KERO Selcom inatukata pesa nyingi kama 'penalty' kila unapokosea muamala

KERO Selcom inatukata pesa nyingi kama 'penalty' kila unapokosea muamala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni selcom penalty, Selcom ulikuja kama mtandao (mobile wallet) mbadala kutokana na kuwa na makato madogo.

Ila kwa sasa hali imebadilika umekua ni mtandao wa kukata watu hovyo ukifanya muamala imepelea hata shilingi moja pengine kwa kujua au kutokujua hawatumi meseji kuwa salio halitoshi.

Badala yake wanakukata 1500 kama faini na wanasubiri ukosee ata mara 2 kila unapokosea chochote kwenye muamala unaofanya ni 1500 na meseji zinachelewa kufika makusudi ili ukosee mara nyingi.

Kwanini wasitume meseji kwanza kwamba salio halitoshi au ukikatwa mara moja usiendelee mpaka urekebishe makosa yako Unakatwaa pesa nyingi kuliko ulizotaka kufanya muamala.

Terms zinasema unapata meseji kwamba kwanini muamala wako umefeli na zinakuja kupitia notification zao za apk maajabu hyo text inakuja kuchalewa masaa mengi na ya kukata muamala inakuaja punde wanafanya kuvizia ukosee mara kadhaa malipo ya mtandaoni wanakwama sana.

Mwisho hata kama terms zingekua hivyo hapa tunaelezea kero ata kama imehalalishwa ili iwe fixed.
 
Sijaelewa kwa kweli, kama Salio halitoshi maana yake muamala hauendi, Sasa unakatwa vipi,

Mimi natumia selcom microfi. Bank nawaona kama wanamapinduzi kwa unafuu wa Makato,
 
Huu ni wizi wa wazi kabisa aiseeee....
Mfano mmekosea watu 10,000 na kila mmoja amekatwa 1,500 nisawa na wanaiba 15,000,000.
Tena hizi ni free soft money ambazo hazikatwi hata kodi, hii nchi kila mahali ni wizi aiseee...😮‍💨
 
Sasa unakatwaje pesa na salio lako halitoshi ?

Fafanua vizuri hapo ?
Unataka kutuma laki moja na iliyopo ni elfu tisini kamili. Inakuogema alaf wakat huo elfu tisini ile wanakwangua
 
Unataka kutuma laki moja na iliyopo ni elfu tisini kamili. Inakuogema alaf wakat huo elfu tisini ile wanakwangua
wanakwangua inaenda wapi kwenye muamala kulipokusudiwa au wanachukua wao
 
Hao ni matapeli achana nao mie walikula elfu 40 yangu hao toka mwaka jana hadi leo sijapewa pesa yangu
 
mhh,mbona wengine tupo huko na hatushuhudii hayo mambo? umelipwa?
 
Back
Top Bottom