INAUZWA SEIKO 5 Automatic Stainless Men's Watch Made in Japan kwenye boksi lake zinauzwa

Hiyo siyo original. Seiko bei yake siyo rahisi namna hiyo.
 
Umeshawahi kuvaa SEIKO, unazijua bei za SEIKO? Nazitoa mwenyewe JAPAN, nina uhakika nazo asilimia mia na ndio maana naziuza hapa, ni original asilimia mia kutoka Kiwandani.


Sent using Jamii Forums mobile app

Internet Purchase Warning
Seiko believes that the best way for you to select and purchase a Seiko watch is at one of our authorized retail stores. Only in these stores can you be sure to find the latest Seiko collection, and be sure that your new watch bracelet will be sized and fitted correctly, free of charge.

Seiko, therefore, recommends that you do not purchase a Seiko watch through any website, unless it is an authorized Seiko dealer with the same emblem "SEIKO AUTHORIZED DEALER SITE" as appears here on this home page.
 

Kwahiyo unamaanisha nini kwa hili tangazo lako, una uwezo wa kununua seiko kwa authorized dealer? hebu jiongeze kidogo mkuu, watu wamekuwa wakiagizia iphone China kwa watu wanaoenda china, je wale wananunua kwa authorized dealer? Kama huna uwezo wa kununua ni bora ukae kimya lakini sio kutumia nguvu zako zote na akili zako zote kutaka kuharibu biashara ya mwenzako, unapata faida gani?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeamua kuuza seiko kwa kuwa nina uhakika nazo asilimia mia kuwa ni original, sasa kama wewe una tatizo na hilo toa vigezo vya kueleweka sio hivi, huwezi kununua mzigo mdogo kwa authorised dealer na hizi saa ninazouza sio za toleo la sasa ni za muda kidogo, Babla Posta wamekuwa wakiuza Seiko miaka yote, je na wao wanauza feki? Na bei zao ni hizi hizi, Sikulaumu haujui saa na haujawahi kuvaa Seiko 5, moja ya saa zinazouzwa rahisi duniani ni SEIKO 5 za Japan.




Sent using Jamii Forums mobile app
 

Saa ghali zaidi duniani ni Rolex na saa ambazo ni bei nafuu zaidi ni Seiko 5, wahindi na watanzania wengi sana wamezivaa seiko 5 kwa kuwa sio expensive kama unavyosema wewe na ndio maana baba zetu na mababu zetu walimudu kuzivaa.

Huwezi kumkuta mtu akavaa Rolex, kama hujui sema ufundishwe mkuu, nimemkuta baba yangu akivaa seiko 5 Original, nimewakuta wazee wengi sana wa zamani wakivaa Seiko 5, ingekuwa kama unavyoongea usingeona mtu anavaa hii saa.

Saa ghali zaidi duniani ni Rolex, kumkuta mtu anavaa Rolex ni adimu, ndio maana maduka yote makubwa ya kuuza saa Original utakuta seiko 5 tu ndio wanazo na huwezi kukuta Rolex wala Omega.

Kabla hujaongea chochote kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya unachokiongea.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kuwa siyo saa za ghali. Hata mimi nawajua wazee wengi wa zamani walikuwa nazo na walikuwa siyo matajiri. Ila hilo tangazo siyo langu. Ni la kampuni mama inayotengeneza hizo saa. Bila shaka watakuwa wameshaona saa nyingi fake masokoni. Kununua bidhaa kama hizi au simu kutoka mkononi kwa mtu, mnunuzi utakuwa unanunua at your own risk. Hata hizo Iphone ukiagiza kama huko makini unalizwa mara moja. Badala ya kunilaumu ungeweza hata kufanya utafiti kama unaweza kuwa authorised dealer wao kwa Tanzania. Hapa tuko kupeana mawazo na sina mbaya na kukuharibia biashara yako.
 

At least umekubali, kabla hujaongea chochote kuwa na utafiti wa kina juu ya unachokiongea, naifahamu seiko 5 tokea niko mdogo, na ndio maana nikaamua kuziuza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii saa niliiuza hapa miaka kadhaa iliyopita kwa yoyote ambaye aliwahi kuinunua anaweza kutoa ushuhuda... Original Seiko 5 ya Japan muda si mrefu nawaletea saa nyengine aina hii hii ya Seiko 5.
 
Hii saa niliiuza hapa miaka kadhaa iliyopita... Oktoba 25, mwaka 2019... kwa yoyote ambaye aliwahi kuinunua anaweza kutoa ushuhuda... Original Seiko 5 ya Japan muda si mrefu nawaletea saa nyengine aina hii hii ya Seiko 5.
 
Kwahyo, inabidi urekebishe mda kila unapoivaa kwa wakat. Filan..?
Hapana labda uiache wiki nzima bila kuivaa, yenyewe ni automatic inajijaza ufunguo pale tu unapoivaa, unapokuwa unatembea na kurusharusha mikono yenyewe inajijaza ufunguo. kwahiyo hata wakati unapolala ukaamua kuivua na kuiweka kabatini, asubuhi unapoamka utaikuta seiko inatembea.

Pia kama hujapanga kuitumia unaweza kila baada ya siku mbili ukawa unaitikisa kidogo na itajijaza ufunguo automatic, hiyo ndio seiko 5 ya Japan.
 
 

Attachments

  • Untitled1.jpg
    133.5 KB · Views: 3
Hizo saa zote zilishauzwa muda ule ule nilipoziposti, kwa sasa muda si mrefu nawaletea mzigo mpya hapahapa, kwa wateja wapya na wa zamani wa Seiko 5 furahia kuvaa saa mpya Original kutoka hapa ya Seiko 5 ya Japan.
 

Attachments

  • Untitled1.jpg
    133.5 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…