Sehemu yoyote ambayo unaweza kufukuzwa muda wowote usiwekeze nguvu nyingi hapo. Sehemu hizo ni kama ifuatavyo

Sehemu yoyote ambayo unaweza kufukuzwa muda wowote usiwekeze nguvu nyingi hapo. Sehemu hizo ni kama ifuatavyo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017

SEHEMU YOYOTE ÀMBAYO UNAWEZA KUFUKUZWA MUDA WOWOTE, USIWEKEZE ÑGUVU NYINGI HAPO. SEHEMU HIZÔ NI KAMA IFUATAVYO;​


Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kama Kichwa kinavyoeleza.
Sehemu yoyote na Mahali popote àmbapo Upo lakini unaweza kufukuzwa Muda wowote basi kiushauri sehemu hiyo usiweke Ñguvu nyingi Hapo, usiwekeze Ñguvu nyingi Hapo. usije ukaumia.

Tumia Ñguvu nyingi kadiri uwezavyo, wekeza Ñguvu nyingi kadiri ya ulivyojaliwa Mahali àmbapo hakuna wakukufukuza, yàani wewe ndiye Mmiliki wa Eneo Hilo.

Sehemu yoyote àmbayo ukigombana na wakubwa WA eneo Hilo wanauwezo wa kukufukuza, Eneo Hilo usitumie Ñguvu kûbwa na usiwe na matarajio nayo Makubwa. Ipo Siku utaumia.

Maeneo hayo ni Kama Ifuatavyo;
1. Vyama Vya Siasa.
Ikiwa unajua Kabisa wewe sio Mmiliki wa Chama hicho au Sheria haikupi mamlaka ya KUMILIKI Chama hicho kwa umilele yaani mpaka mwisho wa uhai wako. Usitie Ñguvu nyingi Sana. Usijitese kivile.

2. Madhehebu ya Dini.
Upo dhehebu Fulani, usitumie Ñguvu zako zote kujenga dhehebu àmbalo wewe sio Mmiliki Wala muanzilishi WA dhehebu Hilo.
Unaweza ukafukuzwa Muda wowote.

Kwa Sasa mambo yanaweza kuonekana Sawa lakini hiyo haimaanishi kwamba yataenda Sawa Siku zote.
Jambo ambalo Mmiliki wake NI Mwingine na sio wewe linaweza kukubadilikia Muda wowote.

Mfano, Madhehebu ya Dini yanaweza kuanzisha utaratibu mpya kinyume na misingi ya zamani na hutokuwa na lolote la kufanya. Kwa mfano Dhehebu Fulani linaweza kusema Ushoga siô Kosa na watafungisha Ndoa za mashoga. Àmbaye hataki afungashe virago aondoke.

Hutokuwa na lakufanya, kitakachokuuma zaidi ni Ñguvu nyingi ulizotumia na kuamini katika Jambo ambalo wewe sio Mmiliki.

3. Kampuni au Taasisi
Kampuni au Taasisi àmbayo wewe sio Mmiliki àmbayo Muda wowote unaweza ukafukuzwa usitumie Ñguvu nyingi kuwekeza Hapo. Fuata job descriptions ya Kazi yako, usizidishe Wala kuwa n kiherehere cha kujitoa kupita kiasi. Ili Siku ukifukuzwa au kukosewa heshima usije ukaumia na kulaumu.

4. Mtoto wa Kambo
Usije ukatumia Ñguvu nyingi kuwekeza Kwa Mtoto ambaye unajua Kabisa sio Wako Kwa kule kujidanganya kuwa ni Sawa na wako.
Huyo siô Mtoto wako na hauna mamlaka naye yoyote Kwa Sheria zozote labda Sheria za kitapeli.

Unaweza ukawekeza Kwa kiwango cha Kati ambacho hakikuumizi lakini siô kuwekeza Kwa kiwango ambacho unadhani NI kitû chako yàani Kutumia Ñguvu zako zote. Utaumia Hakika.

5. Dunia
Usitumie Ñguvu kûbwa kiasi cha kujiumiza kuwekeza Hapa Duniani Wakati unajua hata ufanyaje Ipo Siku yôte unayoyafanya na uliyonayo utayaacha na utakufa.
Fanya Kwa kiasi,

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Mkuu point no 5.....................binafsi nimeconclude kuwa hatutakiwi kuwekeza popote, si ndio? Mana 1 - 4 zote zipo duniani

Wekeza Kwa kiwango cha Kati tenà kwèñye Vitu, Jambo, sehemu au Watu unaowamiliki Kwa muda utakaokuwa Duniani.

Kuzidisha kipimo itakuumiza mwishoni Kabisa
 
Hasa kipengere #5,unajenga bar,majumba ukifa wanauza wanaenda kuonesha ufahari bar.

Kwa sie tulioamini,najenga misikiti,nanunua viwanja na mashamba naacha wosia wajenge misikiti,nachimba na visima,ah lazima nitoboe.
Unaweza kukuta umetengeneza tatizo kubwa zaidi, ukapigwa na mshangao huko unakoenda, ukabaki unalia kua mbona sio kwenyewe

No no no, can't believe it, this might be a dream.
Utakapo kuta yule mnayemwitaga mwizi wa mbao ndio yupo pale getini na kakitabu, anakwambia mbona sikujui
 
Back
Top Bottom