Sefu Musa adaiwa kuawa na askari baada ya kutuhumiwa kuwa mjangili Ngorongoro

Arusha -Babati
Ukunje pale Makuyuni?Then wamepitaje get ya Ngoro*2
Na mimi ndio hilo swali najiuliza, mtu anaeijua Arusha na miji ilioizunguka hawezi kukubaliana na huu uongo. Hakuna polisi anaependa kuua maana na wao ni wenzetu ni binadamu, labda katika kumdadisi kujua ukweli ndio jamaa akakata moto. Na unaweza kukuta hao waliokamatwa ni mtandao wa wao majangili ndio maana wanatumia pikipiki. Huwezi kupotea kihivyo Arusha to Babati ukapita hadi gate la Ngorongoro. Nawaza tu kwa kina.
 
Nani anaewapa mamlaka hayo ya kuuwa kila leo?
Hakuna sheria kabisa na wakubwa wao wako kimya.
Unamtuhumu mtu kuwa ni jangili kisa anapita hifadhi?
Na kwanini wanakuwa wakatili kiasi hiki
Vijana wamejieleza kwanini uwatese
 
Vita ya jangili na askari ni kuwahiana, so sometimes askari anaweza changanya raia na jangili. Nina mwanangu askari akikusimulia yanayo wakuta mbugani, utazani wapo uwanja wa vita ni kazi ngumu sana,wanadai majangili sometimes wanatumia mpaka ushirikina, kwani unaweza kumuona akijificha humuoni tena.
Hii inafundishwa kabisa jeshini, adui yako muwahi kabla hajakuwahi wewe, vita ni vita muraaa.
 
Hii inafundishwa kabisa jeshini, adui yako muwahi kabla hajakuwahi wewe vita ni vita muraaa.
Ndicho ninacho maanisha na hasa askari anapokuwa kwenye lindo ni sawa na kusema yupo vitani na ndio maana JWTZ hawataki kukaa wala kusogelea maeneo yao kabisa, hata kama gari lako likiharibika karibia na kambi ya jeshi watatafuta namna ya kukuondoa wanajua kuna hatari.
 
Inahuzunisha sana, ingawa hii habari kuna kitu hakipo sawa.Hivi mtu inawezekana utoke Arusha unaenda Babati ukapotelea Ngorongoro??? Kuna kitu, na hao wenzake aliokua nao waeleze ukweli tu?? Arusha kwenda Babati ni njia ya moja kwa moja haina kona hio, sasa hio kufika Karatu na wasiulize hata kwa mtu kama wamepotea??Au labda walikua wamelewa, Ila kwa wenyeji wa Arusha sio rahisi kupotea kihivyo. Kuna kitu hakipo sawa hapo. Tusipende kulaumu, poleni sana wafiwa.
Unaweza kuwa mwerevu zaidi? Hebu tukubali hisia zako... kuna kitu hakipi sawa. Kuua na kupiga ndiyo adhabu ya ''kitu kinapokuwa siyo sawa?''
 
Ndicho ninacho maanisha na hasa askari anapokuwa kwenye lindo ni sawa na kusema yupo vitani na ndio maana JWTZ hawataki kukaa wala kusogelea maeneo yao kabisa, hata kama gari lako likiharibika karibia na kambi ya jeshi watatafuta namna ya kukuondoa wanajua kuna hatari.
Ulimbukeni wa kukulia mbugani unawadanganya mengi.
 
Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Sefu Musa amefariki dunia baada ya kudaiwa kuuawa na askari watatu katika eneo la Ngorongoro mkoani Arusha, baada ya yeye na wenzake kutuhumiwa kuwa ni majangili.

Sefu alikuwa pamoja na Salim Hamisi maarufu Pachaa na Abdallah Nuru, wakitokea Arusha mjini kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kumzika mwenzao ambaye walikuwa wakifanya naye kazi ya kutengeneza magari maeneo ya Desemba jijini Arusha.

Watatu hao walikuwa wamepanda pikipiki moja na walipofika Makuyuni walipotea njia na kuelekea Karatu badala ya Babati. Waliendelea hadi Karatu mjini na kufika katika lango la kwanza la Ngorongoro lililokuwa likilindwa na askari watatu.

