sana maana imeshindwa kutoa majibu kwa mambo yaliyo wazi kama haya.

Wewe unaonaje haya?

Je una uzoefu wowote ambao unaweza kushea nasi hapa?

Kama unao hebu tueleze ili tufikie mahali tukubali mambo mengine hata kama hii sayansi yao inakana au wanajidai kukana.

Hatuwezi kukana mambo yaliyo wazi kama haya!
[/SIZE][/QUOTE]
 
Back
Top Bottom