Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Scopolamine ni dawa inayotumika hospital kwenye ishu za upasuaji nk. Lakini hii dawa ikifanyiwa kalabo hutengeneza kitu kibaya kabisa
Ninini hicho?
Ni burundanga kwa jina la kihalifu.... Huu hutumika kuondoa utashi wa mtu hasa kwenye kufikiri na kuchukua maamuzi sahihi. Humfanya mtu atekeleze bila kikwazo kila anachoambiwa
Miaka ya nyuma tulikuwa tunashuhudia matukio mengi ya wizi wa hiari.. Yani mwenye mali kutoa mwenyewe bila kulazimishwa japo si kwa utashi wala ridhaa yake
Wezi hutumia kukupulizia usoni ama kupeana mikono. Huwa wanakuwa wawili ama zaidi. Anayekusemesha ni mwingine na anayekupulizia ni mwingine kabisa, akijifanya mpita njia na kujikwaa karibu yako huku akihakikisha mkono wake umepita karibu na uso wako ama kama mmepeana mikono anahakikisha mkono wako unafika usoni mwako.
Sometimes hutumia mbinu ya kutaka kukutoa kitu usoni. Pumzi moja yenye sumu ya Burundanga hukupumbaza na kulemaza hisia za utashi wako kwa muda. Kinachofuatia unakijua?
Kama una fedha utakabidhi zote kama una ATM card utaenda kutoa fedha na kukabidhi. Kama una gari bila kujitambua unakabidhi funguo na wakati mwingine unapewa na mkataba usaini kama umeuza gari na umelipwa cash
Kama ni samani za nyumbani utawaongoza wezi na fuso na wapakiaji. Majirani wakikuuliza unasema unahama. Kama una chochote cha thamani unaweza kukabidhi kwa hiari kabisa
Muda wa kumbukumbu kukurudia hutegemeana na kiwango cha dawasumu uliyopuliziwa. Zamani watu walikuwa hawajui na kudanganywa kuwa ni uchawi ndio unatumika. Lakini huu si uchawi wala ushirikina bali ni kama dawa ya usingizi ama kaputi.
Wauza madawa ya kulevya hutumia sana hii dawasumu kupata habari za wapinzani wao kutoka kwa mateka waliowakamata. CIA waliitumia wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Na vitengo vingi vya kijasusi yakiwemo magenge ya kihalifu huitumia sana kufanikisha mambo yao.
Cha kushangaza ni mmea wenye kutumika kama malighafi ya kutengeneza hii dawa. Wengi tunaufahamu hasa wale tunaoishi sehemu za baridi.
Wito wangu kwako:
Epuka kupeana mkono na mtu usiyemfahamu barabarani
Epuka kusimama na kuongea na mtu usiyemjua kwenye msongamano wa watu
Makinika na yeyote anayetaka kujifanya msamaria wa kukutoa kitu usoni... Haraka mkamate mkono wake na kuurudisha usoni kwake
Haya mambo huenda na kujirudia kila wakati.. MAKINIKA!