Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Huoni division one na A's
 
Hizo ni shule maalumu kwa waliopata alama za juu tu.
Bila kujali wameibia mitihani?

Maana tunaona namna baadhi ya shule zinavyopambana kuvujisha mitihani ili tu shule ionekane inafaulisha kwa ufaulu wa juu.

Wapo watoto wanaenda hizo shule zinazoitwa vipaji maalum hadi unashangaa maana ni wa kawaida kabisa sema tu amekutana na shule yake walanguzi na wavujishaji wazuri wa pepa.
 
Unadhani ni jambo Gani?
1. Mazingira kwenye hizo shule zina/zilizoitwa vipaji maalumu.
Hizi shule hazina utafauti wowote na shule za kata tulizonazo mitaani. Kwa maana ya style ya ufundishaji, nyenzo za kufundishia na hata aina ya walimu. Ni shule hizi hizi ambazo waalimu wanaoanekana darasani kwa nadra kama kwengine kote.

Hamna jambo ambalo lipo labda kibaha/Mzumbe ukalikosa Minaki au Pugu.

2. Muendelezo
Kama serikali ilitaka kuweza kupata vipaji kutoka kwa hawa wanafunzi walioitwa maalum kungekuwa na program/utaratibu wa kuwaendeleza wanapomaliza shule za sekondari, kwa labda kufadhili masomo yao kwenye taasisi nguli za mataifa yaliyosongambele za masuala mbalimbali kulingana na fani zao, na kuendelea kuwafuatalia kuhakikisha wanarudi nchini kufanya mageuzi kwenye maeneo yao.
 
Hizo sekondari zilimepitwa na wakati kwa mtazamo wa miaka ile zinaanzishwa. Vipaji maalum inaweza kuwa shule yeyote maadamu wanafunzi wanafundishwa vema na wana IQ kubwa
 
Well, inawezekana walimu wanafanya hivi ili kuwa Test Umaalum wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…