Sehemu ya 2: Ajenda za Masih Dajjal, vita vya Gaza, Lebanon, Syria (Mashariki ya Kati ) na kuzaliwa taifa la Kiyahudi la Israel

nelo de nelo

Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
89
Reaction score
104
Sehemu ya 2



Kila sifa njema zinamstahiki Mungu wa pekee aliyetupa uzima, afya na ufahamu wa mambo haya. Rehma na amani ziwe nao manabii wa Mungu wote wakiongozwa na nabii wa mwisho nabii Muhammad swalla lllahu alayh wasallam pamoja MASIH Issa bin Maryam ( Yesu Kristo )

Ndugu zangu nichukue nafas hii kukumbusha kuwa tupo katika kipindi kizito cha fitna za masih wa dajjal ambaye lengo lake ni kutaka kuitwala dunia. Kama ilivyozungumzwa katika qur an na sunna kuwa tangu kuumbwa mwanaadam hakuna fitna kubwa kuliko hii. Ni fitna ambayo kati ya watu 1000 atakaesalimikia ni mtu m1 tu.Kama tulivyowah kusoma katika darsa zilizotangulia ni kwamba dajjal anataka kutawala dunia, na sharti la kutawala dunia ni lazima utawala huo uanzie ardhi takatifu kwa kuwa ndio Ikulu ya dunia hii. Yeyote anaetaka kuitawala dunia lazima kwanza aimiliki ardhi takatifu. Eneo hili ndipo baba yetu wa imani nabii Ibrahim alayh salaam alipokabidhiwa na Mungu kuwa awe mtawala wa dunia yeye na wanawe. Utawala huo ulianzia pale ardhi takatifu na kuenea dunia nzima. Point ya kubwa na ya msingi kuifahamu ni kuwa UTAWALA WA IBRAHIMU KUPITIA KIZAZI CHAKE ULIKUWA UNAFUATA SHERIA ZA MUNGU. HAWAKUJITUNGIA SHERIA ZAO KAMA ILIVYO LEO DUNUANI

Mwana wa Ibrahim wa mwisho kutoka kizazi cha Is haaq aliyetakiwa atawale pale ni Masihi Issa bin Maryam( Yesu Kristo ) alayh salaam. Baada ya wayahud kumkataa kwa kusema kuwa hakuwa MASIH ndipo Mungu akamleta kiumbe huyu dajjal kama mtihani kwa wayahud ( waliomkataa Issa bin Maryam ) na watu wote wa imani wasemao Ibrahim ndiye baba yao wa imani ( waislamu na wakristo ). Kwa kuwa Issa bin Maryam alikuja ili kurithi kiti cha enzi cha Daudi yaani ufalme ( utawala ) hivyo huyu anaejifanya kuwa ndiye masih ilhali ni muongo yaani ni dajjal ili akubaliwe na kuaminiwa na wayahud inabid azitekeleze ajenda ambazo zilitakiwa zitekelezwe na Masih wa ukweli ( Issa bin Maryam./ Yesu Kristo ). Katika harakat yake ya kutaka kuaminiwa na wayahud ndipo ilipo fitna kwa kuwa ili asijulikane kazi ya kwanza aliyoifanya ni kuwapofoa macho ya rohoni ( kuwauwa kiimani ) watu waliomkubali Issa bin Maryam kuwa ndiye Masih.Njia aliyoitumia kuwapofoa watu macho ya rohoni( imani ) ni kuwapambia dunia na mambo yanayohusu mwili. Kafanya hivi ili asionekane na kuifanya kazi yake iwe nyepesi. Wale watakaosimama na kuishika imani kwa mioyo yao kuuiishi hiyo kweli watafanikiwa kuziona fitna zake na wataweza kumuepuka kama ilivyoelekezwa katika qur an na sunna. Mpaka sasa anaendelea kukamilisha mission yake na mambo / matukio mengi yanayofanyika ni sehemu ya mipango yake lakin wengi katika watu hawajui kwa kuwa washakuwa vipofu, nao wanaona na jicho moja kama dajjal mwenyewe. Tukumbuke kuwa kuwa fitna zote anazifanya kupitia viumbe waitwao yaajuj na maajuj. Hawa ndio watendaji wake wakuu ambao katika wakat tulio nao wanajiita na kujulikana kwa jina la ZIONIST. Mambo mengi tunayoyaona na kuyasikia ni miongoni mwa mengi yanayofanywa sirini na watu hawa au wakat mwingine wanayadhihirisha kwa kuyapa majina au muonekano m baya kupitia vyombo vya habari wanavyovimilik. Leo hii kuna baadhi ya majeshi ya serekali za nchi yanatajwa kuwa ni jeshi la kigaid na watu wamekubal kumeza uongo huo bila kutafakar. Mfano Hizbullah ya Lebanon wanaitwa ni magaid wakat ni kikundi chenye viti bungeni pale Lebanon. Jeshi la Iran liitwalo IRGC nalo wanaliita mi jeshi la kigaid ilhal ni jeshi la nchi inayotambulika. Kiufupi ni kwamba Kupitia vyombo vya habari hawa jamaa wamefanikiwa sana kuwafanya watu kuwa wajinga. Wanaletewe uongo nao wanaumeza tu

