mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
- Thread starter
- #21
PSRS kukataa kutambua testmonials lilikuwa ni pigo sana kwa wazee wa vimemo!! Kukubali kutoa kipaumbele kwa waliojitolea itakuwa ni kukubali tena kupokea testmonials ambazo nyingi ni za michongo!! Utakuta testmonial inasema "Aliyetajwa hapo juu alijitolea kwa moyo mkunjufu sana hapo TRA/bot nk kwa muda wa miaka miwili. Alionyesha umahiri na bidii kubwa sana kuliko hata waajiriwa wa kudumu. Tunashauri kwa dhati apewe ajira ili kujenga moyo wa kujitolea kwenye Taifa letu". Uozo kama huu ndio wabunge wanataka kuurudisha tena kwenye taratibu za ajira kwenye utumishi wa umma!! Msimamo ni kwamba anayetaka kujitolea mwache ajitolee, lakini kujitolea huko hakutampa kipaumbele kwenye utoaji wa ajira!!