Mkuu Paskali; andiko lako limekuja wakati murua.
Marekani hapiganii vita ya kuwavuruga watu ndani ya ardhi yake; wanapigana nje ya ardhi yao.
Marekani wanajua Tanzania bara CCM itashinda maana upande wa pili hawana credible and strong candidate kuzunguka Tanzania nzima apate kuaminiwa kuwa CiC.
Zenji hapo kuna sintofahamu maana Dr. Shein anamaliza muda wake na hamna kiongozi mwenye ushawishi na kujulikana kuliko maalim.
Marekani kaumia sana kwa JPM kukomaa na mikataba ya madini kuwa reviewed na ile tabia ya kupiga magoti na kuomba vimisaada ambavyo kama tukiamua kusimama kwa miguu yetu, tunaweza kutoboa.
Spirit ya kujiamini na kutowatetemekea mabeberu, jambo hilo sio dogo kwao. Hivyo basi, baada ya mtu wao wa UNDP alie-plan kuharibu 2015 election kushindwa plan yake; bila shaka wana contingency plan.
Tanzania tukisimama kama Wataifa na wamoja tutatoboa. Changamoto kubwa kuna wenzetu wana passport mbilimbili na ndo hao wanachonga sana kwenye mitandao ya kijamii, wanakejeli kila kitu as if hamna jema linalofanyika.
Hata usalama wa kutembea; kuingia sokoni, kuwasiliana kwa uhuru, mambo hayo Congo, Rwanda, Northern Kenya, Northern Uganda sio shwari. Marekani ana nini na Tanzania?
Hataki umoja wa kitaifa na utulivu wetu. Kuna wanawake watoto wa wakibwa walisoma best schools wakilindwa wazazi wao; sasa hivi wana activate mimba ruksa kwa wanetu ili hao wenye mimba pia wasome.
Badala ya ku-deal na umasikini na ujinga; tuna wapiga debe wa kutetea wenye mimba wasome badala ya kusimama kama wataifa kukomaa kudhibiti vitendo vinavyoweza kusababisha mimba. Struggle zipo kwenye outcome badala ya ku-deal na source.
Wamarekani watatumia wenzetu na wanawatumia kutugawa. Wanajua a divided house can not stand still.
Mbona Congo DR uchaguzi Kabila aliuvuruga na wakala nae deal za kulinda maslahi yao. Toka lini chaguzi za Afrika zikawa kipaumbele cha Marekani?
Marekani anajua linchi hili lina utajiri na kuna wajinga wengi japo wana vyeti vya shahada za uzamili na uzamivu. Tamaa yao ni kama Esau; wako radhi kula dengu sasa at expense ya haki yao ya uzaliwa wa kwanza.
Umoja wetu ni kukubaliana kutokubaliana huku tukiendelea kuwa wana familia Watanzania.
Tukiruhusu kuwasikiza vibaraka na kuwapa nafasi, Marekani haitasita kutuvuruga.
Nyoka alimhadaa Eva kwa uongo na kweli; majasusi wa Marekani wanajua deception huwa ina work pale unapomhadaa Eva ili tokea hapo iwe rahisi kumfikia Adam. Adam akivurugikiwa tu; ndo tiketi ya kuondoka Eden inafika hapo hapo.
Libya wangejua; Iraq wangejua, wasingewasikiza Marekani.
Kwa mtu alisoma kitabu cha Robert Kaiyosaki mwanajeshi na rubani wa ndege za kivita aliepigana vita ya Vietnam, atakubalina kuwa CIA ni Capitals Invisible Army. Na mapepari wa kijeshi kama nzige. Wakitua kwako na ukawaruhusu...loh
Tanzania ni kubwa na tuna wajibu kuilinda kwa nguvu zetu na akili zetu zote.
Uzalendo ni pale hata kama hatujawa enlisted as men and officers in uniforms kupigana hata kwa kombeo kama la Daudi ili kumshinda Goliath baba la mabeberu na wanyonyaji.
Sent using
Jamii Forums mobile app