Sehemu yoyote ambayo unaweza kufukuzwa muda wowote usiwekeze nguvu nyingi hapo. Sehemu hizo ni kama ifuatavyo

Dunia
Usitumie Ñguvu kûbwa kiasi cha kujiumiza kuwekeza Hapa Duniani Wakati unajua hata ufanyaje Ipo Siku yôte unayoyafanya na uliyonayo utayaacha na utakufa.
Fanya Kwa kiasi,
Kuwekeza ni muhimu (kama utaweza) Ili kuwaandalia 'kesho bora' kizazi kijacho.
 
Itoshe kusema ni nondo nzuri hii bandiko..
 
Sahihi kabisa, Ujumbe huu umfikie Tundu A. Lissu popote alipo.
 
Wewe jamaa uwa ni mwandishi mzuri uwa nasomaga mada zako japo sijawahi changia hata mada yako moja. Hii leo ni mara ya kwanza nafanya hivyo. Mada zako uwa-zinafikirisha kwa msomaji makini lazima upate kitu. Sema hii ya leo umeiandika kama mtu aliyekata tamaa. Hata hivyo naomba nikurejeshe kidogo kama wewe unamwamini Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu basi yafaa uwe na imani.

Tangu Mungu alivyotuumba ni kwaajili yake hivyo kila umuonaye humu duniani lipo kusudi la Mungu ndani mwake. Watu wengi unaowaona hawajui Mungu kawaumba ili iwe nini! Uwenda hata wewe labda hujui. Mara nyingi tunakuwa tayari kufanya kitu ili kiwe faida kwetu ni sawa lakini yafaa kabla ujajiwaza, Jiulize huyu Mungu aliyeniumba anapata faida gani kutoka kwangu? Mungu na watu wake kwanza alafu wewe baadaye Kasome kitabu cha Waamuzi kuanzia sura ya 13 - 16 juu ya habari za Samson na vita yote aliyopigana je yeye alinufaika nini hadi anakufa

Lakini ukisoma kitabu cha 1 Samwel na 2Samweli humo unakuta habari za Daudi angalau huyu alinufaika na ufalme aliupata na kuufurahia.

Nataka kusema nini wapo watu ambao tangu kuumbwa kwao Mungu amewalenga kama wachonga njia ili wengine waje wapite kiurahisi

Nimalize kwa kurjea kitabu cha Muhubiri

Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

3:2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3:3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

3:4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

3:5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

3:6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

3:7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

3:8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani. Kazi Tupewayo na Mungu

3:9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

Mwisho kabisa nikuombe uhariri upya andiko lako maana kwa msomaji aliyekata tamaa akiliona hatapote mazima.

Hata hivyo nikushukuru maana andiko lako ndilo limenisukuma nami kuandika humu JF kwa mara ya kwanza. Barikwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…