Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Paschal wewe mwanasheria wa aina gani. Umeishutumu Marekani kwa taarifa za hisia. Na hili ni taifa kubwa ambalo uwezo wake wa kiintelijensia sio habari za kijiweni kwako. Umetumia kitu ambacho tunakiita STATEMENT OF FACT kisheria. Bw Mayala unaweza kudhibitisha pasipo shaka madai hayo. Usiingize taifa letu kwenye mgogolo wa kidiplomasia kwa sababu ya MATAMANIO yako ya uteuzi. Umepigania uteuz kwa mda mrefu.

Tulia siku itafika tu utakumbukwa. Yanayofanya na utawala wetu duniani tunaonekana. Acha tunyolewe. Waziri wa mambo ya nje wa Marekali ni wa pili kwa umaarufu na kimamlaka baada ya Raisi wao. In fact anasauti kuliko hata VC wao. POMPEO ni jausi bobezi na amekuwa mkurugenz wa mashirika ya ujasusi wa Marekani kwa mda mrefu. Sio mtu kukurupuka. Yajayo yataneemesha demokrasia ya Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe anaweza kuwa kisababishi cha taifa letu kuanguka kama sio kufikia kugawanyika kama Somalia ya zamani ambayo sasa hivi ni nchi mbili ,naweza kusema kwamba Namna ya anavyoongoza hasa kuwa mtu asie kidiplomasia ,kauli n.k ujue uongozi wa nchi kwa zama za leo inahitaji kutumia akili nyingi sana

Hivyo wanavyowatukana vizazi vya leo vya wazungu kuwa mabeberu, wanyonyaji na majina mabaya mabaya sio kama hao wanaoitwa hivyo hawajui ,dunia ya leo ni kijiji hii sii ile ya zamani vyombo vya habari ni magazeti pekee

Kingine kitendo cha kumaliza miaka mitano hajatembelea taifa kubwa hata moja hii haijakaa vizuri

Why hao mabeberu waingie kuivuruga nchi yetu wakati wa jiwe na si wakati wa JK ,Mkapa etc?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali, Hiyo # 2 umeandika wewe kwa hiari yako ukiwa na akili yako timamu?, sitaki kuamini haraka haraka, hivi kulikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa au kulifanyika uchafuzi?, Paskali hao watu unaodai wanaweza kutumiwa na mabeberu kuchokoa na wewe pia unafanya kazi hiyo ya kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Hivi kweli kuna demokrasia hapa Tanzania unayotaka kulazimisha watu na jamii ya kimataifa kuamini?,
Ulishaona wapi duniani, uchaguzi wa vyama vingi chama kimoja kikashinda kwa 99%?

Ni lazima uwe chizi kwanza kuamua kuandika hayo uliyoandika, watu hawataletwa hapa kuja kuchokoa bali watakuja hapa kuonesha jamii ya kimataifa uozo ulijificha nyuma ya pazia, Unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za kiraia unaofanywa na serikali hii dhalimu hakuna mtu aweza kuuvumilia, washauri serikali waache Sanduku la Kura lisimame lenyewe, washauri waeke pembeni Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi ili tufanye siasa FAIR PLAY.
 
Kinachoziangamiza nchi nyingi za Afrika ni hypocrisy ya raia wake kama wewe mleta uzi.

Fact is the chance for USA to win hiko ulichokiandika ni 98%. Unajua ni kwa nini?

Nchi imepasuka vipande vipande haina mshikamano kabisa. Unajua ni kwa nn hamna mshikamano?

Sababu zipo kibaaao na unazijua mwenyewe. Lakini kikubwa ni siasa za ghilba, vitendo vya kighilba na kinyanyasaji vinavyotendeka katika nyakati hizi ambavyo raia walikuwa hawajavizoea mfano watumishi kunyimwa haki zao, wakulima kunyanyaswa, wafanyabiashara ndio full kibano mpaka hawana hali.

