Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Kumradhi
Msalato Girls ipo Dodoma siyo Morogoro
Morogoro Kuna Kilakala na Mzumbe.
 
Huko umeenda chini kabisa je umewahi kujiuliza SUA imekusaidia nini licha ya kuwa ni chuo kikubwa na cha muda mrefu hadi sasa? Je umenufaika nacho nini?
Niliwahi kusikia waligundua Namba ya Panya kugundua Magonjwa ya TB kwenye Sample za Makohozi. Hadi leo sijajua imefikia wapi ile project
 
Asante kwa maelezo ya kina Ndugu Natafuta Ajira.
Umetaja Lecturer na Daktari hata huku wapo.

Mada hii ilikuwa inajielekeza zaidi kwenye ubunifu ili kuendana na hadi ya Neno "Kipaji Maalum"
Kwenye izo izo fani zao kuna ubunifu wanaufanya. Taarifa zao hatuna kwa sababu hatuna utaratibu mzuri wa kufuatilia watu wetu uko nje wanafanya nini, labda mpaka wanapokutana na changamoto mbaya ndio tunaamka.

Mfano mzuri nemes raymond tarimo, mtanzania mwenzetu aliekufa kwenye vita ya ukraine na urusi. Yule ni mshkaji wangu kitambo na alipata scholarship ya kusoma IT kule urusi si ajabu hata mamlaka hazikua zinajua uwepo wake kule. Kama asingekutana na yaliyomkita isingejulikana uwepo wake kule.

Kitu kingine huwa hawa vipaji maalumu ambao wengi wao ni diaspora huwa hawapendi kujitokeza kwa sababu wanakwepa siasa za afrika.

Kuna mshkaji wangu mmoja ambae ni kama broo angu alinitangulia madarasa mawili pale azania, jamaa anaishi canada na yupo vizuri, katika kuwasiliana nikamuuliza kwanini asije kuwekeza bongo? aliniambia huku kuna masuala ya uraia pacha yanakwamisha, na usipokua puppet wa wanasiasa unafanyiwa vigisu sasa kwa mtu ambae hawezi kuwa chawa ni changamoto.


Trust me mzee baba, hawa finnest wa vipaji maalumu wapo uko google, nasa, harvard n.k wanafanya mambo makubwa tu
 
Uuh! He was Great Man then.
 
System yetu ya hovyo
 

In addition hata mleta uzi anaweza fanya innovation sio jukumu la waliosoma hizo shule tu exclusively.
 
Hili ni swala muhimu sana. Kumbe tunaweza kuona jinsi Siasa zetu zinakuwa kikwakzo.
 
In addition hata mleta uzi anaweza fanya innovation sio jukumu la waliosoma hizo shule tu exclusively.
Ni kweli. Lakini tuone mifano kwanza kutoka kwao.
 
Kama MSALATO ipo Morogoro basi sawa
 
Hao ndo wanakuendeshea maisha mkuu,

Wamejaa mawizara yote, wamejaa mataasisi yote makubwa,

Kama haujui Hao ndo muhimili wa watanzania, sio wote ila like 20% wanafanya vzr na wanazibeba saana taasisi wanazozifanyia kazi
 
In addition hata mleta uzi anaweza fanya innovation sio jukumu la waliosoma hizo shule tu exclusively.
Kweli kabisa, kila mtu kwenye field yake anaweza kufanya innovation. Uwe dalali, bodaboda, mhasibu, mgavi, n.k unaweza kufanya innovation kwaiyo kabla ya kuwaangalia wengine jiangalie wewe kwanza umeongeza nini kwenye mchezo.

Mtu kama Jeff bezos yule ni winga tu alijiongeza na amazon yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…