Sehemu ya hotuba ya Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema katika UAPISHO wa Rais Samia

Sehemu ya hotuba ya Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema katika UAPISHO wa Rais Samia

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, akizungumza jana wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Tanzania, amesema kuwa njia pekee ya kuwalinda vijana wa kizazi cha Gen Z ni kuwapatia elimu, ujuzi, pamoja na fursa za ajira na biashara.

Aidha, amempongeza Rais kwa ushindi wake na kwa kuendelea kuwaongoza Watanzania kwa awamu nyingine, akimsisitizia umuhimu wa kuwapa nafasi wote waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kwa kutafuta mfumo rafiki utakaowafikia wote.

Rais Hichilema pia ameahidi ushirikiano wa karibu kati ya Zambia na Tanzania, hususan katika kuendeleza Reli ya TAZARA.
 
Back
Top Bottom