Binafsi Waandishi wa habari wenye upande kama huyu Pascal Mayala sikubaliani nao na ni watu hatari sana kwa Taifa.
Waandishi wa namna hii watatufikisha mahali pabaya.
Serikali inawakumbatia watu wa aina hii sababu tu wapo upande wa serikali, wakikosoa wanawapa kesi za uhujumu UCHUMI kama E. Kabendera.
Sasa mambo haya huanza taaratibu kama hivi.
Huyu anaandaa andiko lake na kuita wamarekani Mabeberu, huku akisifia ushindi wa asilimia 99.9% ni halali.
Hivi mtu yeyote mwenye akili timamu hili linaingia akilini?
Nchi ina mfumo wa vyama vingi, yaani katika asilimia 100, kuna sehemu ya asilimia ni upinzani, sasa iweje ushinde kwa asilimia 99.9?? Hilo wala hamfikirii na mnajiita wasomi wa PhD. Halafu unasifia kabisa ulikuwa uchaguzi huru na wa haki, huku vyama vya kisiasa vikisusia na kutoa malalamiko lukuki yenye ushahidi.
Marekani anaye wafadhili katika mambo mengi ya bajeti zenu anapowahoji na kuwapa tahadhari kwa matumizi mabovu ya fedha na mikopo yake, mnakaza shingo na kumuita Beberu.
Badala ya kuishauri serikali yako ijitathimini na kurekebisha mapungufu, unaleta kusifia. Hivi umeshajiuliza kuna malalamiko kiasi gani kila kona? Kuanzia watumishi na vyama vyao vya wafanyakazi sauti zimezimwa, vyama vya upinzani kesi kila mahali, hali ya UCHUMI mbovu, watu wanatekwa kila siku na watu wasiojulikana, mahakama zimekosa usawa watuhumiwa tu wananyimwa haki zao za dhamana na kulazimishwa kuomba misamaha ili hali ni mahabusu, wewe unaleta Usukuma tu.
Aina ya waandishi wa habari kama wwe (Pascal Mayala) walikuwepo Rwanda na walichangia kwa kiasi kikubwa yaliyokuja kutokea.
Sasa ushauri wangu kwako, endelea tu kuwa bora wa hicho unachokiamini, lazima kitakuja kutoa majibu Chanya kwako na hasi kwa walio wengi.
Jaribu kurudi katika enzi zako za Muandishi mdadisi na mchambuzi wa mambo kwa kina, bila kuwa na upande tena waziwazi.
Chambua habari acha ushabiki, jambo hilo ni hatari kubwa kwa nchi yako.
Sent using
Jamii Forums mobile app