zabron k
JF-Expert Member
- Nov 11, 2015
- 943
- 1,107
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ni kweli watanzania hawavutiwi na mfumo wa uendeshaji wa serikali yetu mbona katika uchaguzi wa serikali za mitaa CCM imepata ushindi wa 99%??
Tanzania tuna akiba ya dola bilioni 4 zinazoweza kuendesha nchi kwa miezi minne.Marekani hatuwezi.Sisi ni donor country.
Mbona uhoji wapi walipata silaha wale walimshambulia Mh Lissu ndani ya eneo ya eneo la bunge?.Paskali umeshusha nondo nzito kwa kweli, tena umezishusha muda muafaka, wakati huu ambapo kila tukiamka tunasikia wakristo wamechoma Quran, then wakachoma Juzuu, haya matukio yakufuatana hivi hayapangwi kweli? na kwanini yaje wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu?
Hapa ninachoona, kuna jamaa wameshaona hali yao kisiasa ni mbaya, kuanzia ndani ya nchi, ndani ya chama chao, mpaka nje kwenye mahusiano na jumuia za kimataifa, sasa wanachojaribu kufanya ni ku-divert attention, tutoke kuwaza yaliyotokea hivi karibuni ( kumbuka zuio la wamarekani kwa mkuu wa mkoa wa Dsm), watulete kwenye mambo ya kidini ili wapate ahueni kisiasa.
Pia, maswali yako kuhusu hayo yanayoitwa extremist groups kwenye hiyo mikoa mitatu uliyoitaja, hebu tujaribu kukumbuka yale matukio ya Rufiji wakati ule yalivyotokea, utapata picha kwamba hali ya usalama hasa ukanda wa Pwani hairidhishi, wale watu walitoa wapi silaha za kufanyia yale matukio? kama yale yaliwezekana kwanini hayo wanayosema sasa yasiwezekane? na habari kwamba wapo wanaofanya mazoezi ya "karate" misikitini zipo muda mrefu tu, pia wale wasomali ambao huwa wanakamatwa kwenye malori wakisafirishwa, je, wote hukamatwa?.. sidhani, na kama wapo wasiokamatwa huwa wanaishia wapi?
Kwa ufupi usalama wa nchi yetu sio wa kuridhisha hata kidogo, ndio maana kwangu mimi naona bora nifunge mdomo kuliko kupinga hiyo kauli kwamba kuna makundi ya wenye itikadi kali kwenye hiyo mikoa mitatu, tena inawezekana ikawa zaidi ya hiyo mitatu.
Mwisho kabisa, mchawi wa mengi kati ya hayo uliyoandika ni viongozi wetu wenyewe, waache ukatili dhidi ya raia, wawe na mioyo mipana, wakubali kukosolewa, na wajue anaekukosoa sio adui, ubabe kwenye dunia ya sasa hauna maana, hivyo kwa hili pia siwezi kumlaumu Marekani, inshort, tumevuna tulichopanda.
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji106]Kama ni kweli kwa nini Tishio hili litokee kwenye utawala huu? Lazima kuna shida mahala ktk utawala huu na tusitafute mchawi na ubabe wetu usio na maana
Sent using Jamii Forums mobile app
True taifa lolote lenye umoja ni ngumu kulisambaratisha kosa kubwa alilofanya Gadaffi na saddam ni kutowaunganisha watu wao.Jiulize mbona Iran imeshindikana kuisambaratisha sababu ni moja.Taifa lolote lisilo na umoja haiitaji dakika kulisambaratisha je ni nani chanzo cha kuvunja umoja wetu?Ni rahisi sana serikali kuyaepuka hayo yote kama serikali ikijitahidi kuwatengenezea mazingira mazuri vijana wa Tanzania maana wao ndio watakao tumika kwenye machafuko yoyote yale yatakayo pangwa na hao mnao waita mabeberu.
Cha msingi [emoji117]serikali ijitahidi sana kutoa ajira kwa vijana ikiwemo fursa za kujiari zinazo eleweka na sio za ki babaishaji
Nazungumzia vijana maana wao ndio wahusika wakuu watao tumika katika ushawishi wowote ule.
Na ihakikishia serikali ikifanya hivyo mbinu za mabeberu kujaribu kuihujimu Tanzania yetu haita fanikiwa kamwe maana watanzania ni wazalendo sana na nchi yao kama viongozi wakiwa wanawajali.
ona ili nalo..Mkuu hawa majamaa wametupima na kujua kuwa udhaifu wetu upo kwenye dini.
Hiyo itakua njia rahisi ya kutuvuruga.
Huko kwenye sekta ya madini wameona wanapoteza.
Fahamu kuwa, Sekta ya madini mabeberu wamejaza majasusi wastaafu ndio wanaofanya hizo shughuli. ( Inabidi pia na sisi tuweke assests wetu huko, tena wale wazalendo haswa)
Kwakua sekta ya madini ni muhimu mno, na kuwabana huko ni kuwanyima ulaji hawana namna zaidi ya kuretaliate.
Serikali inapaswa kuwa makini mno, kwenye maswala ya Udini na hasa Uhaguzi wa 2020.
Kila la heri mama Tanzania.
Libya walikuwaje?Mitanzania mijinga sana yaani hata kujifunza kwa waloharibiwa nchi zao kwa hila ka hizi(Libya) .. Endeleeni kushadadia tuu ujinga mkidhani marekani anajali hii nchi..
Nyie ngojeni tuuu si mnajifanya wajingA
Sent using Jamii Forums mobile app
Marekani inapaswa kuwachukulia hatua mapema wote wanaoashiria uvunjifu wa amani hii itaipunguzia dunia kuingia gharama za kuhudumia wakimbizi ni heri wachache waliokosa malezi bora wakaangamizwa ili ibaki salama.Kuna watu walitakiwa wabakie kuzimu wamsaidie ibilisi kazi na sio kuwaleta duniani kuwaumiza wengine Mungu alikosea sanaPascal Mayalla,
Paskali, nadhani unatakiwa kuwaambia hao watawala ndio wawe makini, unaposema tuwe makini sisi sikuelewi kabisa, sijasoma maelezo yako yote kwani yanakatisha tama hata kuyasoma yote, (kwa kutumia heading yako tu), mimi naona Marekani wanachelewa tu, wangechukua hatua ya wanachotaka kufanya ile tujue kinachofuata.