William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Kuandamana?? nani afanye huo ujinga wa kupigwa mabomu kwa kumsemesha kiziwi JK asiyeona hata nchi inakokwenda yeye anaona sawa tu
Mimi naona kamati ilifanya kile kilichotakiwa, wewe ukiitwa mahakamani akakata mahakama ina mawili ya kufanya kuhukumu kesi bila ushahidi wako au kukulazimisha kutoa ushahidi wako.RA alikataa kutokea kwa hiari yake; kamati ya bunge ilikuwa na nguvu na uwezo wa kutumia njia zingine halali kisheria kuwalazimishiwa watuhumiwa kuhojiwa.
Kama wahusika wakubwa kwenye hili ni Lowassa na RA, ninashangaa kweli hii kamati ilishindwa kutumia nguvu zake kisheria kuwahoji hawa watu. Maneno ambayo wangeyasema mbele ya hicho kikao, yangelikuwa na nguvu na ingelikuwa hata rahisi kuwachukulia hatua za kisheria.
So according to you mtetezi wa mafisadi if nothing is happening then we should all forget about mafisadi who're plundering the wealth of our beloved country while millions of our fellow Tanzanians are living in very poor conditions.
Kanywe Tusker wewe fisadi ambaye unataka RICHMOND ipotee katika mijadala ya Watanzania ili muendelee kuchota mabilioni. Watu wengine kwa kujikweza bwana! Duh! Who do you think you are!? Wabunge ambao ni wawakilishi wa Watanzania katika majimbo mbali mbali walikaa kumsikiliza Selelii bila kuchoka lakini wewe fisadi umeshachoka na sijui kauli yako hapa inamuwakilisha nani!? na huu mjadala wa RICHMOND unakukera sana unataka uachwe ili watu wakanywe Tusker! 😕 Kweli ukistaajabu ya Mussa...... Na wewe utajidai una mapenzi ya kweli na nchi yako wakati hutaki ufisadi uliokithiri ndani ya Tanzania ujadiliwe! Kanywe Tusker zako na tuache sisi tunaotaka kujadili hali ya nchi yetu tufanye hivyo.
............- Haya maelezo yote aliyoyatoa Seleli yamo kwenye ripoti yao ya kamati,
Respect.
FMEs!
Mkuu napenda kusisitiza hilo hapo juu kuwa ni sahihi,...........watch out though kuna watu wana ajenda zao hapa...........na hii ni hatari
- Bunge limetimiza kazi yake, sasa wewe utueleze unataka nini hasa? The only thing wananchi we can do hapa ni kuandamana kuwashinikiza Rais na Waziri Mkuu kuchukua hatua kufuatilia mapendekezo ya bunge, ikibidi kuwazomea na kuwarushia mawe unakumbuka last time haya yalipofanyika Mramba na Yona wakapelekwa Rumande kutunyamazisha!
- Sasa wewe utueleze unataka nini maana bunge limemaliza kazi yake tayari on the ishu?
FMEs!
Bunge limepewa mamlaka ya Kuidhinisha mipango yoyote ya muda mfupi au mrefu ya JMT. Katika kuidhinisha linanguvu ya kukataa kubadilisha au hata kutoa maelekezo ya nini kifanyike. Na likikataa (nguvu yake ya kusimamia) serikali (RAis) hawezi kuendelea na mpango huo. Wabunge wasipojua nguvu yao hii ndio sababu serikali wakati mwingine inajifanyia tu mambo yake.
Msingi wa nguvu hii ni kuwa Bunge ndio wawakilishi wa watu siyo Rais. Falsafa nzima ya utawala wa demokrasia ni kuwapa nguvu watu siyo mtu mmoja. Ndio sababu ya Magna Carta, mapinduzi ya Ufaransa na yale ya Marekani.
Katika Tanzania wabunge wetu wanataka kupoteza nguvu hii na kumwachia Rais cheki isiyojazwa. Hatuwezi na hatupaswi kuwaacha wabunge waache jukumu lao la kuisimamia serikali na hata kuilazimisha serikali kufanya kile sisi wananchi tunataka wafanye. This amounts to relegation of duty.
Kama serikali inaweza kufanya lolote bila kulazimishwa au kusimamiwa na Bunge, basi hatulihitaji Bunge! what for? kupitisha bajeti tu? Rais si anaweza kufanya hivyo yeye mwenyewe?
samahani kama tutakuwa tumipishana kwenye dhana ya post yako hapo juu aidha yapo sawa, au yapo tofauti, ni kwamba Kamati ya Bunge au Bunge halina mamlaka ya kuhukumu, labda hiyo kamati iapishwe kwenda kusimamia issue na kui-hukumu, lazima tutofautishe bunge linapo kaa kama kamati ya uchunguzi au ya kutoa hukumu. na hili litaelezwa kwenye hadidu za uundaji wake. Na kama wanatakiwa kuhukumu ni lazima waapishwe kutekeleza hilo.By M.M.Mwanakijiji
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lele-za-kingunge-hazininyimi-usingizi-11.html
Mkuu ukisoma post namba 104 utajua kazi na Mamlaka ya bun
Mkuu wangu nawe unaingia mkumbo huu...Mkuu Mkandara,
Ni kweli wananchi tunataka ukweli; tunataka ukweli wote na wala sio nusu nusu.