Baada ya kufika lango kuu la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro walibaini kuwa wamepotea njia na wakaamua kurejea. Inadaiwa walipofika katika lango la kwanza walikamatwa na askari hao na kutuhumiwa kuwa ni majangili, licha ya kueleza kuwa walikuwa wamepotea na walikuwa wakielekea Babati kwa ajili ya mazishi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah Nuru, ambaye ndiye aliyenusurika, vijana hao waliamriwa kuvua nguo na kujigaragaza kwenye majani yaliyokuwa yakiwasha huku wakimwagiwa maji na askari hao, kabla ya kudaiwa kupigwa.

Katika tukio hilo, Sefu Musa alidaiwa kuzidiwa nguvu na kupoteza fahamu huku Salim Hamisi naye akizimia. Abdallah anadaiwa kupata majeraha mbalimbali lakini aliendelea kuwa na nguvu na kuwasaidia wenzake.

Baada ya hali kuwa mbaya, inadaiwa waliambiwa wavae nguo na kuondoka eneo hilo. Abdallah alitafuta bajaji na kuwapeleka wenzake katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Walipofika hospitalini, Sefu alikutwa amefariki dunia huku Salim akiwa katika hali mbaya na kupewa huduma ya oksijeni iliyomsaidia kurejea kwenye fahamu. Anaendelea kupatiwa matibabu.

Abdallah Nuru ndiye aliyenusurika na kufanikiwa kuwasaidia wenzake hadi hospitalini licha ya yeye mwenyewe kupata majeraha. Mwili wa Sefu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha alipigiwa simu kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu taarifa hii, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

R.I.P sefu
Waliotenda watalipa.
 
Inahuzunisha sana, ingawa hii habari kuna kitu hakipo sawa.Hivi mtu inawezekana utoke Arusha unaenda Babati ukapotelea Ngorongoro??? Kuna kitu, na hao wenzake aliokua nao waeleze ukweli tu?? Arusha kwenda Babati ni njia ya moja kwa moja haina kona hio, sasa hio kufika Karatu na wasiulize hata kwa mtu kama wamepotea??Au labda walikua wamelewa, Ila kwa wenyeji wa Arusha sio rahisi kupotea kihivyo. Kuna kitu hakipo sawa hapo. Tusipende kulaumu, poleni sana wafiwa.
Hoja sio ujangili,hoja ni kuuliwa kwa kijana sefu Mussa,je polisi ana kibali cha kuidhisha kuua au ni mahakama oekee yenye uwezo wa kuidhinisha kifo?
 
Inahuzunisha sana, ingawa hii habari kuna kitu hakipo sawa.Hivi mtu inawezekana utoke Arusha unaenda Babati ukapotelea Ngorongoro??? Kuna kitu, na hao wenzake aliokua nao waeleze ukweli tu?? Arusha kwenda Babati ni njia ya moja kwa moja haina kona hio, sasa hio kufika Karatu na wasiulize hata kwa mtu kama wamepotea??Au labda walikua wamelewa, Ila kwa wenyeji wa Arusha sio rahisi kupotea kihivyo. Kuna kitu hakipo sawa hapo. Tusipende kulaumu, poleni sana wafiwa.
Na mimi nikusaidie kujiuliza hivi kwa maelezo ya huyo chalii anasema waliteswa na askari walio kuwa lindo la geti la kuingia Ngorongoro kwa akili ya haraka haraka ni jangiri gani anaweza kupita getini tena wakiwa na pikipiki na muda wote hapo getini kuna askari , tufanye basi kweli ni majangiri waliwakuta na siraha yoyote na kwanini waliamua kuwaachia ?
 
Kuna kitu wengi hawajaelewa, mimi ni mwenyeji ngorongoro, kabla ya kufika geti la ngorongoro(gate no 1) hapo nyuma yake kuna barrier, mbele kidogo ya kona ya kuelekea mountain lodge, hawa vijana wanasema walipita kwenye hiyo barrier bila shida( pale huwa kuna askari wawili au watatu na sijui walikuwa wapi muda huo) then walipoenda mbele ndiyo wakakuta geti kuu la kuingilia hifadhini (laobare) hapo ndiyo wakagundua wamepotea njia, na kuamua kurudi,

Sasa walipofika kwenye ile barrier waliyoipita awali ndiyo wakakuta askari wamerudi na kusimamishwa na kufanyiwa walichofanyiwa, kwa mujibu wa maelezo ya kijana aliyenusurika na kwa uzoefu wangu binafsi hivyo ndivyo ilivyokuwa.
 
