Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Mada nzuri.
Kwa kuwa ume declear kuwa hukubahatika kuchaguliwa shule hizo basi moja kwa moja umekiri wengi huwajui na hujawahi wafuatilia.

BInafsi nawatambua vijana kadhaa waliopita shule hizo na wana mchango mkubwa kwa taifa katika nyanja mbalimbali.

Mfumo wa elimu zetu hazikutuwezesha kufanya gunduzi mbalimbali kwa sababu ya mazingira na vifaa. Lakini pia ugunduzi si mpaka urushe ndege. Matumizi sahii ya akili yako yanaweza kuleta matokeo chanya katika jamii.

Mfano juzi tumeona wanafunzi wa kibaha wakiwekeza mfumo wao wa kupiga kura kidigitali na kufanya uchaguzi.

Vipaji maalumu wengi walivyofika chuo wameendelea katika taaluma mbali mbali na pia wengi wapo na kampuni kadhaa....

Naweza kukutajia mbili tu. Anayeendesha AI ya kiswahili ni kipaji maalumu. Aliyeandika code za kampuni moja ya mawasiliano ni kipaji maalumu.

Nyerere ni kipaji maalumu n.k

Kwa namna ulivyotaja hao influencer wako ni dhahiri wewe ni mtu wa social media unayedanganywa na mafanikio ya picha.
Tatzo la watanzania wengi hudhania mafanikio ni hela nyingi au umaarufu.

Mimi nikuhakikishie tu. Kusanyiko la vilaza sio sawasawa na kusanyiko la vipaji maalumu. Kuna tofauti tu mtaonyesha kwenye kufikiri na kwenye kuamua.

Leo form 1 failure anaweza kutamba kuwa ana hela kuliko aliyesoma chuo. Lakini anasahau kuna watu behind walioweka mifumo imara inayofanya yeye apate hela.

Uvivu wa kufikiri unafanya tunakuwa na jamii isiyo na misingi imara na iliyokosa fikra timamu. Leo mtu mzima ana praise wauza uchi na machawa kuwa ndio wenye mafanikio. Huu ni ugonjwa wa akili.
 
Vipaji maalumu wengi walivyofika chuo wameendelea katika taaluma mbali mbali na pia wengi wapo na kampuni kadhaa..
Asante sana Kaka kwa mchango wako. Hii ni Mada nzuri ingependeza ukatoa na Mifano ya Watu unaowajua walionufaika na Mfumo huu wa elimu.

Tusiwafiche, hakuna sababu ya kufanya siri. Let them be Rewarded angalau tu hata kwa kuwatambua. It is a motivation kwao.
Huenda hajavumbua Mashinery tool lakini akavumbua mfumo wa mahesabu ya fedha au kuandika.
 
Uvivu wa kufikiri unafanya tunakuwa na jamii isiyo na misingi imara na iliyokosa fikra timamu. Leo mtu mzima ana praise wauza uchi na machawa kuwa ndio wenye mafanikio. Huu ni ugonjwa wa akili
Mimi nadhani umechangia wazo zuri tu hukuwa na haja ya kutukana watu.

Sasa hao wauza uchi na machawa ndio wanaoonekana. Hao unaodhani wana maana hatuwaoni. Sasa jamii ifanyeje?
 
Asante Mhandisi Mzalendo.
 
Hehehee na hii mbinu ipo?
 
Gugu kampuni inaitwa SARTIFY angalia co founder wake then gugu PAWA AI swahili ujue watu wako behind hiyo project.

Angalia mtanzania aliye NASA ni nani na katokea wapi....

Do your homework then turudi kujadiliana ila sio kwa kuweka kina Mobeto as watu wanaoku inspire wewe na generation yako.
 
Sometimes unaweza ukawalaumu ila umewawekeza kwenye Mazingira gani? Mnafacility za kulea hizo vipaji, shule zote unazo zijua wewe za Serikali zina changamoto za walimu na vifaa vya ufundishaji.Huwezi linganisha na wenzetu wa Ulaya.Wenzetu ulaya shule zina facility zote kuanzia walimu, vifaa,maabara bado wana research centers za kitosha.

Ila wapo wengi walio toka shule hizo,kwenye nchi za Ulaya na wanafanya vizuri sana.
 
Mdogo wangu ni kipaji maalum yupo form 2. Huwezi kumfananisha na average mwanafunzi wa form 2 hata wa shule ya private. Dogo anafanya coding na pia hizi vipaji maalum zina mfumo mzuri na walimu wazuri sana wa kuendeleza uwezo wa mwanafunzi.
 
100%
 
Mdogo wangu ni kipaji maalum yupo form 2. Huwezi kumfananisha na average mwanafunzi wa form 2 hata wa shule ya private. Dogo anafanya coding na pia hizi vipaji maalum zina mfumo mzuri na walimu wazuri sana wa kuendeleza uwezo wa mwanafunzi.
Yupo Shule gani? Naona ina mifumo na resources nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…