Nilianza kusikia kuhusu HAARP tangu nasoma shule na niliifuatilia sana kwasababu lilikuwa linafurahisha. Katika usomaji wangu wa historia nilichojifunza ni kutokubaliana na kila taarifa kwa haraka, lakini pia kutokuipuuzia. Kutokufahamu kitu wewe hakuondoi ukweli wala uhalisia wa uwepo wa hicho kitu, nadhani hapa wanadamu wengi ndiyo tunakwama. Tuhuma za HAARP, CERN na DARPA naziangalia kwa jicho la umakini, lakini siwezi kuzipuuza hata kidogo.
Dunia imekuwa na vipindi tofauti, na kuna baadhi ya mambo ya kale mpaka leo hii wanadamu na akili yao wameshindwa kabisa kuyaelezea vizuri. Mambo yaliyofanywa na binadamu miaka zaidi ya 4000 iliyopita. Mfano, mapiramidi ya Misri mpaka leo hii yameacha kitendawili kikubwa kwa wanadamu hata wale ambao wamesoma kuliko sisi. Wengine wanasema ni makaburi ya mafarao, lakini siku za karibuni imekuja nadharia nyingine inasema mapiramidi ni vinu vya nishati (Power-Plants) na wanatoa ushahidi kabisa.
Inasemekana, Waparthi/Waajemi (Parthians) walikuwa na teknolojia ya kukamata radi (Lightining-Trap) kwenye chupa maalumu miaka mingi iliyopita. Hili lilionekana ni ulaghai na ngano za kusadikika, lakini miaka ya hivi karibuni wanasayansi wameweza kutengeneza radi ndogo kwenye chupa. Hivyo ile nadharia kwamba radi inaweza kukamatwa inaonekana ina ukweli kidogo. Japo bado tunahitaji ushahidi mkubwa.
Eneo la dunia la Mesapotamia ya kale kule Iraq wanahistoria na wanasayansi walichimba chini na kukuta eneo hili limejaa (Carbon Isotopes) ambayo ilikutwa hata kwenye mafuvu ya watu. Hili lilionesha kwamba lile eneo liliwahi shambuliwa na mionzi. Wakachimba zaidi na kutambua kwamba kitu chenye mlipuko kama ule wa nishati ya atomic kiliwahi kulipuliwa pale miaka 5000 iliyopita. Sasa sisi tumeanza kujifunza kuhusu nishati ya atomiki na kutengeneza makombora mnamo karne ya 20. Wanahistoria wanatuambia kwamba sisi siyo wa kwanza kufanya hivyo. Hili linafikirisha.
Kuna jamii za kiafrika kama The Dogon Tribe kule Mali, wamekutwa wanamiliki ramani ya anga la nje (Outer Space) ambapo kuna sayari nyingi ambazo haziko hata kwenye mfumo wetu wa jua na wanasayansi hawasadiki kama zitakuwepo. Miaka zaidi ya 2000 iliyopita watu wa Afrika walikuwa na ramani ya sayari zote zinazolizunguka jua (Solar System). Walifahamuje hayo yote bila kuwa na teknolojia ya kisasa ??? Binafsi hata mimi sina majibu. Mwaka 1970 wanasayansi wa NASA kwa mara ya kwanza wanaifahamu sayari ya SIRIUS X, waliiona kwenye michoro ya Dogons wa Mali, lakini wakapinga.
Miaka michache baadaye wakaigundua ile sayari na kutambua kwamba michoro ya Dogon ilisema ukweli kuliko Hadubini zao kubwa (Giant Telescopes). Wameifahamu SIRIUS X, lakini sayari nyingine kwenye mchoro bado hawajaziona. Ukimwambia mtu mwenye akili ya kawaida, haya mambo hawezi kukubaliana nayo, lakini ni ukweli ambao upo na hata wanasayansi wameshindwa kuuelezea.
Namalizia hoja yangu na NIKOLAI TESLA, ambaye ni uthibitisho tosha kwamba INTELLIGENCE IS ALL ABOUT IMAGINATION AND NOT KNOWLEDGE. Kuna mambo aliyafanya huyu bwana mpaka leo hii wanasayansi wanafikiria tu kuyafanya, huku wajinga na wapumbavu wengine tulioenda shule na kupata shahada zetu za sayansi na tafiti tukidhani kwamba ni mambo yasiyowezekana. Tesla aliifahamu IONOSPHERE na nguvu ya mapinduzi ambayo ingeletwa kwa mwanadamu. Akaenda mbali kabisa na kutengeneza gari ambayo betri yake inajichaji yenyewe. Akapeleka pendekezo kwa mabeberu ya Marekani kwamba wafanye hivyo lakini akapigwa chini. Akili ya TESLA ilikuwa iko miaka 3000 mbele.
