haitawezekana SLAA atakuwa wapili
source
Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
P.MZIRAY 50,675 J.KIKWETE 2469507 W.SLAA 736366 I.LIPUMBA 308597 H.RUNGWE 10120 M.MUHANYWA 6994 F.DOVUTWA 4321 KURA ZILIZOHARIBIKA 74,138
Jamani, tuwe makini sana. Siyo suala la SLAA kuwa wa pili au wa tatu. Kama kura zikihesabiwa kihalali bila wizi, kuna uwezekano mkubwa kuwa SLAA atakuwa wa
kwanza na hivyo kuwa Rais wa Tanzania. Hapa CCM wanacheza na mind games. They are manipulating the results makusudi kuwakatisha tamaa wafuasi wa CHADEMA kuhusu SLAA kuwa Rais ili juhudi zao wazihamishie kuhakikisha SLAA anakuwa mshindi wa pili badala ya wa tatu wakati SLAA anaweza kushinda kuwa Rais. Narudia tena, matokeo yaliyotoka so far hayafiki hata kura milioni 1.5 na ni ya mikoa ambayo CCM na CUF ina nguvu. Zingatia kuwa watu waliojiandikisha kura ni 19.6 milioni. Turnout ilikuwa ndogo na huenda ikawa 50%, hivyo kura halali ni kama milioni 10. Mikoa ambayo SLAA kafanya vizuri sana na ina kura kama milioni 8 zilizobaki wamezuia matokeo na watayatoa very late haraka haraka ili huenda kesho usiku wamtangaze Kikwete Rais na ijumaa aapishwe fasta.
Nadhani hii strategy yao ya kutengeneza
illusion kuwa Kikwete anashinda kwa kishindo kwa kutoa matokeo ya mikoa ambayo CCM iko strong imekuwa very effective. Watu wengi sasa mitaani na hata huku JF hawazungumzii tena ushindi wa SLAA na ukombozi wa Tanzania. Wanazungumzia 2015 na kujadili zaidi ushindi wa wabunge wa CHADEMA. Naambiwa hata baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA wenyewe wameshakata tamaa.
We must not forget the bigger picture! Bado SLAA ana nafasi nzuri sana ya kwenda Ikulu iwapo kura kwenye mikoa mikubwa iliyobaki zitahesabiwa bila wizi. Tulinde kura za Urais kama tulivyolinda kura za wabunge wetu. Tushinikize matokeo ya kura za Rais kwenye mikoa iliyobaki ambayo SLAA amezoa kura nyingi yatolewe mapema na bila kuibwa kama tulivyofanya kwenye ubunge kwa mafanikio makubwa.
Timu kabambe ya wabunge teule wa CHADEMA isaidie pia kutoa shinikizo hili.
Tusikubali kuchezewa akili na kudanganyika na kukata tamaa kuwa Urais ni mpaka 2015. Huu unaweza kuwa mwaka ambao SLAA atashinda Urais tukiwa makini.
By the way, wanaosema CHADEMA iende mahakamani wakumbuke kuwa katiba mbovu iliyopo inasema kuwa NEC inapo tangaza matokeo ya Urais hayawezi kupingwa mahakamani au popote na ni final hata kama kuna ushahidi wa wazi wa rushwa, wizi wa kura au fraud yoyote. Matokeo yanayoweza kupingwa mahakamani ni ya Ubunge na udiwani tu.
Hapa suluhisho tu ni PEOPLE'S POWER!