Hayo ndio mambo ambayo walitakiwa kuyaweka kwenye report ya Richmond lakini hawakufanya hivyo, why?
Kwenye uchunguzi wowote, watu wanasema follow the money? Sasa kama walijua hata fedha zilikuwa zinatumwaje na nani alikuwa anafuatilia, mbona hiyo ndio ingelikuwa taarifa muhimu zaidi?
Kama wanachoandika sasa ni sahihi, ilikuwa muhimu mno kumhoji Rostam maana mahojiano chini ya kiapo cha bunge yangelikuwa na maana zaidi, huko ndiko kungelikuwa ni kumfunga paka kengere. Nashangaa pamoja na info wanazotoa sasa, walishindwa kutumia nguvu ya bunge kuwahoji hawa wahusika. Hata kama Rostam asingeenda kuhojiwa kwa mapenzi yake, kuna njia zingine ambazo zingemlazimisha yeye kuhojiwa.
Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.
Miaka mitatu tunapiga mduara kwenye jambo moja huku hali ya umeme inazidi kuwa duni na kuathiri uzalishaji na huduma zingine. Ifike mahali tulimalize hili suala na kuhangaika na mambo mengine kwa faida ya wananchi wote.
Hii kamati ya Richmond wasalimishe documents zote walizo nazo kwa spika na polisi, ili vyombo vya umma vizipitie na kuchukua hatua pale inapobidi. Kutoa habari nusu nusu kwa faida zao kisiasa ni abuse of power. Walipewa hiyo kazi kwa niaba ya bunge na wananchi. Wanatakiwa kutuambia wananchi ukweli wote na hawana haki ya kuficha baadhi ya documents.
Mtanzania said:Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.
Hayo ndio mambo ambayo walitakiwa kuyaweka kwenye report ya Richmond lakini hawakufanya hivyo, why?
Kama wanachoandika sasa ni sahihi, ilikuwa muhimu mno kumhoji Rostam maana mahojiano chini ya kiapo cha bunge yangelikuwa na maana zaidi, huko ndiko kungelikuwa ni kumfunga paka kengere. Nashangaa pamoja na info wanazotoa sasa, walishindwa kutumia nguvu ya bunge kuwahoji hawa wahusika. Hata kama Rostam asingeenda kuhojiwa kwa mapenzi yake, kuna njia zingine ambazo zingemlazimisha yeye kuhojiwa.
Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.
Miaka mitatu tunapiga mduara kwenye jambo moja huku hali ya umeme inazidi kuwa duni na kuathiri uzalishaji na huduma zingine. Ifike mahali tulimalize hili suala na kuhangaika na mambo mengine kwa faida ya wananchi wote.
Hii kamati ya Richmond wasalimishe documents zote walizo nazo kwa spika na polisi, ili vyombo vya umma vizipitie na kuchukua hatua pale inapobidi. Kutoa habari nusu nusu kwa faida zao kisiasa ni abuse of power. Walipewa hiyo kazi kwa niaba ya bunge na wananchi. Wanatakiwa kutuambia wananchi ukweli wote na hawana haki ya kuficha baadhi ya documents.
Kwa hiyo lawama zote unawashushia kamati ya kina Selali na Wapiganaji! yaani sielewi mkuu wangu point yenu hasa ni ipi.Mkandara,
..vyombo vya sheria vipi ndugu yangu?
..Rostam anafuatilia malipo ya Richmond/Dowans mpaka Hazina halafu unaleta habari za vyombo vya sheria?
..kinachoendelea hapa ni jitihada za kumrudishia Rostam pesa zake alizotumia kwenye kampeni za wanamtandao.
Mkandara,
..vyombo vya sheria vipi ndugu yangu?
..Rostam anafuatilia malipo ya Richmond/Dowans mpaka Hazina halafu unaleta habari za vyombo vya sheria?
..kinachoendelea hapa ni jitihada za kumrudishia Rostam pesa zake alizotumia kwenye kampeni za wanamtandao.
Mtanzania,
..I am 100% with you on this one.
NB:
..Waswahili wana msemo wao "majuto ni mjukuu."
..wakati tunamchagua JK, hatukufikiria kabisa atamlipa vipi fadhila za Rostam Aziz .
Ndugu yangu Mtanzania,
Ulisoma report yote ya Mwakyembe ama ulisimuliwa? Uliona viambatanisho vyote vya hiyo report? Kwanini unasema kwamba haya yaliyoandikwa kwenye gazeti la MwanaHalisi ama kwa maneno mengine maneno aliyoyasema Mbunge Selelii hayakuwamo kwenye report?
