Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Dah...
Aibu kubwa sana

Unajarbu kututahadharisha kuhusu Marekani kweli?
Ni mbali sana toka hapa tulipo,yote haya umeyajuaje bro?

Kwann hukufaham kuhusu mtawala ajae hatazorotesha imani ya waTz
Una imani na kusadiki juu ya bandiko lako,wakat mtu anayeongoza ameshindwa kutoa msaada wa tetemeko

Kiongozi atawachapa vp shangazi wa majaliwa?

Yawezekana usemalo ni kweli lkn ni utawala umeleta janga juu ya janga

Awamu ya 5 ni shetani mkuu

Ujue ya wao kutuletea shida,usijue waliompiga risasi lissu
Wapi binti mrembo Akwilina
Ubani wa 80m haufuti dhambi

Unachojaribu kutuambia ni namna mzee baba kayakoroga sasa anahanya
Amewapa sababu mwenyewe

Ni upuuzi wa madaraka
Upuuzi wa katiba
Upuuzi wa dola

Chama tawala hakina tija na maisha
Chaguzi mbovu

Raia hawana heshima na nchi yao

Kura yetu ndo kula ya kamati ya ulinzi na usalama wa nchi

Mwisho tusimame kama waTz kushinda ajae kutuvuruga

Baraka juu yetu




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nasema hivi, hao wamarekani waje hata leo jioni, hao magaidi kama bdo wamejficha porini watokee kbisa hata kesho asubuhi.
Huu ni ujinga, haiwezekani watu wanapotea, watu wanashambuliwa kwa SMG, risasi 20+, watu wanatekwa, wanateswa & no one cares, kama vile hii nchi ni ya watu fulani tu,... Binafsi hii hali inaniumiza sana.

Tulikua na viongozi makini wa CHADEMA na ACT huku kwetu ambao wamefanya vitu vnavyoonekana kwa mika mitano ya uongoz wao uliopita (ikiwemo kuwafanya polisi waonevu waheshim raia), mwisho wa siku CCM wamelazimisha kupitisha watu wao wajingawajinga, halafu wanatoka nje wanasema wameshinda 99.9%, Upumbav mkubwa sana, very stupid.

Serikali inaongozwa na mtu mmoja, yeye ndo mahakama, ndo bunge yeye tu anaepanga bajeti, wengine wanaonekana wanawezakfanya kazi kwa kupokea instruction ktoka kwake tu! No hii haipo sawa. Tuna 3 organs. Tuache kila mhimili ufanye kazi yake. Alie na kazi ya kupanga bajet afanye hvo. Wa kusimamia sheria nae afanye kaz yke. Mtu mmoja akilazmisha ayafanye yote ndo definition ya udikteta inapatkana.

Tukiruhusu hii iendelee, yatatukuta kama ya Libya, mwisho wa sku libya imeahndwa kabisa kua stable bila uwepo wa gadafi ambae ndo alikua anaendesha kila kitu.

Kwaio mtoa maada USITUTISHE, awa jamaa waje tu, labda itasaidia baadh ya watu wajitafakari waone kama hayo wanayofnya sio sawa. Hii nchi ni ya kwtu sote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi Waandishi wa habari wenye upande kama huyu Pascal Mayala sikubaliani nao na ni watu hatari sana kwa Taifa.
Waandishi wa namna hii watatufikisha mahali pabaya.
Serikali inawakumbatia watu wa aina hii sababu tu wapo upande wa serikali, wakikosoa wanawapa kesi za uhujumu UCHUMI kama E. Kabendera.
Sasa mambo haya huanza taaratibu kama hivi.

Huyu anaandaa andiko lake na kuita wamarekani Mabeberu, huku akisifia ushindi wa asilimia 99.9% ni halali.
Hivi mtu yeyote mwenye akili timamu hili linaingia akilini?
Nchi ina mfumo wa vyama vingi, yaani katika asilimia 100, kuna sehemu ya asilimia ni upinzani, sasa iweje ushinde kwa asilimia 99.9?? Hilo wala hamfikirii na mnajiita wasomi wa PhD. Halafu unasifia kabisa ulikuwa uchaguzi huru na wa haki, huku vyama vya kisiasa vikisusia na kutoa malalamiko lukuki yenye ushahidi.
Marekani anaye wafadhili katika mambo mengi ya bajeti zenu anapowahoji na kuwapa tahadhari kwa matumizi mabovu ya fedha na mikopo yake, mnakaza shingo na kumuita Beberu.

