Science ina support uwepo wa Mungu

Ni mtizamo wako.
Sio mtizamo wangu ndio uhalisia ulivyo.

Huyo Mungu mnayedai yupo hamuwezi na mmeshindwa kumthibitisha uwepo wake.

Mmebaki kufosi tu kwamba yupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe ajiongelee, ajitetee na ajidhihirishe mwenyewe, yeye kama yeye, kama ana huo uwezo.

Mnacho hangaika kumtetea na kumuongelea huyo Mungu ni nini?

Kwani yeye hawezi kujidhihirisha mwenyewe?

Huyo Mungu kama yupo, Atoke huko alipo, ajiongelee mwenyewe kama ana huo uwezo.
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na creator, Hata creator wa kila kitu lazima awe na creator wake mwingine.
Nashukuru hapa umeanza kunielewa sasa ...!!
Katika hivyo vyanzo vingi visivyokua na ukomo, Chanzo cha mwisho kikaamua kujiongeza kika create universe, Kikaunda ulimwengu na sisi...

Narudia tena, Logically hakuna anayejua Mwanzo...

Sasa haijalishi vimepita vyanzo vingapi visivyokuwa na mwisho Ila kwakua tu Chanzo cha mwisho kwenye mtiririko kiliamua kujiongeza kika create universe na kutuumba Sisi, kina haki miliki zote kuitwa Muumba...


NB: Maswali yako najibu - yangu hujibu, ni wakati sasa wewe kunijibu na sio kunirundikia maswali ...!!


Kama ulimwengu hauna chanzo, Ulimwengu huu tunaouona umetoka wapi?
 
Nashukuru hapa umeanza kunielewa sasa ...!!

Katika hivyo vyanzo vingi visivyokua na ukomo, Chanzo cha mwisho kikaamua kujiongeza kika create universe, Kikaunda ulimwengu na sisi...
Ukishasema visivyokuwa na "ukomo" Huwezi kuwa na mwisho.

Tayari hakuna mwisho hapo, Maana hakuna ukomo.

Ukomo= Pasipo kukoma
(Yani hakuna mwisho)
Narudia tena, Logically hakuna anayejua Mwanzo...
Kama hakuna anayejua mwanzo, Uliwezaje kujua yupo muumba?
Sasa haijalishi vimepita vyanzo vingapi visivyokuwa na mwisho Ila kwakua tu Chanzo cha mwisho kwenye mtiririko kiliamua kujiongeza kika create universe na kutuumba Sisi, kina haki miliki zote kuitwa Muumba...
Unathibitishaje kuna chanzo cha mwisho?

Kwanza Ulijuaje kipo na unathibitishaje kipo?

Kama hicho chanzo cha mwisho, kilitoka kwenye chanzo kingine, Basi hicho chanzo cha mwisho sio chanzo cha kila kitu, Maana na chenyewe kina chanzo chake kingine. Kilichokuwa na vitu vyake.

Hivyo chanzo cha mwisho, Hakiwezi kuwa chanzo cha kila kitu, Maana na chenyewe kilitoka kwenye chanzo kingine chenye vitu.
NB: Maswali yako najibu yangu hujibu, ni wakati sasa wewe kunijibu na sio kunirundikia maswali ...!!


Kama ulimwengu hauna chanzo, Ulimwengu huu tunaouona umetoka wapi?
Kama kitu hakina chanzo, Huwezi tena kutaka kiwe kimetoka sehemu fulani.

Ukianza kutaka kiwe kimetoka sehemu fulani, Hata hiyo sehemu fulani lazima iwe imetokea sehemu nyingine fulani.

Ulimwengu tunao uona, Haujatokea mahali popote pale( Hauna chanzo)

Ulimwengu ulikuwepo ndio maana tumeukuta upo na utaendelea kuwepo.

Ulimwengu usingekuwepo, Hata sisi tusingeweza kuwepo.

Mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote ule wa jinsi gani ulimwengu ulifanyika, Zilizopo ni nadharia za kidini na kisayansi tu ambazo hazijitoshelezi na hazina uthibitisho wa uhakika.
 
Tumeukuta tukiwa tumetokea wapi?
Binadamu tunazaliwa kwenye ulimwengu ambao tayari upo. Lakini hatujui ulimwengu ulikuwepo vipi, Au ulifanyika vipi.

Na kama hatujui, Huwezi kuhitimisha moja kwa moja kwamba kuna creator wa ulimwengu.

Maana tunazaliwa kwenye ulimwengu ambao tayari upo, ila hatujui kwamba uliumbwa, Au ulikuwepo tu.

Kwa hivyo huwezi kuhitimisha moja kwa moja kwamba, Ulimwengu uliumbwa na creator.