NB 1: Mwaka 1907, Balozi wa Uingereza nchin Ujerumani, EYRE CROWE, aliandaa muhtasari wake wa kijasusi (THE CROWE MEMORANDUM) kwa serikali ya Uingereza kwamba Ujerumani ananunua chuma kingi mno na anatanua jeshi lake la maji. Wengi walipuuza kwasababu hawakuziona hizo meli zikiwa sehemu yoyote ile na bahati mbaya sana mwenye teknolojia kubwa ya majini (Maritime Technology) na meli za kisasa alikuwa ni Muingereza. Kumbe Ujerumani alikuwa hatengenezi meli zinazoelea majini, yeye amekuja na kitu kipya kabisa, NYAMBIZI (Submarine/U-Boats), silaha ambazo hakuna nchi iliyowahi kufikiria kuzitumia jeshini kwa kiwango kile cha Ujerumani.
Vita ya dunia ilipoanza, ndipo Uingereza walitia akili kwamba kumbe kupigana kutokea chini ya maji inawezekana. Hivyo binafsi siwezi kupuuza chochote kwasababu tu akili yangu inaniambia hakiwezekani au sijawahi kukiona.
NB 2: VITA VYA UKRAINE, ndiyo mara ya mwisho kabisa mataifa makubwa yatatumia teknolojia na mbinu za kivita kutokea karne ya 20. Katika lugha ya kiingereza, nasema hivi: It's the last time major powers will ever use means and methods of warfare from the 20th Century. Mapokeo ya kijeshi (Military Doctrines) ya karne ya 20, yaliangalia vita katika maeneo matatu makubwa ya, VITA VYA ANGA, VITA VYA ARDHINI na VITA VYA MAJINI.
Leo hii kuna mapokeo mapya kabisa kwenye sayansi ya jeshi kwasababu dunia imebadilika mno na uwanja wa vita hauko tu kwenye anga, ardhi na maji. Mambo kama mtandao (Cyber-Space), Anga la nje (Outer-Space), Baiolojia (Biology and Organic Fields), Uchumi (Economy), Taarifa (Information) na Mazingira (Geography, Nature and Environment) n.k yamegeuka kuwa uwanja wa vita na silaha hatari mno zimetengeneza na mataifa makubwa ili kupambana. Sisi bado hatujaziona hizi zilaha kwasababu bado tunaangalia mambo ya karne ya 20.
Changamoto kubwa kiusalama kwa dunia ya leo hii ni hizi hapa:
-Cyber-Warfare,
-Weaponisation of Nano-Technology,
-Artificial Intelligence & Autonomous Weapons,
-Weaponisation of Genetic Engineering,
-Electronic Warfare,
-Weaponisation of Outerspace.
- Energy Weapons
Mataifa makubwa yametumia silaha na mbinu mpya (New Means and Methods of Warfare) tajwa hapo juu kwa kiwango kidogo sana, na imeonekana zina hatari kubwa mno kuliko matumizi ya vifaru nyambizi na ndege. Urusi, Marekani na Isreali wametumia kwenye vita zao Artificial Intelligence, Cyber-Warfare, Electronic Warfare na Space-Warfare katika kiwango kidogo tu (SUPPORT OPERATIONS) ila madhara yake yamekuwa ni makubwa mno. Siku wakiamua kutoa kila kitu nje itakuwa ni hatari mno.
Ikitokea vita kubwa baina ya mataifa kama Uchina na Marekani, silaha kama Abram Tanks hazitatumika katika kiwango kikubwa kwasababu zimepitwa na wakati (They are Obsolete) na kijeshi kwenye dunia hii ya leo ambayo karibia kila mtu anamiliki satelaiti na rada za kisasa, vifaru na mizinga havina maana kabisa (They are visible, and make a Military Commander lack the Element of Surprise)....
Amin, Amin nawaambia silaha ambazo Marekani, Uchina na Urusi wanazo leo hii ni zile za kufikirika kwenye filamu kama Star-Wars, Star-Treck, X-Men na Universal Soldier. Siku wanapambana basi wanadamu wengi mno watapoteza maisha katika kiwango kisicho cha kawaida......