chalii wa ara
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 1,063
- 931
Tatizo Polisi wakiwa wanafanya uchunguzi mnaanza kuwaingilia na kuwakejeli, mfano Tukio la lissu, watu wanaropoka tu na kuipa Serikali wakati mgumu kufanya kazi, hata hao wahalifu wakitangazwa bado mtakuja mtasema Polisi ni Waongo wametunga stori we huoni hiyo ni kasoro Kubwa sana mlionayo?? Nikueleze tu hakuna kitu kibaya Kama kuingiza siasa kwenye jambo lolote lile ndo maana hata jeshini hawaruhusiwi kua mwanachama Wa Chama chochote kile..
Sasahv tunataka chama kimoja basi, tuone watauanaje maana hivi vyama vyama vya visiasa viko Ki maslah hata hayo mauaji yanaweza kua yanaratibiwa na viongozi Wa vyama vya Upinzani ili Ku gain popularity..
Mkuu mbona una hoja dhaifu sana !!
Ulishawah kuskia kuna raia hata mmoja ameenda central au oysterbey kuomba jalada la uchunguzi wa case flani ?? Kama ipo prove me wrong here
Ama una maanisha kuwaingilia kwa namna gani ? Infact police wana namna yao ya ky collect data na kuzifanyia kazi
Naunga mkono hoja kwamba ni vibaya kuliingiza jeshi na siasa na ndyo maana huko hamna wanasiasa
Lakini kubali ukutae jeshi letu linatumika kisiasa
Kwa kumalizia hi tanzania siyo ya mtu fulani ama kikundi cha watu flani flani , hii ni nchi ya watanzania wote
Wa kizazi cha leo na cha kesho kutwa huna uwezo wa kusema tunataka chama kimoja bila kuhusisha maamuzi ya watanzania wote , kupingana kwa hoja isiwe uadui wapendwa.