SEHEMU YOYOTE ÀMBAYO UNAWEZA KUFUKUZWA MUDA WOWOTE, USIWEKEZE ÑGUVU NYINGI HAPO. SEHEMU HIZÔ NI KAMA IFUATAVYO;
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kama Kichwa kinavyoeleza.
Sehemu yoyote na Mahali popote àmbapo Upo lakini unaweza kufukuzwa Muda wowote basi kiushauri sehemu hiyo usiweke Ñguvu nyingi Hapo, usiwekeze Ñguvu nyingi Hapo. usije ukaumia.
Tumia Ñguvu nyingi kadiri uwezavyo, wekeza Ñguvu nyingi kadiri ya ulivyojaliwa Mahali àmbapo hakuna wakukufukuza, yàani wewe ndiye Mmiliki wa Eneo Hilo.
Sehemu yoyote àmbayo ukigombana na wakubwa WA eneo Hilo wanauwezo wa kukufukuza, Eneo Hilo usitumie Ñguvu kûbwa na usiwe na matarajio nayo Makubwa. Ipo Siku utaumia.
Maeneo hayo ni Kama Ifuatavyo;
1. Vyama Vya Siasa.
Ikiwa unajua Kabisa wewe sio Mmiliki wa Chama hicho au Sheria haikupi mamlaka ya KUMILIKI Chama hicho kwa umilele yaani mpaka mwisho wa uhai wako. Usitie Ñguvu nyingi Sana. Usijitese kivile.
2. Madhehebu ya Dini.
Upo dhehebu Fulani, usitumie Ñguvu zako zote kujenga dhehebu àmbalo wewe sio Mmiliki Wala muanzilishi WA dhehebu Hilo.
Unaweza ukafukuzwa Muda wowote.
Kwa Sasa mambo yanaweza kuonekana Sawa lakini hiyo haimaanishi kwamba yataenda Sawa Siku zote.
Jambo ambalo Mmiliki wake NI Mwingine na sio wewe linaweza kukubadilikia Muda wowote.
Mfano, Madhehebu ya Dini yanaweza kuanzisha utaratibu mpya kinyume na misingi ya zamani na hutokuwa na lolote la kufanya. Kwa mfano Dhehebu Fulani linaweza kusema Ushoga siô Kosa na watafungisha Ndoa za mashoga. Àmbaye hataki afungashe virago aondoke.
Hutokuwa na lakufanya, kitakachokuuma zaidi ni Ñguvu nyingi ulizotumia na kuamini katika Jambo ambalo wewe sio Mmiliki.
3. Kampuni au Taasisi
Kampuni au Taasisi àmbayo wewe sio Mmiliki àmbayo Muda wowote unaweza ukafukuzwa usitumie Ñguvu nyingi kuwekeza Hapo. Fuata job descriptions ya Kazi yako, usizidishe Wala kuwa n kiherehere cha kujitoa kupita kiasi. Ili Siku ukifukuzwa au kukosewa heshima usije ukaumia na kulaumu.
4. Mtoto wa Kambo
Usije ukatumia Ñguvu nyingi kuwekeza Kwa Mtoto ambaye unajua Kabisa sio Wako Kwa kule kujidanganya kuwa ni Sawa na wako.
Huyo siô Mtoto wako na hauna mamlaka naye yoyote Kwa Sheria zozote labda Sheria za kitapeli.
Unaweza ukawekeza Kwa kiwango cha Kati ambacho hakikuumizi lakini siô kuwekeza Kwa kiwango ambacho unadhani NI kitû chako yàani Kutumia Ñguvu zako zote. Utaumia Hakika.
5. Dunia
Usitumie Ñguvu kûbwa kiasi cha kujiumiza kuwekeza Hapa Duniani Wakati unajua hata ufanyaje Ipo Siku yôte unayoyafanya na uliyonayo utayaacha na utakufa.
Fanya Kwa kiasi,
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Wewe jamaa uwa ni mwandishi mzuri uwa nasomaga mada zako japo sijawahi changia hata mada yako moja. Hii leo ni mara ya kwanza nafanya hivyo. Mada zako uwa-zinafikirisha kwa msomaji makini lazima upate kitu. Sema hii ya leo umeiandika kama mtu aliyekata tamaa. Hata hivyo naomba nikurejeshe kidogo kama wewe unamwamini Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu basi yafaa uwe na imani.
Tangu Mungu alivyotuumba ni kwaajili yake hivyo kila umuonaye humu duniani lipo kusudi la Mungu ndani mwake. Watu wengi unaowaona hawajui Mungu kawaumba ili iwe nini! Uwenda hata wewe labda hujui. Mara nyingi tunakuwa tayari kufanya kitu ili kiwe faida kwetu ni sawa lakini yafaa kabla ujajiwaza, Jiulize huyu Mungu aliyeniumba anapata faida gani kutoka kwangu? Mungu na watu wake kwanza alafu wewe baadaye Kasome kitabu cha Waamuzi kuanzia sura ya 13 - 16 juu ya habari za Samson na vita yote aliyopigana je yeye alinufaika nini hadi anakufa
Lakini ukisoma kitabu cha 1 Samwel na 2Samweli humo unakuta habari za Daudi angalau huyu alinufaika na ufalme aliupata na kuufurahia.
Nataka kusema nini wapo watu ambao tangu kuumbwa kwao Mungu amewalenga kama wachonga njia ili wengine waje wapite kiurahisi
Nimalize kwa kurjea kitabu cha Muhubiri
Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
3:2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3:3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
3:4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
3:5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
3:6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
3:7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
3:8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani. Kazi Tupewayo na Mungu
3:9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?
Mwisho kabisa nikuombe uhariri upya andiko lako maana kwa msomaji aliyekata tamaa akiliona hatapote mazima.
Hata hivyo nikushukuru maana andiko lako ndilo limenisukuma nami kuandika humu JF kwa mara ya kwanza. Barikwa sana