Sele Bonge akamatwa kwa wizi wa TV na gari

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limemkamata Seleman Kalembo, maarufu kama Sele Bonge na wenzake 9 kwa tuhuma za wizi na kuwakuta wakiwa na gari aina ya Noah vifaa mbalimbali vya kuvunjia nyumba, TV nne pamoja na mfuko wa kufichia TV baada ya kuiba.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Wiliam Mkonda, amesema jeshi hilo liliendesha operesheni kali baada ya nyumba nane kuvamiwa na kuibiwa vitu maeneo ya Kinyerezi, Kibaga usiku wa kuamkia Septemba 6, mwaka huu.



 
Sasa mbona sisi wa huku vijijini hatuna taarifa za kutosha kuhusu huyo Sele Bonge!! Ni nani huyo huko kwenu Darisalama?

Maana watu wa Dar hamna dogo.
Ni jamΓ a mmoja anaewajulia sana wanaume wa daslamu na viunga vyake.....anawakaangia chips tamu, na broiler bila kusahau chachandu mayonaizi na ukwaju
 
Sele bonge ni wengi na sio sele bonge naye mjua muuza biryani leo tuu katoka nipakulia kisinia cha biryani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…