Baada ya kuifahamu ajenda ya kwanza na namna alivyofanikiwa kuitimiza in shaa Allah leo tuiangalie ajenda ya pili iliyofanywa naa Dajjal ili kuwaaminisha wayahud kuwa yeye ndiye Masih

2: KUWAKUSANYA WAYAHUDI NA KUWARUDISHA ARDHI TAKATIFU ( Jerusalem )

Kama tulivyosoma katka somo lililotangulia na kufaham namna Dajjal alivyofanikiwa kuiteka ( kwa wayahud ni kuikomboa) ardhi takatifu hivyo kazi yake ya pili ikawa ni kuwarudisha wayahud na kuwakusanya pale ardhi takatifu ( Jerusalem ). Tukumbuke kuwa kazi ya kwanza ya kuiteka ardhi ilifanywa na askar wa Dajjal kutokea katika kisiwa ambacho ndipo alipofungiwa ambacho ni Uingereza ya leo. Ajenda hii ya pili ya kuwakusanya wayahud na kuwarudisha pale Jerusalem ilifanywa na askar wake walio katika kituo chake cha kwanza wakishirikiana na wale walio katika kituo pili cha harakati zake ambacho ni nchi ya Marekani ( USA ). Ilikuwa ni mwaka 1948 baada ya vita ya pili ya dunia iliyomalizika mwaka 1945 ambapo katika vita hivi Marekani ndiyo iliyoibuka na ushindi na kuwa taifa babe duniani mpk leo. Tangu kutekwa ardhi takatifu mwaka 1917 na kuanza kumilikiwa na Wayahudi wa Uingereza ambao kiasili ni wazayuni , ilipofika mwaka 1948 baada ya mshindi wa vita vya pili kupatikana ndipo alipotangaza rasmi kulitambua taifa HURU la Israel. Alikuwa ni Harry Truman rais wa 33 wa Marekani ambaye yeye kama mtawala wa DUNIA alisimama mbele ya vyombo vyao habar na kuutangazia ulimwengu habar za kuzaliwa upya kwa taifa la Israel na Marekani kuwa nchi ya kwanza kulitambua kama ambavyo Donald Trump alipouhutubia ulimwengu mwaka 2017 kwa kutangaza kuhamisha makao makuu ya Israel kutaoa tel Avivi na kuyapeleka Jerusalem na Marekani ikawa nchi ya kwanza kuhamishia ubalozi wake Jerusalem. Kwa sababu hizi ndio Marekani na Israel ni kama nzi na harufu mbaya. Hawa ni wale wale waliofanikisha ajenda ya kwanza ya dajjal na hapa wanaikamilisha ajenda ya pili.