Maana bado huna uthibitisho huo, inawezekana vilevile ulimwengu haujaumbwa na creator, ulikuwepo tu wenyewe.
 
Binadamu tunazaliwa kwenye ulimwengu ambao tayari upo. Lakini hatujui ulimwengu ulikuwepo vipi, Au ulifanyika vipi.
Unajua vipi kwamba ulimwengu ndiyo umemzaa binadamu ikiwa hujui chochote kuhusu ulimwengu?

Unaamini vipi kwamba binadamu amezaliwa kwenye ulimwengu ambao tayari ulikuwepo, Je kama binadamu ndiye alianza?

Kwanini kuna ulimwengu?
 
Mimi nimeuliza swali ila ulichofanya ni kuja kujichekesha, pia umeongeza msamiati mwingine. Haya unijibu Sasa, Mungu ni nini au ni nani? Na shetani ni nini/nani pia??
 
Listen human, Mungu yupo ! Wacha kuzunguka zunguka
 
Mimi nimeuliza swali ila ulichofanya ni kuja kujichekesha, pia umeongeza msamiati mwingine. Haya unijibu Sasa, Mungu ni nini au ni nani? Na shetani ni nini/nani pia??
Sijichekeshi. Hata hivyo utakua mtu wa wa ajabu kufikiri kua hakuna Mungu!!

Maana hata hio sayansi ulio soma, haikupi uhakika wa dai lako, kwamba dunia imetokea kwa ajari.

Hivyo basi wewe kama ni binadamu wa kawaida utakubaliana na mimi, kwamba si kweli katika hilo

Imagine mtu ametokana na nyani!! Kama sayansi inavyo dai. Sasa hawa nyani waliopo toka wewe umezaliwa hawatamani kuwa watu?

Sikuhukumu kwanamna ya mtazamo wako. Ila nina wasiwasi na ubinadamu wako yawezekana wewe si binadamu wa kawaida, ila unaishi miongoni mwetu kwa sura yetu ila wewe si mwenzetu
 
Kwahiyo hapa Mungu unamfananisha na Atom kweli? 😀
Umesoma hadi kitabu gani kwenye maandiko na je huku kwenye sayansi umesoma hadi la ngapi. Si kwa ubaya lakini
 
Ndio ndio maana haya mambo mnayojifunza humo makanisani na misikitini yakaitwa ni ya kiimani , shida inakuja pale mnapotaka kulazimisha kwamba ndio ukweli mwenyewe 🤔
Huwa hatuuliziulizi kuhusu Imani maana Imani ni kuamini tu swala lilivyo. Shida huja tukianza kulinganisha ya darasani na kwenye nyumba za ibada halafu tukaishia kusema atom ni sawa na Mungu. Labda mtu atengeneze hoja ambayo itatupitisha kwa upana wake tukaelewa haya mambo
 
Listen human, Mungu yupo ! Wacha kuzunguka zunguka
Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe yupo, Kama ana huo uwezo.

Huyo Mungu kama yupo, Anacho jifichia huko alipo ni nini?

Au huyo Mungu wenu amekuwa mwali?

Unahangaika sana kumwelezea na kumuongelea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe, yeye kama yeye. Kwamba yupo.

Huyo Mungu wenu ni mchovu na mdhaifu sana, kiasi kwamba hawezi hata kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.
 
Ndio maana watu waliotengeneza dhana hiyo ya imani waliweka na vitisho kwa sababu walijuq ipo siku watu watahoji kwa kasi mno🤔
 
Bro umeandika meengi na umejibu ambayo sijakuuliza, sayansi ipi imesema mtu katoka Kwa nyani!? Hata ivo hakuna mahali nmesema habari za sayansi.
Nmekuuliza Mungu ni nini/nani, shetani ni nini/nani!? Hujajibu hili swali mkuu. Na pia unasema mi sio binadam wa kawaida okay ni binadamu wa namna gani basi? Hujajibu swali ila unanishambulia muuliza swali....au huna majibu, sema!!!
 
mtoto kua atheist. nadhani unalazimisha kutetea, ulichoaminishwa na nadharia yako ya atheism ilorasmishwa na yule mhuni wa kifaransa, bila yule jamaa sidhani kama tungedebate hapa.

hatuamini uwepo wa mungu ajili ya kuaminishwa na wazazi bt tunaamini ajili ya deities experience.

Kuamini ktk deities kumeanza karne nyingi ktk jamii tofauti tofauti duniani kabla ya dini na jamii za watu kuchangamana, je ushawahi jiuliza aliezipelekea idea ya kuamini deities jamii zisofahamiana ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…