Badala ya kuishauri serikali yako ijitathimini na kurekebisha mapungufu, unaleta kusifia. Hivi umeshajiuliza kuna malalamiko kiasi gani kila kona? Kuanzia watumishi na vyama vyao vya wafanyakazi sauti zimezimwa, vyama vya upinzani kesi kila mahali, hali ya UCHUMI mbovu, watu wanatekwa kila siku na watu wasiojulikana, mahakama zimekosa usawa watuhumiwa tu wananyimwa haki zao za dhamana na kulazimishwa kuomba misamaha ili hali ni mahabusu, wewe unaleta Usukuma tu.

Aina ya waandishi wa habari kama wwe (Pascal Mayala) walikuwepo Rwanda na walichangia kwa kiasi kikubwa yaliyokuja kutokea.
Sasa ushauri wangu kwako, endelea tu kuwa bora wa hicho unachokiamini, lazima kitakuja kutoa majibu Chanya kwako na hasi kwa walio wengi.

Jaribu kurudi katika enzi zako za Muandishi mdadisi na mchambuzi wa mambo kwa kina, bila kuwa na upande tena waziwazi.
Chambua habari acha ushabiki, jambo hilo ni hatari kubwa kwa nchi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asikusumbue Mayala maana yake ni NJAA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe Pascal Ina maana mpaka sasa hivi hujaelews tu mtu kaishaingia kwenye kumi na nane za mabeberu,Imebaki muda tu, kwahiyo bandiko lako halimsaidii chochote anakwenda na maji .
 
Pascal anatafuta uteuzi kwa muda mrefu sana, mwaka 2014 au 15 nikiwa na jamaa yangu tulikutana naye Moro kwenye 8 8 akawa anatuuliza jambo huku akijiona yuko juu tumnyenyekee, tukaishia kucheka tu.
Paschal wewe mwanasheria wa aina gani. Umeishutumu Marekani kwa taarifa za hisia. Na hili ni taifa kubwa ambalo uwezo wake wa kiintelijensia sio habari za kijiweni kwako. Umetumia kitu ambacho tunakiita STATEMENT OF FACT kisheria. Bw Mayala unaweza kudhibitisha pasipo shaka madai hayo. Usiingize taifa letu kwenye mgogolo wa kidiplomasia kwa sababu ya MATAMANIO yako ya uteuzi. Umepigania uteuz kwa mda mrefu.

Tulia siku itafika tu utakumbukwa. Yanayofanya na utawala wetu duniani tunaonekana. Acha tunyolewe. Waziri wa mambo ya nje wa Marekali ni wa pili kwa umaarufu na kimamlaka baada ya Raisi wao. In fact anasauti kuliko hata VC wao. POMPEO ni jausi bobezi na amekuwa mkurugenz wa mashirika ya ujasusi wa Marekani kwa mda mrefu. Sio mtu kukurupuka. Yajayo yataneemesha demokrasia ya Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni Magufuli hapa acheni kujiuma uma!, Kwanini nimchukie beberu anaye muhimiza kiongozi wangu asiniteke wala kuniuwa???....... Nikiwa mtekwaji/muuliwaji mtarajiwa, beberu huyo kwangu ni mkombozi.
Kweli kabisa mabeberu wanataka Jiwe,si waje wamchukue tu waende nae wa nini kwanza.
 
