Paskali umeshusha nondo nzito kwa kweli, tena umezishusha muda muafaka, wakati huu ambapo kila tukiamka tunasikia wakristo wamechoma Quran, then wakachoma Juzuu, haya matukio yakufuatana hivi hayapangwi kweli? na kwanini yaje wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu?
Hapa ninachoona, kuna jamaa wameshaona hali yao kisiasa ni mbaya, kuanzia ndani ya nchi, ndani ya chama chao, mpaka nje kwenye mahusiano na jumuia za kimataifa, sasa wanachojaribu kufanya ni ku-divert attention, tutoke kuwaza yaliyotokea hivi karibuni ( kumbuka zuio la wamarekani kwa mkuu wa mkoa wa Dsm), watulete kwenye mambo ya kidini ili wapate ahueni kisiasa.
Pia, maswali yako kuhusu hayo yanayoitwa extremist groups kwenye hiyo mikoa mitatu uliyoitaja, hebu tujaribu kukumbuka yale matukio ya Rufiji wakati ule yalivyotokea, utapata picha kwamba hali ya usalama hasa ukanda wa Pwani hairidhishi, wale watu walitoa wapi silaha za kufanyia yale matukio? kama yale yaliwezekana kwanini hayo wanayosema sasa yasiwezekane? na habari kwamba wapo wanaofanya mazoezi ya "karate" misikitini zipo muda mrefu tu, pia wale wasomali ambao huwa wanakamatwa kwenye malori wakisafirishwa, je, wote hukamatwa?.. sidhani, na kama wapo wasiokamatwa huwa wanaishia wapi?
Kwa ufupi usalama wa nchi yetu sio wa kuridhisha hata kidogo, ndio maana kwangu mimi naona bora nifunge mdomo kuliko kupinga hiyo kauli kwamba kuna makundi ya wenye itikadi kali kwenye hiyo mikoa mitatu, tena inawezekana ikawa zaidi ya hiyo mitatu.
Mwisho kabisa, mchawi wa mengi kati ya hayo uliyoandika ni viongozi wetu wenyewe, waache ukatili dhidi ya raia, wawe na mioyo mipana, wakubali kukosolewa, na wajue anaekukosoa sio adui, ubabe kwenye dunia ya sasa hauna maana, hivyo kwa hili pia siwezi kumlaumu Marekani, inshort, tumevuna tulichopanda.
Sent using
Jamii Forums mobile app