Kwenye kipengele walichokuwa wanaeleza kwanini walitaka kumhoji RA, walisema wazi kwamba kuna vitu walikuta ambavyo ni vya Caspian lakini vilikuwa vinatumiwa na Dowans, mfano, anuani ya posta, e-mail address, na baadhi ya wafanyakazi wa Caspian walikuwa ni wafanyakazi wa Dowans. Leo hii unakuja kutuambia haya hayakuwamo kwenye report? Hapa sikubaliani na wewe, ndiyo maana nikasema labda hukusoma report yote.
Au ulitaka waandike kwenye report kwamba walimshirikisha Rais? Kwamba walifanya utaratibu gani kumpa report mapema?
Mimi nina amini kwamba kilichoandikwa ni sahihi na ndiyo maana Lowassa hakutaka kujibu hoja zao akakimbilia kujiuzulu. Kumbuka kwamba alipewa report a day kabla ya kuwasilishwa, so he had more than 48 hrs za kuipitia na kuangalia kama anaweza kujibu hoja. Kama hakuhusika na kwa jinsi ninavyomfahamu, angepangua hoja moja baada ya nyingine. The problem ni kwamba alishajua hana ubavu wa kujibu hoja hizo. Matokeo yake akaishia kujibu report kwa staili ya Sofia Simba (mipasho style) kitu ambacho kimeharibu jina lake mpaka leo na ndio maana ana haha kuangalia namna ya kujisafisha.
RA alikwepa kwa makusudi kabisa kuhojiwa na hiyo kamati kwa kuwa hakujua jamaa wana info kiasi gani na angejipeleka angejimaliza mwenyewe, ndipo akaja na hiyo janja janja ya kujifanya ana safari za kibiashara. Lakini ukweli ni kwamba aliwakwepa, hakutaka kwenda kichwa kichwa bila kujua jamaa walikuwa wanafahamu nini.
Wameanza kugombana lini? Wameanza kugombana leo? Report ni ya 2008, na yalisemwa hayo yote na kuna viambatanisho lundo ambavyo hata sisi wengine hatujui vina nini. Ulitaka waseme nini?
Ni kwa kuwa Kikwete na serikali yake wanaendelea kupiga chenga na wanaonekana kuzidiwa nguvu na mafisadi ndiyo maana bado tunaendelea kuongelea Richmond ambayo ilitakiwa iwe imemalizwa tangu mwaka jana, may be serikali ilihitaji miezi 6 kusafisha kila kitu. Hujiulizi kwanini wale wote ambao walitakiwa kuchukuliwa hatua mamlaka zao wameishia wameishia kustaafu, hata kama ni kabla ya umri wao. Bado utawabebesha wabunge lawama hizo?
Pendekezo lako la mwisho limeniacha hoi, hivi wewe bado una imani na Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU?
Kwani TAKUKURU walipofanya kazi hiyo mara ya kwanza walikuja na report gani? Excuse wanayotupatia ni kwamba walitumia sheria ya TAKURU and the deal was clean. Hivi pamoja na huu uchafu wote Lawyer Dr. Hoseah anaweza kuja kusema mbele za watu kwamba the deal was clean?
Tuje kwa Usalama wa Taifa, JK alijitetea kwamba alizuwia malipo akihisi kwamba inaweza kuwa ni kampuni fake. Je, Usalama wa Taifa walikuwa wapi kufanya kazi ya kuchunguza kama kampuni hiyo ilikuwa ni genuine ama fake? Kweli Rais wa nchi anashitukia deal, Usalama wa Taifa wamelala! Kwanini hawaku-act immediately baada ya kuona kelele zimezidi kwenye magazeti? Mpaka mtaalam RA akashituka na kuweka watu waliobobea kupika majungu akina Salva ili kusafisha hali hewa, UwT wao wapo tu, hao ndio wapelekewe documents ili waende kuzi-destroy? Kwani hivyo vyombo vya dola havijui akina Mwakyembe walipata wapi hizo documents? Wao kama wako serious si wangetumia hizo leads za report ya Mwakyembe ili kufuatilia na waanze kuwashughulikia wale wote waliohusika.
Wabunge na Kamati ya Mwakyembe walifanya kile walichoweza kufanya, tatizo ni serikali yetu inalinda mafisadi kwa nguvu zote na hili limejidhihirisha kwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge. Hakuna hata moja lililofanyika, yote ni usanii kwa kwenda mbele na bado wanapiga chenga mpaka leo.
Pinda alipochukua kiti cha PM alisema angepeleka report yeye mwenyewe na kwamba apewe miezi 6 tu. Leo ni miezi karibu 18, hakuna kitu. Labda wanasubiri Hoseah afikishe umri wa kustaafu ndipo wataenda kupeleka report Bungeni.
Mkandara,
..we will never get to the bottom of this scandal.