Kitu kimoja tu bila kujali chama tusiharibu amani na utulivu wa nchi tufanye siasa safi tushindane kwa hoja bila uadui ila sasa naomba walioko madarakani kuweka mfumo wa haki na uhuru wa kuongea haijalishi unapenda au hupendi kusikia watu wawe uhuru wa kuongea ila kuchochea kuvunja amani isikubalike. sasa sisi kauli zote za kupiga marufuku haki sio sawa mbaya zaidi ikifika wakati mtu hana imani na vyombo vya usalama au mahakama basi ishara mbaya sana ni lazima tuweke mahakama zetu huru kabisa ili sehemu ya kwenda kudai haki na ukishindwa basi uwe umeridhika kuwa haki imetendeka bila kuwa na vitu hivi sio usalama tu utakuwa hatarini hata uwekezaji hautakuja. uchaguzi ni suala lingine linahitaji tume huru 100% lakini hata baada ya uchaguzi system ya kimahakama iwe sehemu pekee ya mtu kukimbilia haki akiona amekosa sehemu ndio msingi bora wa amani.
 


Naunga mkono hoja hii
Tanzania is a Sovereign State, kamwe tusikubali kuingiliwa mambo yetu ya ndani.
Uchaguzi ni mambo ya ndani

P

Mkuu Paskali,
Mimi nimesoma House Resolution 1120.Vilivyoandikwa hmo ni kweli vimefanyika.Hakuna ambacho kimetungwa au tumesingiziwa.Pili kuhusu uzito wa hii resolution Unaona madai wanayodai ndio ambayo hata wewe unayadai na hata mimi ninadai.

Ukweli ni kwamba kwa mujibu wa sheria za sasa hivi.Hii comment yangu tu inaweza kuonekana ninkosa nisipochagua aina ya maneno.Nakushangaa sana Paskali unapotaka kusema wabaya wetu ni USA ilhali tatizo tulilianza wenyewe,Tuliwanyima wapinzani nafasi ya kusema ndani ya nchi wakatafuta wa kuwsemea nje ya nchi.Mlitaka kwa sababu mmewabana ndani ya nchi wafanyaje?

Mimi ninachoona ni muendelezo wa uzandiki wako wa kuogopa kusema kile ambacho unakiona ambacho ni hiki "CCM pamoja na RAIS wao hawana kabisa nafasi wala mvuto wa kuipeleka hi nchi mbele.Wanawatia wananchi HOFU na WASIWASI na kusahau kwamba tuna KIZAZI CHENYE HASIRA ambacho hakijui hofu wala mashaka na hakuna namna unaweza kukibadilisha.

HIKI kizazi hakihitaji Mmarekani ili kiendelee Mbele.Hakihitaji mwanasiasa ili kichukue hatua.KITACHUKUA hatua kwani Kinafahamu haki na wajibu wake.Ni kizazi cha KUHOJI.

Pole sana Paskali kwani naona JITIHDA zako za kujikomba bado hazizai matunda.
 
Mkuu Paskali,
"CCM pamoja na RAIS wao hawana kabisa nafasi wala mvuto wa kuipeleka hi nchi mbele.

Pole sana Paskali kwani naona JITIHDA zako bado hazizai matunda.
Mkuu andoza , ama kweli tuna watu wana macho lakini hawaoni, na masikio lakini hawasikii!, hivi maendeleo yote haya yanayofanyika na yaliyofikiwa hadi Tanzania kuingia nchi ya uchumi wa kati hautaoni?!.
Hebu panda gari pita Ubungo uone mambo!.
Uchaguzi 2020 - Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli
midege ile hujaona?
SGR?, Stigler?, etc, etc
P
 
Mkuu andoza , ama kweli tuna watu wana macho lakini hawaoni, na masikio lakini hawasikii!, hivi maendeleo yote haya yanayofanyika na yaliyofikiwa hadi Tanzania kuingia nchi ya uchumi wa kati hautaoni?!.
Hebu panda gari pita Ubungo uone mambo!.
Uchaguzi 2020 - Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli
midege ile hujaona?
SGR?, Stigler?, etc, etc
P
Mkuu Paskali;
Kama uamuzi wa kuchagua kiongozi unafanywa kwakuangalia flyover basi bado uko katika zama za ujima.Mimi binafisi naamini kwamba Uongozi una mambo mengi ya kutazamwa besides-Midege.Hebu ondoa hio midege na Madaraja halafu Umpime bila hio the uniambie kama anafaa kuwa kiongozi wetu.na kwa sababu zipi ndipo utaelewa.
 
Back
Top Bottom