Sekretarieti ya Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA imewasilisha waraka Maalumu kwa Kamati kuu ya Chama hicho ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wa CHAUMMA na mgombea Urais wa Chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Salum Mwalimu.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kwenye chumba chetu cha habari Royal Tv leo Jumatatu Juni 29, 2026, kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika ndani ya Kikao hicho cha kamati kuu, miongoni mwa wajumbe na viongozi wa Sekretarieti ya CHAUMMA taifa waliosaini waraka huo ni pamoja na Benson Kigaila, Edward Kinabo, Ismail Kangeta na Elia Gregory Mahwa.
Wengine waliosaini waraka huo kupitia kwenye Kikao hicho kinachoendelea muda huu Makao Makuu ya CHAUMMA, Kinondoni Jijini Dar Es Salaam ni Aisha Madoga, David Chiduo, Dorcas Mpatili na Mohamed Pume.
Miongoni mwa yale yaliyotajwa katika waraka huo wa kutokuwa na imani na Salum Mwalimu ni pamoja na kutokuwa muwazi katika mapato na matumizi ya Chama kufanya ubadhirifu wa fedha za chama, kubadilisha msimamo wa Chama kwa utashi na matakwa yake binafsi na kushindwa kuheshimu uongozi na kuendesha chama mithili ya mali yake binafsi.
Pesa za kupewa na TISS na CCM kwa mlango wa nyuma haiwezi kuwa ni "mapato ya chama" cha CHAUMA
Hizi yeyote anayeweza kuziwahi na kuzipokea zinakuwa ni halali yake
Salumu Mwalimu na Yericko Nyerere wamewazidi ujanja wenzao
Na ofcoz, pesa za hongo daima haziwezi kuwa mapato halali ya taasisi yoyote. Na mtu yeyote anayewahi kuzipokea kutoka kwa mhongaji, anazitia mfukoni, halazimiki kuzitolea taarifa popote kwa sbb ni RUSHWA na ni HONGO...
Kinachowatokea CHAUMA, ilikuwa ni suala la muda tu kwani kila mtu muona mbali alitegemea kitokee.
Chama cha siasa ni watu, wananchi au umma kuwaunga mkono. Ukiikosa hii, hicho inakuwa ni kampuni au taasisi ya kutafutia faida ya kifedha.
CHAUMA ndivyo ilivyo. Ni chama cha siasa kwa jina na kwa sbb labda kipo kwenye vitabu vya Msajili wa vyama vya siasa.
Lakini hii ni kampuni ya kutengenezea pesa kupitia siasa za mamluki na fitna..
Mamluki waliokimbia CHADEMA baada ya Fursa za ujasiriamali wa kisiasa kufungwa na uongozi mpya ulioingia tarehe 21/1/2025 chini uenyekiti wa Tundu Lissu, walitafuta fursa kwingine kwa kukiteka CHAUMA ya Mzee wa ubwabwa.
At the beginning, walizivuna kwelikweli toka kwa CCM ya Samia ili wasafishe njia yake ya kuingia Ikulu
Wakapewa mapesa na magari. Wakaahidiwa ruzuku na viti vya ubunge kadhaa vya majimbo na vile maalumu
Samia na CCM wakawatumia kwelikweli kama toilet paper au condom. Wamepata walichokitafuta, sasa wametupwa mavumbini na sasa zinapigwa na kutupiana lawama. Sababu, mgawo hauendi kwa usawa. Salumu Mwalimu kajimilikisha magari na mali zingine walizopewa na Samia