Ninyi " Waamini Mungu" ndio hamnaga hoja. Na wala hamuwezagi kujenga hoja zaidi ya kuanza kutushambulia Atheists.
Nakuuliza hivi na ujenge hoja sio kuleta hadithi zako uchwara za kwenye Quran zisizo na uthibitisho wowote ule.
Moja, Huyo Mungu kabla ya kuumba kitu chochote kile, Alikuwa wapi?
Mbili, Huko alikokuwa, kulitoka wapi na kuliumbwa na nani?
Eleza na thibitisha. Usianze hadithi za kwenye Quran mara oh! kilipanda kikashuka.
Mimi siandiki tu kwamba ili nijifurahishe, nyinyi nawajua ni dhaifu sana kwa hoja kushinda nyumba ya bui bui.
Twende kazi ila usikimbie mjadala na ukiulizwa maswali jibu, tuone nani anayeshambuliwa na nani muongo.
Tuanzia katika uongo wako juu ya Qur'an. Unajua Qur'an walau hata kuisoma au inafanana vipi ? Kingine naomba uthibitishe ya kuwa Qur'an ni Hadithi na kwanini unaandika uongo juu ya Qur'an. Hili ni swali la msingi kwanza ili kujua ufahamu wako na uwezo wako wa kujenga hoja. Sababu kuandika uongo juu ya jambo usilo lijua ni upunguani wa akili.
Mola wetu hakuwahi kutokuwepo, yeye yupo.
Jibu la swali lako hili hapa :
It was narrated that Abu Razeen said: O Messenger of Allah, where was our Lord before He created His creation? He said: “Nothing existed but Him, with nothing beneath Him and nothing above Him. Then He created His Throne above the water.”
Narrated by at-Tirmidhi (3109), Ibn Maajah (182) and Ahmad (15755).
Swali la pili la uongo na halina maana, sababu halina uhalisia. Huu utoto ndio huwa hatuutaki mnaandika andika tu vitu pasi na kujua mnachokojadili ni kipi. Mfano ukikaa ukatumia akili na kufikiria. Swali lako linaishia wapi. Yaani ukomo wake ni upi ?
Kingine nataka uniambie uthibitisho kwako wewe ni upi na una sifa gani ? Ili tupime unachokiandika ni sahihi au la.
Kingine nataka uje ututhibitishie ya kuwa Qur'an au Hadithi ni uongo na haufai kuwa uthibitisho.
Usikimbie hoja Wala maswali.