Kwanza kabisa Qur'aan tu yenyewe ni muujiza,kama utaamua kuisoma na kutafakari.
Lakini Qur'aan si kitabu cha Sayansi bali ni muongozo kwa watu na kwa wale wamchao Allah aliye juu.
Makosa mengi wanayo yafanya watu wengi wanao jivika vazi la utetezi wa Uislamu ni kupotosha maana za aya na kulazimisha zifate Sayansi wakati hili si sahihi, Qur'aan ndiyo kweli yenyewe na Sayansi inatakiwa kuifata Qur'aan.
Sayansi ni nadharia zilizojengeka katika majaribio, na hakuna Facts katika Sayansi zaidi ya ubahatishaji.
Sayansi inakumbwa na tatizo kubwa sana la kufikia hitimisho juu ya jambo fulani, ma hili tatizo litawakumna mpaka wanakufa hii ni kulingana na misingi yake. Kwahiyo kulazimisha aya ziendane na sayansi ni kuikosea adabu Qur'aan.