Inahuzunisha sana, ingawa hii habari kuna kitu hakipo sawa.Hivi mtu inawezekana utoke Arusha unaenda Babati ukapotelea Ngorongoro??? Kuna kitu, na hao wenzake aliokua nao waeleze ukweli tu?? Arusha kwenda Babati ni njia ya moja kwa moja haina kona hio, sasa hio kufika Karatu na wasiulize hata kwa mtu kama wamepotea??Au labda walikua wamelewa, Ila kwa wenyeji wa Arusha sio rahisi kupotea kihivyo. Kuna kitu hakipo sawa hapo. Tusipende kulaumu, poleni sana wafiwa.
Hilo nimejiuliza sana, kutoka makuyuni hadi kufika geti la ngorongoro ni mwendo mrefu wa kutosha kabisa, kuna miji miwili mikubwa unaipita, mto wa mbu na karatu, sasa kote wamepita bila hata kuuliza ili wawe na uhakika na wanapokwenda...
 
Vita ya jangili na askari ni kuwahiana, so sometimes askari anaweza changanya raia na jangili. Nina mwanangu askari akikusimulia yanayo wakuta mbugani, utazani wapo uwanja wa vita ni kazi ngumu sana,wanadai majangili sometimes wanatumia mpaka ushirikina, kwani unaweza kumuona akijificha humuoni tena.
Hakuna jangili anapita getini Tena kwa pikipiki
 
Hilo nimejiuliza sana, kutoka makuyuni hadi kufika geti la ngorongoro ni mwendo mrefu wa kutosha kabisa, kuna miji miwili mikubwa unaipita, mto wa mbu na karatu, sasa kote wamepita bila hata kuuliza ili wawe na uhakika na wanapokwenda...
ukashindwa kujiuliza Kama Kuna kosa lolote wametenda na Kama kufika hapo gate 2 ni kosa

Je walikua na kielelezo chochote Cha kuashiria ni majangili na ikiwa ndio mbona waliwaachia baada ya kuwapiga na kwanini wapigwe
 
Inahuzunisha sana, ingawa hii habari kuna kitu hakipo sawa.Hivi mtu inawezekana utoke Arusha unaenda Babati ukapotelea Ngorongoro??? Kuna kitu, na hao wenzake aliokua nao waeleze ukweli tu?? Arusha kwenda Babati ni njia ya moja kwa moja haina kona hio, sasa hio kufika Karatu na wasiulize hata kwa mtu kama wamepotea??Au labda walikua wamelewa, Ila kwa wenyeji wa Arusha sio rahisi kupotea kihivyo. Kuna kitu hakipo sawa hapo. Tusipende kulaumu, poleni sana wafiwa.
Tuseme kweli hawakupotea ila walikuwa majangili kama unavyotaka kusema.
Je walistahili hicho walichofanyiwa ?
 
Kama ni majangili kweli, ndio walistahili hicho walichokipata maana kwenye vita hio uwa ni mwendo wa kuwahiana, tuliopita jeshini tunafundishwa hivyo ni aidha adui akuwahi au umuwahi wewe. Mambo ya kuremba sasa hivi dunia imebadilika.
 
Kwenye vita.
Sasa pale walikuwa vitani ???

Na jeshini umefundishwa uue captured enermy ama mateka ambae umemdhibiti unamhoji maswali, hana silaha, hana alama ya uaskari wa adui, hana lolote ?

Na ni wapi jeshini au kwenye law enforcement wamefundisha kwamba suspected jangili au jambazi au gaidi au haini AMBAE HAJAONYESHA DALILI YEYOTE YA KUKUDHURU BASI HUYO NI HALALI YAKO ANAPASWA UMUWAHI KABLA HAJAKUUA BASED ON YOUR SUSPISCION ZAKO WEWE ?????? YANI JANGILI NI ENERMY COMBATANT ???

Get your dumb ass the hell outta here
 
Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Sefu Musa amefariki dunia baada ya kudaiwa kuuawa na askari watatu katika eneo la Ngorongoro mkoani Arusha, baada ya yeye na wenzake kutuhumiwa kuwa ni majangili.

Sefu alikuwa pamoja na Salim Hamisi maarufu Pachaa na Abdallah Nuru, wakitokea Arusha mjini kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kumzika mwenzao ambaye walikuwa wakifanya naye kazi ya kutengeneza magari maeneo ya Desemba jijini Arusha.

Watatu hao walikuwa wamepanda pikipiki moja na walipofika Makuyuni walipotea njia na kuelekea Karatu badala ya Babati. Waliendelea hadi Karatu mjini na kufika katika lango la kwanza la Ngorongoro lililokuwa likilindwa na askari watatu.

