Hili lina ukweli asilimia zote.. Nimeendesha Bus flani ni scania 114, hp380 nilikuwa nainuka kitonga na 70kph kama hakuna vicheche mbele! Na mtoa mada kadanganya kuwa kisa speed ya zhongtong ni 140 basi mwendo ni mkubwa kuliko scania yenye 120kph. Aangalie ukiwa na gari ndogo unatembea 160kph lakini itakuja bus scania yenye 120kph inakukata kama umesimama... Nadhani ameangalia tu maandishi kwenye darshbod ila hajawahi kuzijaribu apate uhakika wa anachoandika.. Kingine kasema golden deer zinasumbua sana scania, amesahau kwasasa gari zote zinatembea mwendo sawa ila ushapu wako kwenye vituo au kuweza kulipia tochi za kwenye 50kph zitakufanya njia nzima utembee 84kph wakati mwenzio akifika kwenye 50kph anapunguza, unategemea watafika sambamba?? Saizi kuwahi zaidi ya mwenzio ni ujanja wako tu njiani sio uwezo wa gari. Labda kupanda milima tu ndo scania itawahi zaidi kumaliza