Sedoyeka: Katika bajeti ya mwaka 2022/23 Wizara imetenga fedha Shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kubuni, kuendeleza

Sedoyeka: Katika bajeti ya mwaka 2022/23 Wizara imetenga fedha Shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kubuni, kuendeleza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka amesema katika bajeti ya mwaka 2022/23 Wizara imetenga fedha Shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi ya kubuni, kuendeleza ubunifu pamoja na kujengea uwezo Taasisi na mbunifu mmoja mmoja.

Prof. Sedoyeka amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha pamoja na waandishi habari kuwajengea uwezo kuhusu Wiki ya Kitaifa ya Ubunifu inayoambatana na Kilele cha Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu inayotarajia kufanyika Jijini humo kuanzia Mei 15 hadi 20, 2022.

Amesema katika bajeti ya Mwaka 2021/22 inayoishia Juni 30 mwaka huu, kiasi cha Sh. bilioni moja kilitengwa kwa ajili ya kuendeleza wabunifu nchini ambapo tayari wengine wameshanufaika.

Aidha, amesema mpaka sasa Serikali imeshatumia takribani Sh Bilioni 2.3 kuendeleza takribani wabunifu 200 walioibuliwa na kutambuliwa na ubunifu wao kuingizwa kwenye kanzidata ya nchi.

“Wajibu wa Wizara pamoja na majukumu mengine ni kuibua, kutambua na kuendeleza ubunifu na teknolojia zinazozalishwa nchini na kuhamasisha matumizi yake katika kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii,” amesema Katibu Mkuu Sedoyeka.

Ameongeza kuwa sayansi na teknolojia ni muhimu duniani kote katika kuchochea kasi ya kimaendeleo, kiuchumi na kijamii na ndio maana Wizara imekuwa ikiwaibua na kuwandeleza wabunifu hao ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na hata utoaji huduma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Maulilio Kipanyula amesema mwaka huu jumla ya wabunifu 862 kutoka makundi ya shule za Msingi na Sekondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya Ufundi wa Kati, Mfumo usio rasmi, Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu wamewasilisha ubunifu wao kwa ajili ya kushindanishwa.

Ameongeza kuwa Wizara imeendelea kuandaa mazingira wezeshi ili wabunifu waweze kuonekana pamoja na ubunifu wao kuendelezwa kwa kushirikiana na wadau ili ubunifu uweze kufikia biashara.

Kwa upande wake Meneja wa Programu ya FUNGUO ya UNDP, Joseph Manirakiza amesema wamekuwa wakishirikiana na Wizara katika kuwaendeleza wabunifu, kutoa msaada wa kitaalamu kwa wabunifu hao kupitia kumbi za atamizi lakini pia kushirikiana na Serikali kuweka mazingira rafiki ya wabunifu katika kuendesha biashara.

Wiki ya Ubunifu Tanzania kwa mwaka huu ina kauli mbiu “Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu” na wabunifu 86 wameingia katika mashindano kati ya 862 waliowasilisha ubunifu wao.

IMG-20220504-WA0009.jpg
IMG-20220504-WA0010.jpg
IMG-20220504-WA0007.jpg
IMG-20220504-WA0019.jpg

IMG-20220504-WA0017.jpg

IMG-20220504-WA0018.jpg
 
Nchi inajengwa na wenye nchi..inaliwa na wenye meno.

#MaendeleoHayanaChama
 
Inapendeza sana, shida ni utekelezaji...
 
Back
Top Bottom