Emanuel leonard
New Member
- Sep 7, 2022
- 3
- 1
SEKTA YA KILiMO TANZANI KATIKA KUKUZA UCHUMI.
Kabla ya ujio wa wakoloni Tanzania, kilimo ndio ilikuwa shughuli kuu ya kiuchumi, pia biashara ambayo ilihusisha mabadilishano ya bidhaa kwa bidhaa ambapo asilimia kubwa ya bidhaa hizo zilihusiana na kilimo mfano majembe na mapanga, ambayo yalitumika katika kilimo, kilimo kilitegemewa zaidi kwani kilikuwa chanzo cha chakula na biashara ilitegemea zaidi kilimo.
Baada ya ujio wa wakoloni walitilia mkazo kilimo,waliwekeza mitaji katika kilimo Cha mazao ya biashara na chakula,walianzisha mashamba ya kahawa,karanga,katani,karafuu na mazao mengine,hasa katika mikoa ya Arusha, Morogoro na Zanzibar. Walipata faida kubwa na malighafi.
Baada ya Uhuru Tanzania pia ilizidi kujikita katika sekta ya kilimo hasa kupitia sera mbalimbali za maendeleo ya kilimo pia azimio la Arusha ambapo serikali ilitoa dira ya kilimo, kupitia kupambana na adui njaa, kilimo kilipewa kipaumbele na kuanzishwa kwa mashamba ya ushirika,vyuo vya kilimo na vyama vya ushirika kitu ambacho kiliweka msingi mzuri wa sekta ya kilimo,sera na Sheria zilitungwa ili kukuza kilimo.
Licha ya jitihada zinazifanywa na serikali kukuza sekta ya kilimo na kuifanya sekta hii ilete tija,sekta hii bado inakabiliwa na changamoto ambazo kama zitapatiwa ufumbuzi kutakuwa na ukombozi wa kilimo hivyo nchi yetu kuwa na uchumi mkubwa, zifutatazo ni changamoto zinazoikumba sekta ya kilimo.
Sekta ya kilimo haijapewa kipaumbele Kama sekta kuu ya kiuchumi ukilinganisha na sekta nyingne za uchumi. Licha ya kuwa kilimo ndio sekta kuu ya uchumi wa nchi yetu lakini bado haijapewa kipaumbele ukilinganisha na sekta nyingine, mfano, wizara ya kilimo inaonekana kutopewa kipaumbele ukilinganisha na wizara ya nyingine, hivyo kukwamisha malengo na matarajio ya sekta hii, mfano bajeti ya wizara ya kilimo haikidhi kwa asilimia zote mahitaji yake kikamilifu hivyo kukwamisha maendeleo.
Uhaba wa pembejeo za kilimo na vitendea kazi vingine vya kilimo kwa wakulima hasa kwa wakulima Wadogo Wadogo wenye mitaji midogo,Ukosefu au uhaba wa pembejeo za kilimo miongoni mwa wakulima ni sababu kubwa inayokwamisha maendeleo ya kilimo kwani pembejeo ni muhimu kwa ukuaji wa mazao,pia ukosefu wa vitendea kazi kama vile matrekta kwa ajili ya kulima na vifaa vingne vya kilimo hivyo kukwamisha maendeleo ya kilimo na kurudisha nyuma matarajio ya serikali katika kukuza uchumi.
Ukosefu wa masoko ya Uhakika kwa ajili ya kuuza mazao, pia kushuka kwa bei ya mazao katika soko la dunia ni changamoto inayokwamisha maendeleo ya kilimo katika nchi yetu,kushuka kwa bei ya mazao imekwamisha maendeleo ya kilimo kwani wakulima hawana Uhakika wa bei ya mazao yao sokoni hivyo kushindwa kuzalisha kwa wingi kwani hawana Uhakika wa masoko,mfano kupanda na kushuka kwa bei ya kahawa ni changamoto kwa wakulima wa kahawa hivyo kukwamisha uzalishaji.
