Nashukuru hapa umeanza kunielewa sasa ...!!
Katika hivyo vyanzo vingi visivyokua na ukomo, Chanzo cha mwisho kikaamua kujiongeza kika create universe, Kikaunda ulimwengu na sisi...
Ukishasema visivyokuwa na "ukomo" Huwezi kuwa na mwisho.
Tayari hakuna mwisho hapo, Maana hakuna ukomo.
Ukomo= Pasipo kukoma
(Yani hakuna mwisho)
Narudia tena, Logically hakuna anayejua Mwanzo...
Kama hakuna anayejua mwanzo, Uliwezaje kujua yupo muumba?
Sasa haijalishi vimepita vyanzo vingapi visivyokuwa na mwisho Ila kwakua tu Chanzo cha mwisho kwenye mtiririko kiliamua kujiongeza kika create universe na kutuumba Sisi, kina haki miliki zote kuitwa Muumba...
Unathibitishaje kuna chanzo cha mwisho?
Kwanza Ulijuaje kipo na unathibitishaje kipo?
Kama hicho chanzo cha mwisho, kilitoka kwenye chanzo kingine, Basi hicho chanzo cha mwisho sio chanzo cha kila kitu, Maana na chenyewe kina chanzo chake kingine. Kilichokuwa na vitu vyake.
Hivyo chanzo cha mwisho, Hakiwezi kuwa chanzo cha kila kitu, Maana na chenyewe kilitoka kwenye chanzo kingine chenye vitu.
NB: Maswali yako najibu yangu hujibu, ni wakati sasa wewe kunijibu na sio kunirundikia maswali ...!!
Kama ulimwengu hauna chanzo, Ulimwengu huu tunaouona umetoka wapi?
Kama kitu hakina chanzo, Huwezi tena kutaka kiwe kimetoka sehemu fulani.
Ukianza kutaka kiwe kimetoka sehemu fulani, Hata hiyo sehemu fulani lazima iwe imetokea sehemu nyingine fulani.
Ulimwengu tunao uona, Haujatokea mahali popote pale( Hauna chanzo)
Ulimwengu ulikuwepo ndio maana tumeukuta upo na utaendelea kuwepo.
Ulimwengu usingekuwepo, Hata sisi tusingeweza kuwepo.
Mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote ule wa jinsi gani ulimwengu ulifanyika, Zilizopo ni nadharia za kidini na kisayansi tu ambazo hazijitoshelezi na hazina uthibitisho wa uhakika.