Baada ya kufika lango kuu la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro walibaini kuwa wamepotea njia na wakaamua kurejea. Inadaiwa walipofika katika lango la kwanza walikamatwa na askari hao na kutuhumiwa kuwa ni majangili, licha ya kueleza kuwa walikuwa wamepotea na walikuwa wakielekea Babati kwa ajili ya mazishi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah Nuru, ambaye ndiye aliyenusurika, vijana hao waliamriwa kuvua nguo na kujigaragaza kwenye majani yaliyokuwa yakiwasha huku wakimwagiwa maji na askari hao, kabla ya kudaiwa kupigwa.

Katika tukio hilo, Sefu Musa alidaiwa kuzidiwa nguvu na kupoteza fahamu huku Salim Hamisi naye akizimia. Abdallah anadaiwa kupata majeraha mbalimbali lakini aliendelea kuwa na nguvu na kuwasaidia wenzake.

Baada ya hali kuwa mbaya, inadaiwa waliambiwa wavae nguo na kuondoka eneo hilo. Abdallah alitafuta bajaji na kuwapeleka wenzake katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Walipofika hospitalini, Sefu alikutwa amefariki dunia huku Salim akiwa katika hali mbaya na kupewa huduma ya oksijeni iliyomsaidia kurejea kwenye fahamu. Anaendelea kupatiwa matibabu.

Abdallah Nuru ndiye aliyenusurika na kufanikiwa kuwasaidia wenzake hadi hospitalini licha ya yeye mwenyewe kupata majeraha. Mwili wa Sefu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha alipigiwa simu kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu taarifa hii, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

je ni matukio mangapi yanafanywa na askari wa wanyama bila kujulikana?ASKARI na SHETANI n ndugu
 
Kama ni majangili kweli, ndio walistahili hicho walichokipata maana kwenye vita hio uwa ni mwendo wa kuwahiana, tuliopita jeshini tunafundishwa hivyo ni aidha adui akuwahi au umuwahi wewe. Mambo ya kuremba sasa hivi dunia imebadilika.

Kwenye vita.
Sasa pale walikuwa vitani ???

Na jeshini umefundishwa uue captured enermy ama mateka ambae umemdhibiti unamhoji maswali, hana silaha, hana alama ya uaskari i wa adui, hana lolote ?

Na ni wapi jeshini au kwenye law enforcement wamefundisha kwamba suspected jangili au jambazi au gaidi au haini AMBAE HAJAONYESHA DALILI YEYOTE YA KUKUDHURU BASI HUYO NI HALALI YAKO ANAPASWA UMUWAHI KABLA HAJAKUUA BASES ON YOUR SUSPICION ZAKO WEWE ?????? YANI JANGILI NI ENERMY COMBATANT ???

Get your dumb arse the hell outta here
Umenivunja mbavu zangu, kwahio wewe Keyboard warrior unaona wale askari hawana akili yoyote mpaka wakawafanyia vile wale vijana?? Wale vijana ni mfumo wa majangili, iweje wapotee eti Makuyuni, waende wapite Mto wa Mbu, waende wapite Karatu hadi kwenye geti la Ngorongoro?? Jaribu kuishughulisha akili yako kidogo utajua walikua katika mission yao hao wakapambana na ajali kazini. Kwa akili za kawaida huwezi kupotea vile kutoka Arusha kwenda Babati.
 
Kwenye vita.
Sasa pale walikuwa vitani ???

Na jeshini umefundishwa uue captured enermy ama mateka ambae umemdhibiti unamhoji maswali, hana silaha, hana alama ya uaskari wa adui, hana lolote ?

Na ni wapi jeshini au kwenye law enforcement wamefundisha kwamba suspected jangili au jambazi au gaidi au haini AMBAE HAJAONYESHA DALILI YEYOTE YA KUKUDHURU BASI HUYO NI HALALI YAKO ANAPASWA UMUWAHI KABLA HAJAKUUA BASED ON YOUR SUSPISCION ZAKO WEWE ?????? YANI JANGILI NI ENERMY COMBATANT ???

Get your dumb ass the hell outta here
Uwezo wao wa kufikiri ni zero, ndiyo maana hata Oct29 walingia vitani na kufyatuafyatua risasi hovyohovyo kukabiliana na warusha mawe.
 
Back
Top Bottom