Siku zote ukitingisha status quo iliyopo na ukataka kuleta changes lazima ufuate taratibu nzuri ambazo majority watakuunga mkono. Sasa ukidisturb status quo iliyopo na majority wakawa hawakuungi mkono kuna uwezekano mkubwa sana wa kufeli.

Siku zote washindani wako wakitaka kukurudisha nyuma basi wataanza kutingisha hali yako ya ndani (internal status quo). Ukitingishika ndio wanapata nafasi ya kukumaliza. Kama ukiwa stable internally hawataweza.

Sasa kwa hali iliyopo sasa hapa nchini unadhani nani mwenye kubeba hizi lawama? Wewe unawalaumu mabeberu bure, wale wanatafuta ulaji, wakiona kuna mtu kaachia tundu la ulaji mahali unadhani wataliacha lipite hivihivi? Unashangaza sana umeweza kugundua kwamba wanapanga kitu hatari kwa nchi yetu na ukashindwa kujua hali iliyopo ndani ndio itaruhusu watufanye chochote.

Solution ni watawala wairudishe nchi kwenye form yake, watu wawe satisfied na hali iliyopo hata kama hakitoshi lkn wahakikishe raia wameridhika na hali. Bila hivyo vijana wenye njaa mtaani na hawana la kushika unadhan akipewa dola 1000 na ahadi nzuri nzuri then akashikishwa bunduki unadhani atakataa? Hawez kataa sababu hana other options.

Unforgetable
 
Mi ninachoamini waafrica wengi hatuna roho ya utu hasa tukishika makali. Afadhar wazungu wanatufanya tuwe watu kidgo. Nakmbuka hata kjjn miaka ile tukiwa wadogo kuna wazee walikua wakali na wakatili kwa watoto wao. Penye kuonya waliadhibu kw kutumia nguvu kubwa sana..kuna watu waliweza kukimbia mpaka wakarudi baada ya wazazi wao kufarki!

Serikali nyingi za kiafrica kama wazungu wasingekuepo kuingilia Kati basi raia wangepata tabu sana. Kwanza wasingekubali kuondoka madarakan asilani. Mfano. Seseko Moboto,Charles Taylor,Chad former President Jina sikumbuki.

Hawa ni mifano tu. Mtazamo wangu kama Western world isingekuepo Hali ya siasa zetu zingekua zakinyama sana!!Tusiwachukie wakat mwingne ni wasulihishi wetu mambo yanapokua Mrama!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coaster2015,
Hiyo #2 ni kichocheo kinachoweza kumpatia nafasi serikalini dakika za lalasalama, Pasiko ni mjanja anajua analolisema kwani Post hii ameileta baada ya naibu balozi wa Marekani kukutana na mhe. Hamad huko Zanzibar.
 
Pascal wewe ni Musiba type tu mnatetea matumbo yenu badala mtetee wananchi masikini wa nchi hii walio kwenye kipindi kigumu mno. Mkapa na Kikwete walipiga hatua nzuri sana kwenye uchumi wa nchi hii na wananchi tulianza kunenepa lakini leo masikini suruali zote zimepwaya, njaa kali mtaani.

Wewe uliwahi kujitutumua siku moja tu siku ulipomuuliza swali gumu Pres lakini baada ya hapo ukawa msaliti kuliko wasaliti wengine wewe hujiulizi Marekani atuchukie sisi kwa kitu gani hasa, miaka yote hiyo wamekuwa washirika wetu kwa nini sasa? Jambo unalotakiwa kulifahamu ni kwamba Marekani wasichopenda ni kuona kiongozi anajifanya Mungumtu.

Ajira hakuna, Maji tatizo, Mauzo ya nje yameporomoka, Bei za mazao kama pamba, kunde, korosha na n.k zimeporomoka, demokrasia, uhuru kutoa maoni na haki za binadamu zimeporoka kupita kiasi, Wazee waliofanya kazi kubwa kwenye hii nchi leo wanadhikiwa na kutukanwa na watoto wanuka mikojo. Nyie wachumia tumbo mnaona sawa tu.

