Scholarship za China: Majina yamechakachuliwa

Scholarship za China: Majina yamechakachuliwa

Lambardi

Platinum Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
18,813
Reaction score
21,830
Wana JF naomba msaada wenu mwenye kujua utaratibu wa kupata scholarship za china kupitia wizara ya elimu.

Maana nimepata official email toka China kuwa nimepata nijiandae kwa safari document zitakuja soon; Nimeenda wizarani wanasema jina langu halikurudi.

Nashangaa niko njia panda naomba msaada!
 
Wanataka kukuchakachua hao ebu waforwadie email uliyopata kutoka china,kama wakikataa itisha press conference uwaumbue hao mabazazi washenzi sana hao mie mwenyewe walinichakachua scholarship za china wakamchukua mtu ana div 2 ya 10. Khaaaa wakati mie nina one ya 3 na kulikua hakuna mtihani wanaangalia max tu!
 
Hiyo mbona kawaida sana. Ilibidi utumike kupitia vyeti vyako na kuandika concept note ili nafasi ipatikane.
 
pole sana ndugu yangu...mie walitaka kunifanyia umafia nikawazidi akili kwani nilikua na jamaa alikua huko akanifowardia list nzima tuliochaguliwa, niliprocess visa na kupata e tikect masaa 5 kabla ya ndege kuondoka. Hata wachina wameshtukia kuwa watz wanachakachua majina.
 
kujuana,ubinafsi na rushwa kunasababisha vijana wakose haki zao ambazo walistahili nakusihi endelea kufuatilia ndugu!
 
Mh! China? simu feki, redio feki,TV Feki, magari feki, mataili feki, piki piki feki, vipi kuhusu elimu nayo si f...i? kama wamekuchakachua achana nao apply nchi nyingine wanaotoa elimu bora.
 
China wanatoa elimu feki kwani miongoni mwa madr pale Moi waliofanya operation kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa walisoma China na baada ya kutimuliwa hapo Moi wapo huku mawilayani na kwenyewe ni bure kabisa achana na China kama unataka elimu bora na sio bora elimu.
 
wana jf naomba msaada wenu mwenye kujua utaratibu wa kupata scholarship za china kupitia wizara ya elimu:
Maana nimepata official email toka china kuwa nimepata nijiandae kwa safari document zitakuja soon:nimeenda wizarani wanasema jina langu halikurudi:nashangaa niko njia panda naomba msaada:

samahani mkuu! Ww uliomba lini?
 
Wewe check sirname za watakaofanikiwa kupata ndo utajua kama walichakachua ama hawatachakachua, majina yetu ya akina Kapufi, Mwanakatwe, Saanane, Nkalandu hutayakuta utakuta yale mengine ya akina ---- malizia mi sitaki kwenda Mabwepande kutoa series nyingine na magazeti mengine yafungiwe
 
Mh! China? simu feki, redio feki,TV Feki, magari feki, mataili feki, piki piki feki, vipi kuhusu elimu nayo si f...i? kama wamekuchakachua achana nao apply nchi nyingine wanaotoa elimu bora.


Ukiendelea na kukurupuka bila ya kutafakari, utakosa mengi yenye tija kwako. Soma thread tena.
 
Wasiliana na hao waliokutumia email haraka iwezekanavyo, wakupatie documents zote e.g. admission, scholarship grant letter, then nenda ubalozi wa China nchini uka-state kesi yako (naungana na anayesema ueleze vyote ikiwemo harufu ya kuchakachuliwa-liwalo na liwe)...wakati huo huo huko ubalozi ikiwezekana uanze process za kupata study permit...ukizubaa ndo hivyo atapewa mtu mwingine!Nchi ishauzwa, ukizubaa ndio wanapewa nafasi yako watu wengine, watoto wa kina fulani, na wakienda huko wengi wao wanaboronga tu!
 
Mimi mwenyewe ilinitokea mwaka jana hawa akina mama kibaya hawa jamani cjui kwa nini wanafanya hivi?
Lakini saa hizi nimeghairi sitaki tena kuusikia ujinga wa gov scholarship ni bora nigoogle tu.
 
Asante sana kwa ushauri inatia hasira sana jamani;ngoja nijaribu kufuatilia kuanzia chuoni na ubalozini nione inakatisha tamaa ndugu zanguni!
 
pigana mjomba,magamba ndo stahili zao hzo kubebana hata kama ni vilaza,fuata ushauri wa wachangiaji,utafanikiwa,uzuri wake wenyewe china wanakutambua,sasa kuna nn hapo
 
Back
Top Bottom