Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Mnavyo ongelea gunduzi na Innovation mnazani zinakuja na kutokea kama Uyoga, research centers ya IBM ya maswala ya Quantum Computing, kujengwa gharama yake ni USD 5bil ,kama hamvijui hivi vitu bora mnyamaze.Hao madogo wenyewe final year project bajeti wanazopewa ni ndogo ,sometimes wanatumia mpaka hela yao ya bumu,tena unakuta kiproject hakizidi hata Tsh 1m.Youtube kuna story za gunduzi kibao na maswala ya Innovation fuatilieni ndipo mtaona ugumu wake
Sababu ya Kuitwa kipaji maalumu ni nini? Si waitwe tu watu wanaofaulu sana?
 
Na mnaojua fizikia ndio kama wewe hapa ambao haujawahi hata kutengeneza hata piki piki ya makoa.😂

Na hiyo fizikia kwanza mliisoma kuijibia mitihani tu hili mfaulu vizuri, halafu mwisho wa siku mje mle mashavu kwenye serikali ya ccm.
Jamaa unawapa boko sana
 
Sababu ya Kuitwa kipaji maalumu ni nini? Si waitwe tu watu wanaofaulu sana?
Kwani kuwa na kipaji peke yake inatosha? Unakipaji cha kugundua dawa,ila theory zimejaa kichwani ,huna hata test tube hizo dawa unagundua vipi na kipaji chako?

Tesla,Newton, Einstein walikuwa wanatalent ila kulicho wafanya leo tuwakumbuke ni combination ya talent zao na practical walizokuwa wanazifanya kwenye mabara zao zenye vifaa vya kutosha.

Unatalenti ya kucheza mpira halafu mpira,hauna kiwanja unazani hiyo talent inakuwa vipi. Talent yoyote ili iweze kuleta faida kwa taifa lazima ijengewe mazingira mazuri, ndio maana Ulaya wana bajeti ya kutosha kuanzia kwenye maabara research centers, library na bajeti ya kutosha.

Sasa wewe nchi yako inavituo vingapi vya research? Huko mashuleni maabara zina vifaa vya kutosha? Library zina vitabu vya kutosha?
 
Thank you for your insight
 
Tatizo la nchi yetu ni siasa kuingilia utaalamu,,kwa style hiyo kila kitu lazima kitaharibika.
Nchi kama German imepiga hatua kimaendeleo,kwa kuweka kipaumbele katika sayansi kwa kiwango cha juu, maana mwanasayansi huwa amenyooka mda wote hana blablaa,nyeupe ni nyeupe tu,uwezi sema ni nyeusi.
Maprof wa SUA wanaandika proposals za miradi na kuomba ufadhili wa wazungu, mpunga ukiingia tu, wanajenga lodges hapo Morogoro hakuna la maana wanafanya.
 
Maprof wa SUA wanaandika proposals za miradi na kuomba ufadhili wa wazungu, mpunga ukiingia tu, wanajenga lodges hapo Morogoro hakuna la maana wanafanya.
Mkuu kwani huo mpunga unatolewa tu kama Maharage haufatiliwi kazi gani umefanya?
 
Huwezi kukalili Physics,Hesabu na Chemistry. Huwezi kwani swali moja linaweza kuulizwa kwa style zaidi ya tatu. Hayo masomo huwezi kukalili.

Hiyo Chai na ili uweze kukalili lazima ujue sentence inamanisha nini, kama ndio hivyo basi hata kujifunza hizi lugha ingekuwa rahisi.

Hii ni chai unatupanga.
Hata uulize swali kwa njia 5 kuna watu wanakunywa/wanakopi kama ilivyo mpaka nukta.
Hivi hujawahi kukutana na wale watu wanakesha kukariri hadi macho yanavimba?
 
Hata uulize swali kwa njia 5 kuna watu wanakunywa/wanakopi kama ilivyo mpaka nukta.
Hivi hujawahi kukutana na wale watu wanakesha kukariri hadi macho yanavimba?
Huwezi kukalili Physics, Math na Chemistry kwa kifupi hayo masomo matatu huwezi kukalili. Kukesha haina maana kwamba unakalili bali sayansi inavitu vungi na ili uwe fiti vyote unabidi usome na uelewe so unahitaji mda mwingi wa kusoma ndio maana watu wanakesha.
 
Hata uulize swali kwa njia 5 kuna watu wanakunywa/wanakopi kama ilivyo mpaka nukta.
Hivi hujawahi kukutana na wale watu wanakesha kukariri hadi macho yanavimba?
Kama tunaona hawa watu wa shule maalumu hawana impact tulioitarajia basi tuangalie tatizo liko wapi, the tuliondoe ili tunufaike na talanta za hawa vipanga. Tatizo linaweza kuwa sera mbovu ya elimu, uwwkezaji duni kwenye tafiti na ubunifu, siasa kupewa nguvu kubwa zaidi ya taaluma n.k kwaiyo turekebishe mfumo wetu.

Lakini hii trend ya kuwadhiaki wasomi na kuwapandisha hadhi vilaza haiwezi kutufikisha popote. Kama mfumo wetu unazalisha vipanga ambao sio competency basi hao wa madaraja ya kati na chini ndio hopeless kabisa
 
Back
Top Bottom