Secretarybird, nimefanya utafiti, nimegundua Dunia inajizungusha kwenye muhimili wake

Wakuu, baada ya ubishi mkubwa kuhusu suala la Dunia kujizungusha kwenye muhimili wake kutawala humu JF na kote vijiweni secretarybird, niliamua kufanya utafiti, ili kuwaleteeni majibu sahihi juu ya sintofahamu hii, ili sote humu na vijiweni tuongee lugha Moja juu ya iwapo Dunia inajizungusha kwenye muhimili wake au la.

Utafiti nilioufanya haukuhitaji hata Senti Moja bali ni akili tu ndiyo iliyotumika. Ona hapa 👇 nilichokifanya.

Ilipofika saa moja jioni, niliketi chini ya mti huku nafuturu. Nikaona nyota inayon'gaa kuliko nyota zingine upande wa magharibi, nilipoichunguza kwa makini nikaona kama ile nyota inazidi kusogea chini. Nilitulia pale pale na kukokaa macho kuifuatilia ile nyota kwa umakini mkubwa huku nikihesabu dakika ambazo ile nyota ilitumia hadi ikazama katika ncha ya Dunia. Ile nyota ilitumia dakika 15 pekee.

Siku ya pili niliporudi nyumbani kutoka kazini, nikakaa tene chini ya ule mti sehemu (point) ileile niliyokaa wakati nachunguza nyota huku nikisubiri jua nalo lifike pale nilikotaka. Jua ulipofika kwenye ili point ambako nyota ilikuwepo ile siku ya kwanza nikaanza kuhesba dakika ambazo jua lingetumia hadi kutua katika ncha ya Dunia. Zikapatikana dakika 15 🔥. Nilianza kushangilia huku nikajipiga kifua kuashiria kuwa Mimi ni mwamba......mke na watoto wangu wakanishangaa hata wakasema, "baba amewehuka", ila Mimi sikujali.

Nikajiuliza swali lifuatayo na kujipatia jibu mwenyewe maana 'katika somo la jiografia Mimi si haba'.

Swali, je, kati ya jua na nyota zingine (maana jua nalo ni nyota) kipi Kiko juu (mbali) kuliko kingine. Jibu, 'NYOTA'.

Swali hili ☝️ na jibu lake lilifanya niwe na uhakika kuwa kweli Dunia inajizungusha kwenye muhimili wake na kufanya tupate usiku na mchana, kwani Dunia isingekuwa inajizungusha kwenye muhimili wake Nyota, ambayo iko mbali ingetumia muda mrefu kuzama kuliko jua ambalo liko karibu. Kwa hiyo kutenda Cha jua na Dunia kuonekana kuwa na Kasi sawa kwa monekano wa kawaida (japo kuwa havizunguki) kinadhihirisha kuwa Dunia ndiyo inayojizungusha.

Ebahna akili ni nywele.

Mwisho kabisa, nawakaribisha wataalamua wa haya mambo waje wagongelee msumari hiki nilichokieleza.

DR Mambo Jambo,
Kiranga,
Yoda,
Xi Jinping,
adriz,
Mbaga Jr,
Dr am 4 real PhD,
MENEMENE TEKERI NA PERESI na wengine wengi.
Kwa hiyo kwa kum tag adriz unamchokoza mudiboy..kwani mud kasema jua ndiyo uzunguka na kuzama kwenye tope 😁 ..kweli jini jibril lilikuwa halijui saysnsi na Allah wake .
 
Sijasoma uzi wako hata kidogo maana naheshimu mchango wako mkubwa kwa baadhi ya vumbuzi za kidunia ulizowahi kuleta humu jukwaani.

Ila kwa hili daah
 
Zote zinaonekana kusogea kwa kasi sawa kwa sababu ya mzunguko wa Dunia

Ndiyo maana muda wa kuzama unaweza kufanana

Ulichokiona ni matokeo ya mzunguko wa Dunia, si umbali wa vitu angani
Ndicho nilichomaanisha kwenye uandishi wangu mkuu. Na ndicho lengo la utafiti wangu.
 
Kwa hiyo kwa kum tag adriz unamchokoza mudiboy..kwani mud kasema jua ndiyo uzunguka na kuzama kwenye tope 😁 ..kweli jini jibril lilikuwa halijui saysnsi na Allah wake .
😂😂, adriz, njoo uone Maelezo ya jamaa yako. Angalia hapa ☝️.
 
Sijasoma uzi wako hata kidogo maana naheshimu mchango wako mkubwa kwa baadhi ya vumbuzi za kidunia ulizowahi kuleta humu jukwaani.

Ila kwa hili daah
Mkuu tufichiane tu madhaifu, maana sote hatujakamilika.
 
Japo hujanitaja kwenye list ya wataalamu wako ila nataka nikuulize, kama dunia inazunguka na ni duara mbona hatujikuti tumeinama au
 
Back
Top Bottom