Kwani kuwa na kipaji peke yake inatosha? Unakipaji cha kugundua dawa,ila theory zimejaa kichwani ,huna hata test tube hizo dawa unagundua vipi na kipaji chako?
Tesla,Newton, Einstein walikuwa wanatalent ila kulicho wafanya leo tuwakumbuke ni combination ya talent zao na practical walizokuwa wanazifanya kwenye mabara zao zenye vifaa vya kutosha.
Unatalenti ya kucheza mpira halafu mpira,hauna kiwanja unazani hiyo talent inakuwa vipi. Talent yoyote ili iweze kuleta faida kwa taifa lazima ijengewe mazingira mazuri, ndio maana Ulaya wana bajeti ya kutosha kuanzia kwenye maabara research centers, library na bajeti ya kutosha.
Sasa wewe nchi yako inavituo vingapi vya research? Huko mashuleni maabara zina vifaa vya kutosha? Library zina vitabu vya kutosha?