Ushirikishwaji mdogo wa sekta binafsi katika sekta ya kilimo ni changamoto kubwa ambayo hupelekea ushirikiano mdogo kati ya sekta hizo mbili kwani sekta binafsi Ina mchango mkubwa sana katika kuchochea maendeleo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiweno maendeleo ya kilimo hapa tanzania,taasisi na mashirika binafsi yanashindwa kuwekeza katika kilimo kutokana na kutowekewa mazingira mazuri ya kuwekeza hivyo kushidwa kukidhi matarajio.mfano kushindwa kufanya tafiti za kisayansi mwenye kilimo.
Mfumo wa elimu kutokidhi mahitaji ya sekta ya kilimo, mfumo wa utoaji elimu hupelekea uhaba wa wataalamu wa kilimo.mfumo wa elimu pia ni kikwazo katika ukuaji wa sekta ya kilimo kwani mfumo wa elimu uliopo umeshindwa kutoka wasomi au wataalamu wa kutosha wa kilimo ambao watasaidia katika kukuza sekta ya hii,mfumo wa elimu unaotumika huzalisha wataalamu wachache ambao hawakidhi mahitaji ya sekta mzima ya kilimo hivyo kukwamisha maendeleo ya kilimo kiujumla.
Uwezeshwaji mdogo wa vijana katika sekta ya kilimo na suala la uelewa mdogo wa wakulima juu ya masuala sayansi na teknlojia katika kilimo. Hii ni changamoto nyingine inayokumba sekta ya kilimo,ukweli ni kwamba idadi ya vijana katika sekta ya kilimo ni ndogo kwa sababu serikali haijaweka mazingira wezeshi kwa vijana katika kilimo kama vile kutoa mikopo yenye riba nafuu na ya Uhakika kwa vijana. pia wakulima kushindwa kwenda na Kasi ya maendeleo ya kiteknolojia,ambapo vijana ndio Wana uelewa mkubwa juu ya mambo ya sayansi na teknlojia lakini hawajawezeshwa,hivyo kushindwa kuleta maendeleo Katika sekta ya kilimo.
Uwepo wa migogoro ya mara kwa mara inayohusisha moja kwa moja sekta ya kilimo hivyo kuathiri sekta hii kwa kiasi kikubwa. Kumekuwa na uwepo wa migogoro ya ardhi ambayo inahusisha sekta hii,migogoro hii huathiri kwa namna moja au nyingine ukuaji wa sekta hii.mfano migogoro kati ya wakulima na wafugaji,wakulima na watunza maliasili kama vile misitu na hifadhi/mbuga za wanyama au wakulima na hifadhi za Barabara na huduma za kijamii kama vile shule na hospitali hivyo kuathiri moja kwa moja sekta hii ya kilimo, kwani kilimo hutegemea zaidi ardhi kama nyenzo kuu,hivyo migogoro ya ardhi hupelekea kukwamisha maendeleo ya kilimo.
Mapendekezo yangu na ushauri kwa serikali na taasisi zinazohusika.Ili kukuza sekta ya kilimo ni muhimu kuwa na jitihada za pamoja yaani ushirikiano wa pande zote kuanzia serikali,wananchi ambao ndio wakulima na sekta binafsi pamoja wadau mbalimbali wa kilimo katika jitihada zote za kukuza sekta ya kilimo, lakini pia serikali inapaswa kutafuta suluhisho la kudumu juu ya migogoro ya ardhi inayohusisha wakulima kwa kizingatia mpango wa matumizi Bora ya ardhi na kuweka vipaumbele katika sekta hii ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kilimo na njia nyinginezo, lakini zaidi ni jukumu la serikali kuhakikisha sera zote,Sheria namikakati iliyowekwa kwa ajili ya kukuza kilimo izingatiwe pia sera na Sheria nyingne zifanyiwe marekebisho ili kuendana na Kasi ya maendeleo kidunia ili kuleta mabadiliko chanya. Kwani sekta ya kilimo ni muhimili muhimu kwa uchumi wa nchi na mtu mmoja mmja na sekta nyingine kama vile biashara ambayo hutegemea sekta ya kilimo. Lengo kuu ni kukuza uchumi wa nchi yetu.
Ahsante;
jina: Emanuel Leonard Petro.

Upvote
1