Kuanzia hapo kazi kubwa ya Marekani ikawa ni kulijengea nguvu ya kiuchumi na kijeshi taifa hili lililozaliwa 1948 ndio maana mpka sasa Israel ni taifa dogo lililo kati ya mataifa yenye nguvu kubwa ya kijeshi duniani. Kukamilika kwa ajenda hii ya kupatikana taifa la KIYAHUD ( sio la wana wa Israel ) mwaka 1948 kumekuwa ndio sababu ya kuanza kwa vita kati ya Israel na Palestin mwaka 1950. Vita hii imesababishwa na kitendo cha wayahud kuwafukuza wapalestina katika maeneo yao na kuzibomoa nyumba zao kisha kujenga nyumba ambazo wakaazi ni wayahud. Hii ndio sababu ya vita inayoendelea mpka Leo pale Jerusalem Lebanon, Syria pamoja na Jordan.Baada ya kupatikana taifa hili kazi kubwa ikawa ni kuanza kuwarudisha pale wayahud wale waliofukuzwa. Kazi hii ya kuwarudisha ilisaidiwa na mjerumani ( mzayuni ) aliyetambulika kwa jina la Adolf Hitler. Walio kataa waliuwawa na ndio maana Htler aliwaua wayahud million 6 ( Holocaust ). Lengo la kuwauwa ilikuwa ni kuwapunguza na pia ni mbinu ya ujanja iliofanywa na wazayuni ili wayahud hawa halisi kutoka kizazi cha Israel waone kuwa kuish nje ya Jerusalem ni hatari kwa maisha yao kumbe wazayun walikuwa na mpango wa kuwatumia wayahud kama ticket ya kuwafikisha Jerusalem ili wafikie lengo lao la kuitawala dunia kutokea Jerusalem. Kuanzia mwaka huo mpk leo kazi kubwa ya wazayuni hawa ni kuwachukua wayahud kote duniani na kuwarudisha Jerusalem na ndio maana miaka michache nyuma waziri mkuu wa Israel aitwae Benjamin Netanyahu aaliwakusanya wayahud 9000 kutoka katika nchi ya Ethiopia na kuwarudisha Israel. Kitendo hiki cha kupatikan taifa linaloitwa Israel na wayahudi kukusanywa na kurudishwa pale Jerusalem baada ya kuwa walishafukuzwa kwa mujibu wa qur an ni miongoni mwa dalili za kiyama. Qur an. 17: 104 inasema

وَقُلۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ لِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱسۡكُنُواْ ٱلۡأَرۡضَ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأٓخِرَةِ جِئۡنَا بِكُمۡ لَفِيفٗا

Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaeni katika nchi . Itapo kuja ahadi ya mwisho tutakuleteni nyote pamoja.

Katika aya hii inaelekeza mambo yalivyokuwa baada ya kuangamizwa firaun aliewatesa wana wa Israel. Walipokoolewa wakaambiwa kaeni ardhi takatifu ( Jerusalem ) wakaa pale kwa muda wa miaka 80 chini ya utawala wa nabii Daud na mwanae Sulaimani alayhimu salaam.. Baadae wakumuasi Mungu kwa kuvunja utaratibu wa maisha ayatakayo Mungu na mwisho wakamkataa Masih Issa bin Maryam aliyekuja kuwarudishia utawala. Baada ya kumkataa wakafukuzwa pale. Ndipo katika aya hii Allah tabaaraka wataala akasema IKIFIKA NYAKATI ZA MWISHO TUTAKURUDISHENI NA KUWAKUSANYA SEHEMU MOJA ( KWA AJILI YA ADHABU )

Hapa tunaona kuwa katika harakati za Dajjal za kuwashawishi wayahudi kuwa yeye ndiye Masih waliyemsubir tayar kashawashawishi na washamkubal kwa kuwa kashawapa baadhi ya yale wanayoyahitaji na kashawatangazia taifa huru la kiyahud duniani. Tangu kuanzishwa kwa taifa hili eneo lote la middle East ( mashariki ya kati ) limekosa amani na kuwa ni uwanja wa mauaji na vita kati ya nchi hii ya wazayuni ( wayahud feki ) na wakaaz wa maeneo hayo. Yote hii ni kwa kuwa inataka kujitanua hivyo inalazimika kuchukua maeneo ya nchi jirani na hili linasababisha vita. Wanataka baadhi ya maeneo katika nchi za Misri , Iraq na Syria .Nchi ya Lebanon na Jordan zote zitafutwa ziwe ni ardhi ya taifa hili. Ndio maana walianza kuishambulia harakat ya Ukomboz ya Hamas pale Gaza baada ya kuhakikisha kuwa Gaza washaimaliza sasa wamehamia Lebanon wanapambana na harakat ya Hizbullah. Jambo wanaloitaka ni kutengeneza nchi iitwayo GREATER ISRAEL kwa kuyaunganisha maeneo hayo kuwa nchi moja.. Lakini pia kuzaliwa kwa taifa hili kumekuwa sababu ya ramani ya dunia kubadilika kwa kufutwa nchi ya Palestine na kuanzisha Israel yenye mipaka ndani ya nchi iliziozikuta. Ili kufanikiwa lengo lao imebid wapachike mistar ya kuhalilisha jambo lao kupitia kumbukumbu la Taurati ili wakat wanawafukuza watu wa nchi hizo ionekane kuwa ni utabir wa maandiko ya kwenye biblia..

