Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Tumejionea wenyewe kule china na mahala pengine kama ulaya Watoto wadogo wanaandaliwa kiwa Wanasayansi na mainjinia wabobezi. Watoto hao wanasukwa na kufinyangwa kiasi kwamba wanaanza kubuni na kuvumbua Mitambo na teknolojia za kipekee zenye mchango mkubwa ktk maendeleo ya kiuchumi kwenye nchi zao.

Hapa Tanzania mfumo wa Shule za Vipaji maalum umekuwepo kwa miaka mingi sasa.

Binafsi sikuwa na bahati ya Kujiunga na shule hizo hivyo nilitarajia pia kunufaika na Ubunifu/ innovations kutokana na kundi hili kubwa wenye vipaji Maalum/ special inteligence.

Tuna sekondari nyingi kama
1. Ilboru Arusha
2. Msalato Girls Morogoro
3.Mzumbe Boys Morogoro
4.Kibaha Boys Pwani
5. Tabora girls na Tabora Boys.

Ndio kusema Maelfu kwa Maelfu ya Wanafunzi waliopita humo hakuna hata wawili watatu walioonesha Ukipaji wao?

Tuseme basi Mtaji ni Mkubwa ku invest, hata Basi Kuwa Social influencer/ matumizi ya tech zilizopo je?

Tunaona Watu wenye elimu kiasi tu ndio wanaofaidi matumizi ya Technolojia na kunufaika na kuitangaza Tanzania.
Watu kama akina Maulid Kitenge, Kipanya, Zembwela, Diamond, Millard Ayo, Mwijaku, Baba Levo, Mobeto.

Angalau hawa hawakugundua chochote kama walivyo wale wa vipaji maalum ispokuwa wameweza kugundua matumizi sahihi ya teknolojia iliyopo.

Vipaji maalumu katika sekondari hizo ni vya mchongo au tunakwama Wapi?

Bonjour, Je M'apelle Bush Dokta habité à Makerere universite.

Bonvenué de discusio reun̈ion
Huoni division one na A's
 
Hizo ni shule maalumu kwa waliopata alama za juu tu.
Bila kujali wameibia mitihani?

Maana tunaona namna baadhi ya shule zinavyopambana kuvujisha mitihani ili tu shule ionekane inafaulisha kwa ufaulu wa juu.

Wapo watoto wanaenda hizo shule zinazoitwa vipaji maalum hadi unashangaa maana ni wa kawaida kabisa sema tu amekutana na shule yake walanguzi na wavujishaji wazuri wa pepa.
 
Unadhani ni jambo Gani?
1. Mazingira kwenye hizo shule zina/zilizoitwa vipaji maalumu.
Hizi shule hazina utafauti wowote na shule za kata tulizonazo mitaani. Kwa maana ya style ya ufundishaji, nyenzo za kufundishia na hata aina ya walimu. Ni shule hizi hizi ambazo waalimu wanaoanekana darasani kwa nadra kama kwengine kote.

Hamna jambo ambalo lipo labda kibaha/Mzumbe ukalikosa Minaki au Pugu.

2. Muendelezo
Kama serikali ilitaka kuweza kupata vipaji kutoka kwa hawa wanafunzi walioitwa maalum kungekuwa na program/utaratibu wa kuwaendeleza wanapomaliza shule za sekondari, kwa labda kufadhili masomo yao kwenye taasisi nguli za mataifa yaliyosongambele za masuala mbalimbali kulingana na fani zao, na kuendelea kuwafuatalia kuhakikisha wanarudi nchini kufanya mageuzi kwenye maeneo yao.
 
Hizo sekondari zilimepitwa na wakati kwa mtazamo wa miaka ile zinaanzishwa. Vipaji maalum inaweza kuwa shule yeyote maadamu wanafunzi wanafundishwa vema na wana IQ kubwa
 
1. Mazingira kwenye hizo shule zina/zilizoitwa vipaji maalumu.
Hizi shule hazina utafauti wowote na shule za kata tulizonazo mitaani. Kwa maana ya style ya ufundishaji, nyenzo za kufundishia na hata aina ya walimu. Ni shule hizi hizi ambazo waalimu wanaoanekana darasani kwa nadra kama kwengine kote.

Hamna jambo ambalo lipo labda kibaha/Mzumbe ukalikosa Minaki au Pugu.
Well, inawezekana walimu wanafanya hivi ili kuwa Test Umaalum wao?
 
Back
Top Bottom