Ukiona awamu inaita nchi za Ulaya, Marekani na Canada mabeberu sijui mabepari alafu at the same time inaita Wabunge na watetezi wa Wananchi Wasaliti! Ogopa sana hiyo awamu maana inatupeleka kuwa kama Zimbabwe ya Mugabe, North Korea, Burundi, Cuba na Venezuela yaani wananchi tunaishi maisha magumu huku viongozi wananenepeana kwa kodi zetu wakilala wakiamuka wananatukana mabeberu.

Wakati marekani hata hajui kama tunamjadili huku yuko bize na mambo makubwa huko ya duniani huko, Hata uangalie CNN siku 365 na robo huwezi msikia Trump kataja hii nchi yetu lakini sisi tuko bize oooohhh beberu dah tunaofutilia mambo tunashangaa mno.

Paschal sema tu kama unataka u-DC mzee sio unakaa anaropoka ropoka sijui we mzalendo kwani nani asiye mzalendo hapa. Wajuzi wa mambo tushawajua mno wazee wa kujipendekeza U-DC utapata ila Ubalozi mzee SAHAU[emoji5][emoji5][emoji5]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Mkuu naona umeshusha mzigo mrefu sana (Haujawa precisely) .Ila hoja ulizoshusha zima mashiko kwa manufaa ya nchi yetu. Je Us wanampango wa kufanya kama walivyofanya libya? Jibu ni hapana Tanzania iko very stable baada ya uchaguzi 2020 hakuna wa kuleta fyoko fyoko. Ghadafi aliponzwa na uroho wa madaraka na kufanya nchi kama ya familia yake na watu toka Sirte alikozaliwa (Hapa Tz hayo hayapo).

Je, Tanzania kuna vikundi vyenye mahusiano na magaidi? Jibu ni ndio. Kwenye shambulio ka kigaidi la Al shababu kule Garissa Kenya kuna Mtanzania alikamatwa na mpaka sasa ameshahukumiwa (jina kapuni) huu ni ushahidi kuwa terrorist cell zipo hapa Tz sababu ndugu zake walijua yupo shule. Kumbe alisha zama somalia kula mafunzo.

Je Tanzania kuna mfumo dini wa kikristo? Jibu ni hapana. Rais aliyepita alikuwa muislamu. Awamu hii ya Tano makamu wa rais ni Muislamu pia Waziri mkuu ni Muislamu (hoja ya udini inatumiwa na watu wenye nia ovu).

Jambo la msingi ni 'jamaa zako' kuwa makini maana kwenye nchi lolote linaweza kutokea. Miaka ya 1993 mpaka 1998 kulikuja makundi ya kiislamu toka pakistan na sehemu mbali mbali ambayo tulikuwa tunaambiwa ni waeneza dini.

Hawa jamaa walikuwa na midevu kama ya Osama. Baadae kidogo 1998 balozi za Us hapa kwetu na kenya zilipigwa mabomu. Jambo ambalo linawashangaza watu ni pale Alqaeda walipokuja kukiri kuwa mmoja wa kiongozi wao Alifariki kwenye ajali ya Mv Bukoba.
 
Pascal Mayalla,
Mimi utawia radhi kidogo kwa kuchangia nje ya hoja zako. Nakutazama wewe zaidi kwa kukuambia kuwa;

1. Pamoja na kuwa tunaambiwa tusiwe wavivu wa kusoma maandiko, hili lako linachosha sana na ku-bore. Halitoi hamasa msomaji kutaka kusoma zaidi na zaidi

2. Nadhani shida siyo kwamba huna hoja, bali shida iko kwenye mtindo (style) wako wa uandishi.

3. Ungeweza kulifupisha andiko lako kwa hoja zisizo zidi tano tu na ukaeleweka vizuri sana!!
 
Back
Top Bottom