SI KWELI Sekretarieti ya ajira wametoa taarifa kwamba walimu walio kosa maksi tano kufikia ufaulu kupangiwa vituo vya kazi kwa utaratibu maalumu

SI KWELI Sekretarieti ya ajira wametoa taarifa kwamba walimu walio kosa maksi tano kufikia ufaulu kupangiwa vituo vya kazi kwa utaratibu maalumu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
SIKWELI_AJIRA_26FEB25.jpg
 
Tunachokijua
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara huru kilichoanzishwa mahsusi kurahisisha mchakato wa kuajiri watumishi wa umma. Sekretarieti hii ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).

Kwa mujibu wa Sekretarieti ya ajira Usaili wa kada za ualimu kujaza nafasi 14,648 zilizotolewa na serikali ulianza tarehe 14 Januari, 2025 na unatarajiwa kukamilika tarehe 24 Februari, 2025 Tanzania Bara na Zanzibar. Hadi tarehe 18 Februari, 2025, jumla ya walimu 6,055 waliofanya usaili na kufaulu walipangiwa vituo vya kazi katika maeneo mbalimbali nchini baada ya kukamilika kwa mchakato wa ajira zao.

Aidha sekretarieti hiyo ilitangaza matokeo ya usaili kwa waombaji wa nafasi za kazi katika kada hiyo kwa nyakati tofautitofauti.

Kumekuwapo na barua yenye madai kuwa walimu walio kosa maksi tano kufikia ufaulu kwenye usaili kupangiwa vituo vya kazi kwa utaratibu maalumu​

Je, ni upi uhalisi wa barua hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key word search) ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli, imetengenezwa na haijatolewa na Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma kama inavyoonekana.

Aidha matumizi ya namba ya ya simu inayodaiwa kuwa ni Ajira Portal kupitia mtandao wa Whatsapp si ya kweli kwani namba hiyo imekuwa ikitumiwa katika taarifa potofu ili kuwarubuni na kufanya utapeli, rejea hapa.

Katika matangazo yake ya kuita waombaji kazi, sekretarieti hiyo imekuwa ikibainisha kuwa, kwa wale ambao majina yao hayapo katika matangazo hayo watambue kuwa hawakupata nafasi ama hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Sekretarieti ya ajira inaeleza katika mchakato wa ajira za ualimu katika utumishi wa umma kuwa Wasailiwa waliofanya vizuri katika usaili wanapata fursa ya kuajiriwa na waliofaulu na kukosa nafasi katika usaili majina yao yataendelea kuhifadhiwa katika Kanzidata ya Sekretarieti ya Ajira kwa kipindi cha mwaka na baadaye kupangiwa vituo vya kazi pasipo kurudia usaili​
Nimetoka kutazama hili tangazo nimebakia kucheka sio kwa mazuri bali ni kuona kuwa ni 2025 na bado tunaishi na watu wenye kutoa maamuzi haya.
1741092485604.jpg
 
Back
Top Bottom