Kumbukumbu la Torati 11:23-25

[23] ndipo BWANA atakapowafukuza mataifa haya yote mbele yenu, nanyi mtamiliki mataifa makubwa yenye nguvu kuwapita ninyi.

[24] Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.

[25] Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.

Hii ndiyo ajenda ya pili ya Dajjal anayoikamilisha akiwatumia wafuasi wake wanaojulikana katika qur an kwa jina la Yaajuja na Maajuja ambao ktk ulimwengu wa kisasa wanajulikana kwa jina Wazayuni, Illuminat ( wenye kuangazia ) au wajenzi huru ( Freemason) wa utawala wa shetani kupitia taifa la Israel.

In shaa wakat mwingine tutaendelea ili kuifahamu ajenda ya 3 na nyinginezo.....

Imeandikwa na Haji Mmbaga

0657453034
 
Dajjal/Anti-christ hayupo mbali, anakuja.

Ni adui wa wote, sio waislamu bali hata wakristo.

 
Mzee umebatizwa kwanza lakin. Maana hii story ndeefu bila kubatizwa ni kaz bure
 
Hivi mbona mnapenda sana kumshobokea Yesu Kristo? Mfalme wa wafalme.
 
Hawa waisraeli origin wako nchi gani? Kila siku mnasema wayahudi wanaoishi Israel ni take. Je wayahudi ambao sio take wako nchi gani?
 
Hawa waisraeli origin wako nchi gani? Kila siku mnasema wayahudi wanaoishi Israel ni take. Je wayahudi ambao sio take wako nchi gani?
Watakuambia kizazi kile "kilipotea" without any further elaboration.
 
Nimesoma Kwa kurudia sijaelewa yafuatayo
1. Mayahudi asili wapo wapi hasa?
2. Suala la kurudi kwao nchi takatifu lilitabiriwa na maandiko matakatifu inakuaje unalihusisha na hicho ulichokiandika na kukiamini
3. Kama Wayahudi wapo je unadhani watatakiwa kwenda kuishi nchi gani hasa?
 
Hawa waisraeli origin wako nchi gani? Kila siku mnasema wayahudi wanaoishi Israel ni take. Je wayahudi ambao sio take wako nchi gani?
Hili swali halijawahi kupatiwa jibu sahihi....

Mathanzua
 
Kama mnavyomsujudia huyo Masih dajal nguvu hizo mngezitumia kumsudujia KRISTO hakika vita hizi zisingekuwepo
 
Hichi kitendo walichokifanya Waisraeli hata Wakatoliki walikifanyq huko Spain na Portugal kuwaondoa wavamizi kwenye Ardhi yao bado Anatolia 😁

Leo ukienda Spain imebaki Misikiti ambayo imefanywa kuwa ni Makumbusho.
 
Hivi mbona mnapenda sana kumshobokea Yesu Kristo? Mfalme wa wafalme.
KILAZA CHA KIZAYUNI KIMEFOKA....hakijui chochote kuhusu yesu kristo maskini ya mungu
 
Huu Uzi, uzi makini ambao ili uelewe ni lazima kwanza ujue maandiko yaan Mkiristo au Muislam uwe na maarifa.


Hongera mwandishi .


Hiyo Jana Rais wa Uturuki Edogarn kaionya Israel isitegemee kuichukua Lebanon au Syria , Kwa maadai ya "Promised Land "....

Edorgan yupo tayari kupeleka Majeshi yake Lebanon .

Na anawaonya waturuki kua Kwa mipango ya Israel ,baada ya Lebanon au Syria ni Uturuki.


View: https://youtu.be/QfrxXbz0_oU?si=9vUMOsYULrUemyZR
 
Ni kweli kabisa ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…