Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Huo anaouita ushindi wa 99.9% kwenye uchunguzi wa serikali za mitaa 2019,ni ushindi wa namna gani,CCM ilishindana na nani?,kwa kuwa na wewe ni idiot hulitafakari hilo unashabikia tu kama punguani,ona ulivyokariri kwamba thread ikichangiwa na watu wachache inakuwa imeandikwa pumba,huwezi tafakari kwamba watu hawachangii kwenye thread fulani kutokana na kutokuwa interested na thread hiyo na si kwamba ni pumba na thread inaweza ikawa pumba na ikachangiwa na watu kwa wingi mfano ile thread ya kupeana likes ni pumba lakini angalia ilivyosheheni wachangiaji
 
Wamarekani ni mabeberu namba moja duniani. Kuna watu hawaelewi ubeberu ni nini. Ubeberu ni mfumo wa kibepari uliyokomaa ndani ya nchi hadi unatafuta maeneo ya kuwekeza nje ya nchi. Katika mbinu za kuwekeza nchi za nje wanakua na mbinu mbalimbali. Ndio utawaona kwenye sura kama wahisani wakopeshaji na sura kama ile waliyoonyesha acacia ndio kawaida yao. Mumesikia jinsi trump alivyokashifu afrika na viongozi wake na pia waziri mkuu wa istael alikwisha toaga lugha kama hizo kuidharau afrika na viongozi wake na kututukana waafrika.
Sasa jiulize anapotokea kiongozi kama magufuli kupambana na rushwa na udhaifu kama alivyodai trump na rafiki yake netanhyahu kwa nini wanahamaki na kuanza kuiundia njama na hila mbaya tanzania?
Watanzania lazima tutambue hakuna njia rahisi kupata maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Lazima tushikamane katika umoja mtakatifu ili tusonge mbele. Upinzani nchini kwetu uwe na lengo moja kwa ajili ya maendeleo wala wasijiuze kwa mabeberu. Isijalishe nani anaongaza la maana kama tuko kwenye njia sahihi.
 
We ulishapigana vita? Au ulikuwepo mwanza wakati wa vita vya kagera? Mig 21 tu ikipita chini unaweza kuzimia. Vita isikie kwa mwenzako. Tatizo ushabiki
 
Ukweli wa nini kilichokua kinaendelea Kibiti hakuna anaefahamu.
Mfano mzuri mzee alieniuzia shamba maeneo hayo kijiji flani mzee alichukuliwa alfajir na wajeda tangu 2015 ila hadi leo hii haijulikani walimpeleka wapi maana si gerezani wala mahabusu hakuna taarifa za mzee, vijana wake walifutilia sana mpaka wakaamua kuacha tu.
 
Kila kitu kina kiasi. Hata mmarekani sio kila kitu wanachotaka wanapata.
Yes, hatuwezi kupigana vita na marekani. Ila kuna mambo ni kuamua tu sisi kama sisi tutafika.
Mmarekani hajawahi kupenda mtu mwingine zaidi ya yeye mwenyewe.
Ulizeni NATO wana hali gani baada ya Trump. Tusikate tamaa. Tusonge mbele. Tukiona siku mmarekani anatupigia ngoma na vigelegele lazima tujue tutakuwa tumeharibu.
Beautiful things in life are earned...and not given for free
 
Ulivyo mjinga unamtolea mfano gadaf wakat hata wazungu wenyewe wanasema hakuna watu wajinga dunian kama walibya Leo hii wanao nufaika na vita ni wale wale waasi walio mtoa madarakan gadaf pamoja na wamarekani kwa kupora Mali za wananch ambao sasaiv kila siku wanakufa baarin wakijitaid kukimbia kwao kwa sababu ya maisha magum Sasa ivi Libya Madada wanataman hata wapate mabwana kutoka buza ilimrad tu watoke kule motoni na mpaka sasaiv hawana jibu la kujibu ukiwauliza kwamba demokrasia mlikua mnaitaka mpaka mkamtoa gadaf mmeipata au ndio mmepoteza matumain yani siasa za waafrica zinafanya niamin mzungu alitufanya watumwa apo awali sababu tulipenda wenyewe Tena inaonekana tuliwaita mana sio kwa ujinga huu tunao ufanya


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa hawa jamaa wanatafta kuhararisha kwamba watakuja kuwatafta maghaidi kama ilivyo kwa somalia,kongo iraq ili kuja kuiba uranium na madin mengine
 
Pascali ni mzoefu wa uandishi wakufikisha ujumbe kwa wa lengwa kwa kutumia diplomasia ya hali ya juu. Hongera sana PM wamekusoma wamekusikia wasikupuuze wanfayie ushauri wako kazi kwa faida ya nchi.
 
Hakuna hofu hio USA siku hizi ashambulii nchi nzima kajifunza madhara Iraq na libya kwamba ukianzisha vikundi vidogo utazalisha magaidi check ISIS na utasababisha mfumuko wa wakimbizi ulaya pia ni gharama kubwa Sana kugharamia vita na kuijenga nchi pia.Wanatumia technology ya kuponda nyoka kichwa kama walivyofanya Iran wanapiga walengwa wasababishi wachache waletao vurugu wanakuwa chakula cha drones wanawaishwa kuzimu hii Ina faida kwanza uepusha kuuwa wengi wasio na hatia,kuharibu nchi,kuzalisha vikundi vya magaidi,kupunguza gharama za kugharamia vita ili kuwaondoa wawatakao,kuepusha vifo vya askari wao.Hawahitaji kutumia njia hizo kwetu ni kulazimisha tu uchaguzi uwe huru na haki chini ya usimamizi wa jumuia za kimataifa hadi kwenye kuhesabu kura hapa tayari watakuwa wameshawaondoa wasiowataka.Ukitaka kuiuwa ccm ni kuomba tume huru na uchaguzi huru tu
 
Bro utakuwa script writer wa MUSIBA siyo bure...🧐

Aisee kwa huo uandishi....

Everyday is Saturday...............😎
 
If you can participate in commenting on a dialogue that you call "nonsense", then you are really a nondescript
 
Jiwe ndiye tatizo la Tanzania. Kavuruga umoja wa kitaifa na wala usiwasingizie Marekani.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora mara elfu na elfu kuingia mgogoro na mataifa makubwa kwa masuala ya kibiashara.
Linapokuja suala la kuruhusu migogoro kwa sababu za kisiasa na demokrasia dhidi ya taifa ambalo hata hujapakana nalo...... ni ujinga na ushamba mkubwa sana.

Kuna watu wanaheshimika sana kutokana na kazi zao hasa uandishi. Bahati mbaya kati yao hawaamini hata katika maandishi yao wenyewe.

Kuingiza mjadala wa matokeo ya uchaguzi serikali za mtaa ni dhahiri unataka watu kuwa spotted.

Kuanzia # 46 hadi 54 naona ni janga kubwa kuliko tunavyolichukulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno mazuri sana ila muwe mnamshauri anko magu apunguze ubabe maana sio Kila muda mnakuwa watu wa kusifia tu
Mnamsifia sana mpk mnaboa wote nyie mtu gani unapenda kusifiwa tu
Asifiwe na mke wake sisi wengine hatuwezi
 
Nipe mfano wa maamuzi ya Makonda na Kabudi yaliyofanywa kwa level ya serikali ya JMT?

Kama Samia na Majaliwa Ni danganya Toto was kulaumiwa nani? Japo pia sikubaliani na hoja yako. Maamuzi ya nchi ielekee wapi yafanywe na Makonda kweli? Mnampa umaarufu hata yy mwenyewe hakuwahi kuutarajia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…